DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu inaendelea tena leo, Jumatano Oktoba 22.2025, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam kama ilivyo kawaida chini ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa kwa mfululizo, haikusikilizwa hapo jana kufuatia uwepo wa mapingamizi yaliyokuwa yamewekwa na mshtakiwa ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo, ambapo miongoni mwa mapingamizi hayo aliyoyawasilisha mwishoni mwa juma lililopita ni pamoja na lile linalohusu kupinga Mahakama kupokea 'Flash Disk' na 'Memory Card' kama kielelezo kutoka kwa shahidi wa tatu (3) wa Jamhuri Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Samwel Elibariki Kaaya
Ikimbukwe kuwa, upande wa Jamhuri uliitumia siku ya Jumatatu ya juma hili kujibu mapingamizi hayo, na Mahakama kutumia siku ya jana kupitia hoja za pande zote mbili na kuandaa uamuzi
Kesi hiyo inatajwa Mahakamani hapo hapo leo, ambapo pamoja na mambo mengine Mahakama itatoa 'uamuzi mdogo (rulling)' wa mapingamizi hayo, lakini pia shahidi wa tatu (3) wa Jamhuri Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Samwel Elibariki Kaaya ataendelea kutoa ushahidi wake.
Pia Soma: Kesi ya Lissu: Mahakama Kuu kutoa uamuzi mdogo Septemba 22
Mwanaume mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika ameleta taharuki mahakamani baada ya kusikika akiwataka majaji wamsikilize kwa vile yeye ametumwa na Mungu.