Kesi ya Mdee, Mbatia yaongezwa muda

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797




Na Esther Mbussi

WAZIRI wa Sheria na Katiba, ameongeza muda wa miezi sita wa kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, Halima Mdee.

Muda huo umeongezwa baada ya Novemba mosi mwaka huu, Jaji anayesikiliza shauri hilo, John Utamwa, kumuagiza Msajili wa Mahakama Kuu, kufuatilia uwezekano wa kuongezwa muda wa kusikiliza shauri hilo baada ya muda wa miezi 12 uliowekwa kwa mujibu wa sheria kumalizika.

Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010, inaagiza kesi zote za uchaguzi kusikilizwa na kutolewa uamuzi ndani ya mwaka mmoja na mwaka mmoja wa kesi hiyo ulimalizika Novemba 23, mwaka huu.

Shauri hilo lilikuja jana kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama waziri ameongeza muda huo.


Jaji Utamwa aliahirisha shauri hilo hadi Februari 6, mwaka 2012, kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali na kuanza kusikilizwa kwa siku nne mfululizo kuanzia Februari 7 hadi 10, mwaka kesho.


Katika usikilizwaji wa awali wa shauri hilo baada ya kumalizika kwa mapingamizi ya awali baina ya pande zote mbili, Jaji Utamwa alisema muda wa kusikiliza shauri hilo unamalizika wakati kesi ya msingi haijasikilizwa na kwamba muda huo uliobaki, atashindwa kulitolea uamuzi na Mahakama haina mamlaka ya kuongeza muda isipokuwa kwa kibali maalum kutoka kwa Waziri wa Sheria na Katiba.


Mbatia alifungua kesi hiyo dhidi ya Mdee akipinga ushindi wa mbunge huyo. Anadai kuwa, wakati wa kampeni Mdee alitoa tuhuma za uongo dhidi yake, akidai yeye (Mbatia) alikuwa akipewa Sh milioni 80 na CCM, jambo ambalo anadai lilimwathiri katika upigaji kura.


Katika kesi hiyo, Mbatia anawakilishwa na wakili Mohamed Tibanyendera na Mdee anawakilishwa na wakili, Edson Mbogoro.


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom