Kesi ya viongozi Chadema yaanza kwa vituko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya viongozi Chadema yaanza kwa vituko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 22, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha; Tarehe: 21st October 2011

  KESI ya kufanya maandamano bila kibali inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na wafuasi wao 19, jana ilianza kusikilizwa huku wafuasi wa chama hicho wakiguna na wakati mwingine wakicheka wakati wakili wa Serikali, Edward Kakolaki akisoma maelezo ya makosa wanayoshtakiwa nayo.

  Aidha kesi hiyo ilibidi iahirishwe kwa dakika 10 kutokana na mabishano kati ya Mawakili wa Serikali na mawakili upande wa washtakiwa wakiongozwa na Method Kimomogolo kutokana na wakili wa serikali, Kakolaki kukataa kusaini Mashtaka.

  Wakili huyo alikataa kusaini mashitaka ambayo wanakubaliana nayo na yale ambayo wameutaka upande wa Serikali kuwathibitishia kwenye hati ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao 19, hatua iliyosababisha Hakimu Charles Magesa kuwapa muda ili wamalize tofauti hizo.

  Akisoma hati ya mashitaka, Wakili Kakolaki alisema Januari 3 hadi 5, mwaka huu katika Manispaa ya Arusha, Chadema ilikusudia kufanya mkutano wa hadhara viwanja vya NMC vilivyopo Unga Limited na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alimtaarifu Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) Zuberi kusudio hilo la kufanya mkutano huo kwa barua yenye kumbukumbu namba CDM/ AR/ W/10/ 2010 na kuanisha njia watakazopitia.

  Kakolaki alisema baada ya kumtaarifu OCD njia watakazotumia ilibainika kuwa si sahihi kuruhusu maandamano hayo kwa vile yangeweza kuleta usumbufu kwa wapita njia kwani hali halisi ya miundombinu ya Jiji la Arusha ni finyu na OCD aliwajulisha Chadema kuwa njia walizochagua si sahihi hivyo wapite njia nyingine lakini walikaidi ushauri huo na kupita njia walizopanga awali katika barua yao.

  Hakimu Magesa kabla ya kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 25, mwaka huu alilazimika kutoa maelezo kwa wafuasi wa Chadema kuwa Mahakama ina taratibu zake na lazima ziheshimiwe kwani imezuka tabia ya watu kucheka, kupiga makofi na wakati mwingine kuzungumza wakati mahakama inaendelea.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wape Wengi Haki Zao!!!
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hii story haina hitimisho? au nawe umechakachua, jitahidi kuikamilisha ili hatima yake iwe wazi ilikuaje au iliondoka mapema

  kimsingi umeeleza vizuri ila hitimisho tu
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Sijui ni kesi au ni stori ndio haieleweki!?
   
 5. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mwandika thread alipokuwa anaandika alivamiwa na majambazi akapigwa roba ndyo maana kashindwa kumalizia thread na jambazi nalo likapost bila kumalizia thread.
   
 6. M

  Mzalendoo Member

  #6
  Oct 22, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ntarud waheshimiwa.
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hawa mende wa cdm wakipatikana na hatia wapigwe mvua kumi
   
 8. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Nachompongeza Nape ni kuwalipa pesa yenu kwa wakati.
   
 9. IGUDUNG'WA

  IGUDUNG'WA JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 1,998
  Likes Received: 887
  Trophy Points: 280
  humu ndani magamba yananiudhi kinyama maana hata jambo la wazi yanaibuka na upuuzi wao. hii kesi ya kutungwa na ccm haina maana yoyote wanawapotezea muda makamanda wetu
   
 10. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe kitu unachokiweza ni kulewa mbege tu. Nothing more.
   
Loading...