Kesi ya Richmond: JK, Mwakyembe, Lowasa............who is a winner? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Richmond: JK, Mwakyembe, Lowasa............who is a winner?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyumbu-, Dec 9, 2011.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Wana Jamvi,

  Kuna kila dalilil CCM kupasuliwa na mjadala wa Richmond. JK ametuhumiwa, na akanyamaza. Bila shaka atakuja na suluhisho zimamoto kama kawaida, ama la kumfukuza kinyemela Lowasa kwa kutumia kamati ya maadili, au kumtia hatiani kwa kumfungulia kesi. Vyovyote vile, njia hii haitomsaidia kwa sababu, Lowasa sasa anapigana kuokoa uhai wake kisiasa, au vinginevyo.

  Na wote tunajua, hakuna nguvu mbaya kama nguvu ya kifo: pumzi ya mwisho hutioka kwa shida, na pengine muuaji anaweza kujikuta kauawa na mfu. Maana yangu hapa ni kwamba, Lowasa has one option: apigane au akate tamaa. Jibu liko wazi, kaamua kupigana, tena vita ya kufa mtu, maana yeye kashika kisu, mwenzie kashika mpini.

  Ijulikane kwamba watu hawa wawili wanajuana vilivyo, so the best way ni kwa wao kumalizana au kukubali yaishe, yote yakiwa na madhara makubwa. Nisiende mbali sana, naomba usome makala hii hapa chini ya Msomaji Raia, na tuangalie nini kitatokea kuelekea uchaguzi wa ndani wa CCM mwaka ujao (2012) na mustakabali wa chama cha CCM na taifa kwa jumla:

  CCM mnasemaje kuhusu Lowassa?


  Msomaji Raia


  WIKI iliyopita nilihoji ikiwa Edward Lowassa anadai ni msafi dhidi ya tuhuma zote ambazo amekuwa anarundikiwa, ni nani basi atakuwa msafi ndani ya CCM? Kwa jinsi ambavyo Edward Lowassa amekuwa akielezwa mbele ya umma na uongozi wa chama chake pamoja na vyama vya upinzani, imejengeka taswira ya kuwa yeye ni alama ya uchafu ndani ya chama wakati wapinzani wake ni alama ya uadilifu.

  Baada ya kile kinachotajwa na mashabiki wake kuwa utetezi wa Lowassa, utetezi uliowafanya watawala wa chama hicho kunywea, ni kama sasa Watanzania wanaaminishwa kuwa Edward Lowassa ni msafi.

  Hili ndilo nililisemea wiki iliyopita, nikilenga kusema kuwa hoja ya Lowassa inatuamsha tukabiliane na ukweli ambao tumekuwa tunaudharau kwa muda mrefu. Kwamba, ama CCM wote ni "wachafu" kama Lowassa au ni wasafi kama alivyodai kuwa yote aliyoyafanya aliushirikisha uongozi wa nchi ambao kwa bahati njema ndiyo uongozi wa chama.

  Madai haya ni mazito, ningependa niyajadili kwa kina zaidi.

  Madai ya Edward Lowassa yanaibua masuala kadhaa yanayofikirisha. Mwenyekiti wa CCM aliyeongoza kikao ambacho Lowassa alikitumia kutoa matamshi ya utetezi wake, ndiye Rais na mkuu wa nchi. Na kwa kuwa matamshi yale yanamhusisha Rais Kikwete kama ama shahidi wa kashfa au mhusika muhimu kashfa ya Richmond, kunajitokeza mgogoro wa kimaadili na kwa sehemu mgogoro wa kikatiba. Nijaribu kufafanua masuala haya tete.

  Ikiwa Kikwete ni shahidi wa kile alichokifanya Edward Lowassa (kwa mujibu wa Lowassa) katika kashfa ya Richmond, unazuka mgogoro wa kimaadili kati ya Kikwete kama Mwenyekiti wa chama tawala na chama chake. Kwamba kile kinacholalamikiwa na wengi kuhusu CCM kupoteza dira na mvuto mbele ya wananchi kuna asili yake katika nafasi na matendo ya Mwenyekiti wake.

  Ufisadi unaolalamikiwa na kuaminiwa kama chanzo cha CCM kupoteza majimbo kadhaa nakupungua ghafla kwa kura nyingi za urais, vina msingi wake katika nafsi na nafasi ya Mwenyekiti wake, yaani Jakaya Kikwete. Haya si maneno yangu, ni maneno ya Edward Lowassa, mbele ya Halmashauri Kuu ya CCM. Kimsingi na kiutaratibu, CCM inapaswa kujibu madai ya Lowassa ama kwa kauli au kwa vitendo. Mgogoro huu si lelemama kwa sababu upo uwezekano wa shahidi kuunganishwa na mashtaka.

  Ikiwa Kikwete ni mshirika muhimu katika kashfa ya Richmond, kwa sehemu kunazusha mgogoro wa kikatiba au hata kama si mgogoro basi ni changamoto kali kwa Katiba yetu. Kashfa ile ilifanyika katika eneo la kiserikali yaani Ikulu na ndani ya Baraza la Mawaziri. Ikiwa matamshi ya Edward Lowassa ni sahihi kuwa Rais Kikwete alikuwa na habari zote za mchakato wa Richmond na kuwa si tu kwamba aliridhia hatua zote bali hata alizuia pale Edward Lowassa alipojaribu kuepusha kashfa hiyo, basi sasa tutafakari je, tunaye rais ‘mhalifu' sambamba na Edward Lowassa.

  Katiba yetu inasemaje kuhusu tafakari hii ya rais ‘mhalifu'? Katiba iko wazi kuhusu mgombea urais aliyewahi kuwa mhalifu lakini sina hakika inasemaje juu ya tafakari kuhusu ‘uhalifu' unaoweza kutendwa na rais aliye madarakani. Kibaya zaidi ni pale rais anayedhaniwa kuwa ‘mhalifu' anapojaribu ama kuficha uhalifu wake au kuzuia haki isitendeke (obstruction of justice).

  Uhalifu wa mkuu wa nchi unaofanyika bila yeye kujua bali katika harakati na mazingira ya kutekeleza majukumu yake ya urais, unaweza kuvumiliwa au kuchunguzwa ili baada ya kumaliza muda wake uweze kushughulikiwa. Lakini uhalifu unaoweza kufanywa na mkuu wa nchi kwa makusudi na kisha kwa jitihada za makusudi uhalifu huo ukafichwa na mkuu wa nchi, au kwa kutumia madaraka yake akazuia haki isitendeke, sidhani kama unaingia katika fungu la kusubiri mpaka mkuu wa nchi amalize muda wake.

  Chama chake kama kimebakiza akiba fulani ya uadilifu na uzalendo kinaweza kumchukuliwa hatua kabla wananchi ambao ni mamlaka ya mwisho hawajalazimika kufanya hivyo. Tumewahi kuona mifano katika nchi nyingine kama Afrika Kusini (sakata la Mbeki) na huko Marekani (sakata la Watergate).

  Wasomaji wa safu hii mtakumbuka kuwa huko nyuma, mara mbili, niliwahi kuhoji inapotokea rais wetu ni mhalifu au ni rafiki wa wahalifu nini. Mara ya kwanza ilikuwa ni baada ya Rais kuwanadi watuhumiwa wa EPA, Rada na Richmond katika Uchaguzi Mkuu.
  Mara ya pili, ilikuwa ni baada ya Rais kuwatuhumu viongozi wa dini kuwa wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kwamba alikuwa na taarifa hizo. Hoja yangu ilikuwa ni nyepesi kuwa "kushindwa kushughulikia uhalifu, ni uhalifu tosha".

  Kigugumizi cha kutoona suala hili katika muktadha ninaoujadili kinaweza kueneza uhalifu huu kwa vyombo vingine. Mathalani, ikiwa chama kitashindwa kutanzua kizungumkuti hiki kitabeba uhalifu huo. Uhalifu wa chama katika suala hili kutaifanya serikali ionekane ni mhalifu pia.
  Hatujasahau na sasa tumekumbushwa kuwa Bunge letu kupitia Kamati Teule iliyochunguza sakata la Richmond, labda lilishiriki uhalifu huu kwa kutotaja kuwa Rais ni sehemu ama ya ushahidi au uhalifu wa kashfa ya Richmond.

  Kwa kitendo hicho, Bunge letu linaweza kuonekana katika taswira ya kubeba sehemu ya uhalifu. Vyombo hivi yaani chama tawala, serikali yake na Bunge letu, vinaponaswa katika buibui la uhalifu wa kashfa ya Richmond ni vigumu kuzuia hakimu wa kweli asifanye kazi yake. Hakimu huyo ni wananchi wa Tanzania ambao CHADEMA wanadai ni nguvu ya umma na kuishia kubezwa na wanasiasa wasiofikiri mbali.

  Bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi liliona kuwa kuna uhalifu umefanyika katika mkataba wa Richmond na kuhitimisha kwa kumtaka Edward Lowassa apime mwenyewe na kuamua. Alipima na kuamua kujiuzulu kwa madai kuwa "anainusuru serikali na chama chake".
  Kama itikio lake, Rais akalazimika kuvunja baraza lote la mawaziri na kuliunda upya.

  Uamuzi huu wa kuvunja Baraza la Mawaziri umeendelea kutumiwa na wasaidizi wake pale wanapomtetea Rais kuwa ni mtu ambaye amefanya uamuzi mgumu katika utawala wake.

  Kwa hiyo, Rais alivunja baraza lile kwa kuridhika kuwa kujiuzulu kwa Waziri wake Mkuu katika kashfa ile kulikuwa kunaigusa serikali yake kwenye kiini na kimsingi aliridhia maoni ya Kamati ya Bunge iliyochunguza kashfa ile.

  Baadaye tulimsikia Rais wetu na Mwenyekiti wa chama tawala akidai haijui Dowans iliyozaliwa na Richmond. Na kudhihirisha kauli yake, akaendesha vikao vya chama chake kuasisi dhana ya kujivua gamba ili kurejesha imani ya wananchi kwa chama iliyopotea kutokana na kashfa mbalimbali ikiwamo Richmond.

  Watendaji wa chama wakatoka nje ya vikao vile wakiwa wakali kweli kweli na kutembea nchi nzima wakinadi azma ya Mwenyekiti kukisafisha chama na kukirejesha katika misingi ya uadilifu. Azma hiyo ilikuwa ni kuwaondoa wote wanaokichafua chama, akiwamo Edward Lowassa.

  Sasa Edward Lowassa kwa maelezo yake ya utetezi ambayo bado hayajakanushwa au kujibiwa, amedai kuwa hakuwa peke yake, alikuwa na Jakaya Kikwete. Suala limerudishwa kwenye Kamati ya Maadili ambako inaelezwa ushahidi na utetezi rasmi utawasilishwa.

  Huko kwenye Kamati ya Maadili, Edward Lowassa ni mtuhumiwa, lakini haijulikani Jakaya Kikwete atakuwa nani? Mwenyekiti, mtuhumiwa, au shahidi? Hapa CCM inabidi itoe kauli, vinginevyo tunadhani kesi imekwisha kabla haijasikilizwa.

  Jambo la mwisho ambalo limeibuliwa na matamshi ya Edward Lowassa mbele ya NEC ni hili alilodai kuwa bila busara na hekima za Rais Benjamin Mkapa, Kikwete asingekuwa rais wetu wa sasa. Ninaamini alilisema hili akimaanisha kuwa ule utamaduni wa kulindana ndani ya CCM ulitumika kumlinda Kikwete dhidi ya tuhuma zilizokuwa zimeibuliwa ili kuzuia yeye asiwe mgombea wa CCM.

  Edward Lowassa alitumia fursa hiyo kumkumbusha Kikwete atumie fursa hiyo hiyo kumlinda yeye dhidi ya tuhuma za namna hiyo. Hata hivyo, matamshi hayo yanadhoofisha na kudhalilisha ofisi ya urais na siyo kumdhalilisha Kikwete kama Jakaya. Watu wengi wanaiheshimu sana ofisi hiyo kuliko pengine wanavyoziheshimu hata dini zao.

  Wanamuogopa na kumheshimu sana Rais wao kuliko hata wanavyowaheshimu wazazi wao, viongozi wao wa dini na hata wenzi wao. Inapofika wakati, watu hao wanaambiwa kuwa mtu waliyekuwa wanamheshimu sana hana sifa za kuheshimiwa hivyo kwa sababu amekalia kiti hicho isivyo halali, ni jambo la kutufanya tufikiri mara mbili kabla ya kumjibu msemaji.

  Ninachotaka kusema hapa ni kuwa, ikiwa sheria imefikia hatua ya kuzuia watu wasihoji uhalali wa Rais baada ya matokeo kutangazwa bila kujali kama mshindi huyo ameiba kura, inakuwaje sasa mtu mmoja anaruhusiwa kuhoji uhalali wa rais aliyekwishaapishwa?
  Kama urais wetu hauko rehani, basi una mbia mwenye nguvu kuliko rais mwenyewe.
   
 2. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nikijibu swali lako; 'Who is a winner' kati ya hao watatu...

  HAKUNA mshindi kati yao, wote ni wezi... Kikwete kwa sababu ndiye mwenye Richmond/Dowans, Lowassa kwa kushirikiana na swahiba wake kuiba na kumfichia siri, Mwakyembe kwa sababu hata baada ya kamati yake kuujua ukweli hakuuweka wazi, alimficha mwizi mkuu akatuzuga kwa kumtaja msaidizi wa mwizi na matokeo yake kapewa rushwa ya cheo....

  Tutakuwa tunafanya makosa makubwa mno kama tutamtetea/kumuunga mkono yeyote kati ya hao watatu..
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Sakata la Richmond limeigharimu nchi yetu rasilmali nyingi sana ukiwemo muda wananchi walioupoteza kujadili swala hili na pesa nyingi zilizotumika na tume ya uchunguzi; achilia mbali hasara za kiuchumi nchi yetu ilizopata kutokana na matatizo ya umeme!!

  Ingawa watu wengi wameisifia tume ya Mwakyembe kwa ripoti yake juu ya swala la Richmond, hivi sasa watu wanaanza kuhoji kama kweli hii tume ilitutendea haki wananchi kwa kuwatuhumu wachache waliohusika na ufisadi ule huku ukimficha muhusika mkuu. Lowassa ameweka bayana kuwa Kikwete alikuwa anafahamu kila hatua ambayo ilichukuliwa mpaka mkataba ule ukatiwa saini sasa Mwakyembe na wenziwe hawakupata taarifa hizo wakati wa uchunguzi wao na kama walizipata kwanini hawakuziweka wazi kwenye ripoti waliyoipeleka bungeni?

  Kama waliweza kuficha sehemu ya mambo je ni sahihi kudhani kuwa hawa jamaa wangeweza pia kuongeza mambo ya uongo kwenye ripoti yao? Mwakyembe na wenzake wamelitendea Taifa hili dhambi kubwa sana kwa Mungukwa kuficha ukweli wa wahusika wa mateso yetu na hivyo inawezekana Mungu wa WATANGANYIKA amechukia na kuwaadhibu wote waliotukosea kila mmoja kwa namna yake hapa hapa duniani!!
   
 4. j

  janejean Member

  #4
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  no comment.
   
 5. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Mkuu Ndinani,

  Ukiangalia majibu ya Lowasa alivyokuwa akijiuzuru, alisema " nadhani tatizo ni uwaziri Mkuu".
  Kwa hiyo , inawezekana kabisa ,Richmond ilijadiliwa na kuchunguzwa kwa mwelekeo wa kumwondoa mtu ambaye bila shaka JK aliona ni tishio kwake.

  Kumbuka Msabaha alitoa angalizo kwa Mwakyembe, na kumsema " Namheshimu sana Mwakyembe kama Mwanasheria mahiri, lakini katika hii ripot na jinsi alivyoiwakilisha, kuna kila aina ya kuamini kwamba ilikuwa conclusive, na hivyo kulikuwa na uwezekano kwamba uchunguzi ule ulilenga kufikia hitimisho fulani."( maneno sivyo yalivyoongelewa, ila alimaanisha hivyo)

  Na bado kitendo cha Mwakyembe kusema angesema na "yaliyofichwa" inaonyesha wazi kwamba, JK aliwaahidi ulinzi hawa wachunguzi wa Richmond, lakini baada ya kufanikisha mradi wa kumwondoa Lowasa, akawatelekeza. Hii ilimfanya (nadhani) Mwakyembe atishie kutoa riport nzima, ili JK akumbuke ahadi yake. Hii ni swala la Logics tu!

  Sasa hawa watatu, kwanini wasirejeshwe kwenye Mjadala, na Lowasa ajibu mapigo kule, huku Mwakyembe atetee riport yake, na JK akanushe uhusika wake? Maana hii kitu italipeleka taifa kusiko!

  Kwa mfano, endapo Mwakyembe au Lowasa wakapata madhara yoyote ya ghafla, huoni kila mtu atakuwa na hisia kwamba kuna mkono wa mtu?

  Ni vyema jambo hili limalizwe haraka, maana kama kweli JK hakushiriki, nini kigugumizi cha kuchukua maamuzi ya kamati teule ya bunge juu ya wahusika? Si ni uso kuumbwa na haya? anajua amewaonea, na yeye kama binadamu, anashindwa kutoa adhabu kwa watu wasio na makosa!
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sikubaliani na wewe kuhusu kamati teule ya bunge na mapendekezo yake, na sababu zinazomfanya Kikwete apate kigugumizi kuwaadhibu wahusika. Tume imewaorodhesha wote waliotuhumiwa na kuwakuta na makosa hivyo Kikwete anashindwa kuwawajibisha sio kwa sababu hawana makosa hapana, anashindwa kwasababu hawa walifanya ufisadi ule kwa maelekezo yake hivyo indictment ya wakina Jairo na Luhanjo na ile kamati teule pia ni indictment ya Kikwete!! Sasa katika hali kama hiyo inakuwa vigumu kwake kutoa adhabu kwani naye pia ni muhusika, ama sivyo angekwisha waadhibu!!
   
Loading...