Kesi ya Manji dhidi ya serikali kusikilizwa Julai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Manji dhidi ya serikali kusikilizwa Julai

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, May 14, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,852
  Likes Received: 83,305
  Trophy Points: 280
  Date::5/14/2009
  Kesi ya Manji dhidi serikali kusikilizwa Julai

  Na Sadick Mtulya
  Mwananchi

  GODWIN Muganyizi, wakili wa mkurugenzi wa kampuni ya Quality Group Ltd, jana alikwamisha usikilizwaji wa kesi dhidi ya Manji na serikali.

  Kesi hiyo namba 265/2008 inayosikilizwa na Jaji Richard Mziray, ilifunguliwa na Manji Novemba 7, 2008 katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na kuanza kusikilizwa Februari 11, 2009.

  Manji anaishtaki serikali akiidai fidia ya Dola 29, 694, 750 za Kimarekani baada ya kumzuia kuendeleza shughuli za ujenzi katika kiwanja namba 2199, kitalu namba 6 kilicho katika makutano ya Barabara ya Samora na Mkwepu. Kiwanja hicho aliuziwa na serikali.

  Jana Muganyizi alifika mahakamani hapo, lakini akaieleza mahakama kuwa asingeweza kuendelea na kesi hiyo kwa kuwa amepata udhuru.

  Katika maombi yake mfanyabiashara huyo anataka serikali imlipe fidia hiyo pamoja na riba ya asilimia 12, gharama zote za kesi hiyo, kulisafisha jina lake pamoja na gharama nyingine kadri mahakama itakavyoona zinafaa.

  Mchanganuo wa fidia hiyo ni kuwa, Manji anataka alipwe dola 23, 694, 750 za Kimarekani kama hasara aliyoipata kutokana na hatua ya ujenzi aliyokuwa amefikia, na Dola 6,000,000 za Kimarekani kama fidia kutokana na kuchafuliwa jina lake, kampuni na biashara zake.

  Agosti 26, 2006 serikali kupitia Wizara ya Utalii na Mali Asili ilimsimamisha Manji kuendelea na ujenzi katika kiwanja hicho kutokana na Sheria Namba 23(1) ya kutotaka kubadilisha mandhari ya maeneo ya kihistoria

  Katika hati ya mashtaka, Wakili Muganyizi kwa niaba ya Manji, amemshitaki katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi na Makazi pamoja na Mwanasheria Mkuu.

  Hati hiyo inasema katibu mkuu huyo anashtakiwa kwa kuwa ndiye aliyetangaza zabuni ya kuuza kiwanja hicho ambacho alikinunua kwa fedha taslim Sh295 milioni.

  Manji anadai kuwa alihalalishwa kumiliki kiwanja hicho na kupewa hati namba 186166/102 baada ya kushinda zabuni iliyotangazwa na serikali kupitia wizara hiyo.

  Pia anadai Novemba 30, 2005, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilimuidhinisha kama mmiliki halali wa jengo hilo ambalo kwa wakati huo lilikuwa likikaliwa na mpangaji aliyejulikana kwa jina la Shekigendo Simon.

  Manji anadai kuwa Februari 14, 2006 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilimtaka kuliendeleza jengo kwa kubadilisha aina ya jengo alilokuwa akitaka kulijenga la ghorofa 20 na kama asingefanya hivyo angetozwa faini ya kutoendeleza kiwanja na hiyo ilikuwa ni amri kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  Hati hiyo, inasema uamuzi wa Manji kudai fidia hiyo umetokana na serikali kutomjibu barua yake aliyowapelekea na kutotoa maelezo kwa wananchi kuhusu ukweli wa tatizo hilo. Kesi hiyo itasikilizwa tena Julai Mosi mwaka huu.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ninavyoipata mie ni kwamba hii kesi ni mchongo wa mipango ya kuitafutia CCM hela za kampeni za uchaguzi mwaka kesho. Kesi itaamuliwa in his favour na serikali haraka haraka itamlipa madola hayo, au pungufu kidogo jinsi mahakama itakavyopangiwa kuamua.
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hisia yako iko karibu na ukweli, si unajua safari hii EPA hakuna mkuu?, naona hata mchongo wa vitambulisho kama una sua sua make nao ulikuwa ni egemeo lingine!

  Yaani hawa mafisadi, nahisi akitokea hata mkoloni akaja akasema niuzieni watu/binadamu, wanaweza mega ka mkoa kamoja waka katuuza alimradi wabaki madarakani!

  Lakini Mungu yupo, siku yaja tena karibu tuta shuhudia ukombozi mpya toka mikononi mwa mafisadi.
   
 4. expedition

  expedition JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2017
  Joined: Jul 16, 2016
  Messages: 709
  Likes Received: 1,566
  Trophy Points: 180
  Leo ni kesi ya Serikali dhidi ya Manji
   
Loading...