Kesi ya Mawakili Alphonce Lusako na Chengula Emmanuel vs Mbarawa na wenzake ni MCHONGO tu.

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Wafuatao waunge mkono jitihada za Mawakili hawa ili tujiridhishe na uhalali wa ufunguaji wa shauri hili:-

1. Viongozi wa Dini (akina Kitima, Kilaini, Kakobe, Niwemugizi, Mwingira, Bagonza, Eliona Kimaro, Hananja, wengine ni Madeganyanga)
2. Wanahabari.
3. Wasomi Vyuo Vikuu.
4. Wapinzani.
5. Wanaharakati.
6. Wamachinga.
7. Trade Unions ambao maelfu ya wanachama wao wanapoteza kazi kwenye bandari 65 (58 za ziwa, 5 za bahari na 2 bandari kavu).

Madai yao yawe ni haya:-
1. Mkataba huu na mingine chechefu ipigiwe kura ya maoni (referendum) kuikataa au kuikubali.

2. Wahusika wote wawajibishwe.

3. Mamlaka ya rais yapunguzwe kwa 50% kwa njia ya kuandika Katiba Mpya.

4. Rais avunje Bunge nchi iende kwenye uchaguzi, maana Bunge haliaminiki tena, Serikali haiaminiki tena, Mahakama nayo haiaminiki tena kwa kuwa inaendesha tu mashauri lakini hukumu inaandikiwa na serikali.

5. Mafao ya wafanyakazi wa bandari zote 65 wanaoachishwa ajira na mkataba huu wa DP World. Vyama vya wafanyakazi DOWUTA, TRAWU, TUCTA vianze jaramba la kudai mafao bora, kikokotoo cha kueleweka kwa kuwa wao ndiyo jasho lao lilichangia asilimia kubwa 39% ya bajeti ya taifa.

6. TAKUKURU ifanyiwe marekebisho upya ya sheria iliyoiunda ili sheria mpya iifanye kuwa taasisi huru kabisaaa 100% ya uchunguzi. Kwa jinsi hii itatenda haki na itatendewa haki pia. Aidha, itakuwa na weledi kitaifa na kimataifa kiasi kwamba itaweza kushinda zabuni za uchunguzi za kimataifa kama zilivyo Scotland Yard, Federal Bureau of Investigation, Central Intelligence Agency, US Intelligence Coy, Federal Security Services, Research Analysis Wing, M16, Secret Intelligence, Canadian Security Intelligence na (SVR, FSB, FSO, GUSP za Urusi zilizochukuwa nafasi ya KGB) na kuliingizia taifa la Tz mapato pia.

7. Katiba Mpya au sheria mpya zieleze ni kwa vipi na wapi Mahakama inaweza kushitakiwa. Hii itafanya Majaji na Mahakimu kuwakana warasimu/wanasiasa wanaoingilia kazi zao; kwamba wanaogopa kushitakiwa pia watapunguza kula rushwa kwa ajili ya kupotosha hukumu. Niliwahi huko nyuma kuhoji humu takwimu za Majaji na Mahakimu walio jela tukizingatia kuwa Mahakama ndiyo kitovu cha rushwa nchi hii.

NB.
Nina wasiwasi hii kesi ya Wakili Alphonce Lusako na Wakili Chengula Emmanuel ni geresha la dola kuwahadaa na kuwachanganya wananchi. Hawa watu wamejipanga. Time and circumstance will prove me right later.



Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom