kwenye Sheria kunakitu kinaitwa kuwajibika kwa makosa aliyofanya mwingine (vicarious liability). Hususani katika tukio hili kinachoangaliwa ni uhusiano uliopo katiyako na dereva wa gari yako. Mfano alipata ajali akiwa katika utekelezaji wa majukumu uliyomuagiza wewe, basi katika Sheria ya madhara utawajibika kwa niaba yake.
kuhusu bima, ikiwa wewe utawajibishwa, basi kama kunamkata hai katiyako wewe na taasisi ya bima kwajili ya kulipia/kufidia madhara yatakayotokea kulingana na chombo hicho dhidi ya mtu mwingine basi bima itawajibika pia.