Kesi ya uchaguzi Kati ya mh. zaituni buyogera vs Nsanzugwanko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya uchaguzi Kati ya mh. zaituni buyogera vs Nsanzugwanko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kajunju, Apr 4, 2012.

 1. k

  kajunju JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Leo nimebahatika kuhudhuria kesi ya Nsanzugwanko dhidi mh. Zaituni Agripina buyogera mbunge wa kasulu vijijini.kumbuka leo mh. Zaituni ndipo alikuwa anatoa ushahidi wake dhidi ya tuhuma zilizotolewa na nsanzugwanko kuwa alimtuukana kuwa ni mchawi,alimuua marehemu teddy magayane na bernad machupa aliyekuwa mgombea udiwani wa mwali,ccm ni chama cha mafisadi. Kesi inasikilizwa na jaji aruna muroso(kama sijakosea jina) na mawakili wa serikali ni advo rweyongeza, Advo…ndamgoba(kama sijakosea jina) na advocate rweyemamu anayemwakilisha mh zaituni buyogera. Ndugu Nsanzugwanko anawakilishwa na advocate musa. kesi ilianza kwa mh. Zaituni kuongozwa na wakili wake • Advo…rweye….Uliwai kutolea kashfa Nsanzu kama alivyoeleza kwenye mashtaka yake?? • Mh. Zai….sijawai.Mashitaka haya ni kwa kuwa nilimshinda kwenye uchaguzi. • Advo rweye ..Je unamfahamu nsanzugwanko? • Mh. Zai..ndiyo..ninamfahamu.alikuwa mgombea ubunge nccr mwaka 2000.alikuwa boss wangu nccr na alinisfundisha siasa.mwaka 2002 alihamia ccm.mwaka 2005 niligombea nae ila mimi kura hazikutosha • Advo rweyi…unamfahamu benard machupa?? • Mh. Zai…..namfamu alikuwa mgombea udiwani wa kata nyachenda/mwali.alifariki tarehe 9/10/2010 na ilibidi tusimamishe kampeini kwa siku tatu. • Advo rweyi….Ulimtuhumu nsanzu kumuua Bernard machupa tarehe 7/10/10 unasemaje? • Mh. Zai..si kweli haya ni majungu.nitasemaje kuwa bernad aliuawa na nsanzu tarehe 7/10 wakti alifariki tarehe 9/10?haya ni majungu • Advo zai….ulitoa tuhuma za wizi na mauaji wakti huko zeze.tuhuma hizi unazisemaje? • Mh. Zai…si kweli.kata hii sisi ndiyo tulikuwa na diwani.mimi niliongelea zahanati ikizingatiwa kata hii ilikuwa na majengo pasipo mganga.watu wa eneo hili walikuwa wanaenda jimbo la kigoma kusini kijiji cha nyanganga. • Advo rweyi..sera zako zilikuwa zipi? • Mh zai….nilitumia irani ya nccr na vipaumbel vyangu ilikuwa ardhi,elimu,afya,barabara na kilimo • Advo rweyi…mwisho kabisa unamwambia nini jaji? • Mh zai…naomba mahakama initangaze mimi ndiye mbunge,pili alipe gharama za kesi hii • Advo rweyi…Unaujua ugomvi wa nsanzu na mwenyekiti ndaheza? • Mh. Zai…sijui. Baada ya muongozo huo advo rweyongeza alitaka kufahamu kama aliwai lalamikiwa sehemu yoyote hile na mh. Zai alikanusha kabisa. Jaji alimruhusu advo musa aanze kuuliza maswali nayo yalukuwa kama ifuatavyo • Advo musa…..Elimu yako? • Mh. Zai…nilimaliza std 7 mwaka 1983 • Advo musa…..mtoto wa kwanza ilimzaa mwaka gain? • Mh. Zai….nilimzaa mwaka 1985 • Advo musa……..taja majina yako • Mh. Zai…naitwa Zaituni agripina buyogera • Advo musa…..Jina la baba yako? • Mh. Zai…anaitwa athuman buyogera • Advo musa….nyumbani kwenu kuna zaituni wangapi? • Mh..zai…tuko wengi kwani hakina zaituni • Advo musa..kwanini uitwe zaituni..ubini wa baba yako haupo? Mh jaji ameingilia kati. Wewe usiingilie mambo ya familia ohh ana wake wangapi baba,kwanini mnaitwa zaituni agripina.malalamiko haya ungepeleka kwa wale wa uzazi na vifo ili watupe maelezo ya majina haya.tunataka ushahidi siyo kupoteza muda. Advo musa anakubali ngoma inaendelea. • Advo musa…Unajua kiingereza? • Mh. Zai…mimi sijui kiingereza najua Kiswahili • Advo musa…kwanini ulikuwa unaenda na vitabu hasa kijani kwenye kampeini? • Mh..zai…nilikuwa naenda na kitabu cha buruu ambacho ni irani ya nccr na kingine ilikuwa ratiba ya mkutano. • Advo musa…sera zako ulizitoa wapi?? • Mh. Zai…nilizitoa kwenye irani ya nccr • Advo musa…tusomee mahali zilipo • Mh. Zai..sisomi ila zimo humu Jaji ameingilia kati kwa kumwambia advo musa,hatutaki kusoma kitabu hapa.chama kinaweza kuwa na sera 30 lakini huyu alitoa zinazomfaa.awezi kueleza sera ya bahari wakati kasulu hakuna bahari. Advo musa endelea • Advo musa. Kabla ya kufunga kampeini.siku moja kabla kule rungwe mlifanya maandalizi nccr.je ni maandalizi gain? • Mh. Zai…mimi sijui ya 29/10 najua mkutano wa 30/10.ukienda mkutanoni unakuta watu wameishaitwa . • Advo.musa…kuna umbali gain toka nyumbani kwako hadi ofisi ya ccm • Mh. Zai…sijui labda km au mita??/sijui. Labda kama hapa na kituo cha polisi. Jaji anaingilia kati kujua umbali naanawauliza maaskari umbali nao wanasema ni kama 0.5 hadi km 1. Baada ya kumaliza naye jaji aliuliza maswali yafuatayo • Jaji….unaishi kijiji gain? • Mh..zai…ninaishi kijiji kumsenga • Jaji……umeishajenga kwenye jimbo lako? • Mh..zai…bado..mimi niko jimbo la kaslu mjini • Jaji…ulikuwa unaudhuria mikutano ya hapa mjini?? • Mh.. zai…hapana.nilkuwa natoka vijijini muda umeenda. Mwisho jaji amemshukuru kwa ushahidi wake uliochukua masaa 4 NILIYOYAONA • Nsanzu halalamikii tofauti ya kura alizozidiwa kama elfu 7 hivi bali ameleta kashfa • Jaji ni mzuri kwa kusikiliza na kutoa ushauri hasa mawakili wakimbana zaidi shahidi. • Kesi hizi ni zakuteketeza kodi za walala hoi wa Tanzania basi Kesi bado inaendele na mashahidi bado wanaendelea wa upande wa utetezi Nawasilisha
   
 2. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Nccr hati hati kupoteza wabunge wote. Wanashitakiwa na kesi zote mbaya isipokuwa kafulila na machali
   
 3. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,449
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Kiongozi nakupa hongera endelea kutujuza nipo dar nikirudi nitashuka ksl kidogo nisikilize kesi
   
 4. k

  kidono Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanx mtoa mada kutujuza yaliyojiri,vp nasikia shahidi wa Mh Buyogera aitwaye Joseph Hittler ambaye ni m/kiti wa nccr mageuzi amezimia mahakamani akitoa ushahidi?
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  mkuu inawezekana umeandika ya maana sana lakini ni bora ukafuata taratibu za uandishi. Panga aya na vituo vionekane.
   
Loading...