Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Well, simo bado ni lile lile - WATU na MAZINGIRA..mlitegemea kitu gani nyie mnaozungumzia sheria ktk mazingira ya Kiafrika..
Binafsi nilitegemea hili kutokea laa sivyo kuendelea kuhonga mahakimu na wengine kutumia wa wachawi kutafuta viungo vya watu ili kesi zizimike, ndio option zilizopo..
Nina hakika hata hao walioko nje kina Mramba wanajishughulisha na moja ya hayo hapo juu, sheria na haki haiwezi kusimama kwa Wadanganyika.. kwani NDIVYO TULIVYO!

Ndio hata mimi nashangaa hapa watu wanapojifanya kushangazwa.

Watanzania wamesharidhika na hali halisi ya ile nchi, tunapoteza muda tu hapa kupiga kelele wakati wananchi wenyewe wanaona kila kitu pouwaaa tu.
 
Au labda yuko hapahapa Dar amejichimbia Uswazi? ansubiri ishu ipoe kisha anaishia kiulaini.

Si rahisi kufanya kosa kama hilo. Nairobi kuna ndege ya Egypt air inaondoka saa kumi asubuhi. Kwa ndege hii mpaka inafika saa sita mchana mtu ameshafika mbali saaaana. Kuna uwezekano alianza safari ya nairobi usiku!
 
Inasemekana hakimu Hadija "ameshachukuliwa" na TAKUKURU ..... tunaomba confirmation kwa mlioko huko.

Hakimu hajachukulwia na yeyote. Faili ndilo limeitishwa Mahakama Kuu (nadhani kwa ajili ya kuangalia kwa nini alipewa dhamana tofauti na masharti). hakimu ndiye aliyewaachia wadhamini wa Liumba yapata nusu saa iliyopita. jana alitoa hati ya kukamatwa Liumba na kuletwa mahakamani lakini hakupatikana nyumbani wala kwa jirani, simu yake kaputi ndipo walipotafutwa wadhamini. Leo tangu asubuhi walikuwa ndani na jioni hii hakimu amesema hawezi kuendesha kesi kwa sababu faili lipo Mahakama Kuu. Hivyo ameaachia hadi kesho asubuhi
 
Hey me...wake up, this is just a dream.
Hapa naota kwamba nipo jf na kuna habari kwamba AL ameruka 'dhamana'.....
No!
Hapana hii nchi ina hadi UWT, halafu mtu aliyehujumu uchumi 'atoroke'? Hapana....
 
Watajitokeza ghafla na kauli yao ya kila leo 'serikali ina mkono mrefu' but 4 sure jamaa ndo kashakitoa hvyo...Ikirud ina pancha!
 
....kwa kuwa bado ni tetesi, atatorokea wapi? Mahenge??


HAhahah Mahenge atakuwa hajafika labda ndo kwanza anaanza mlima Ndururu!!, tukiacha masihara kama ni kweli this is a serious joke of our time in history...usalama wa taifa wako wapi na wanafanya nini.....lazima kuna mchezo hapa unaendelea....
 
Run, run as fast as you can
You can't catch me I'm the Red Rav4 man
I have power, I have steam,
I have wind in my sails
You dont believe me
Ask all those females!!
 
lakini kwani jamaa wakati anadhaminiwa hakunyang'anywa paspoti yake ?

Linyang'anywa passport ya zamani iliyokuwa imejaa, na nafikiri alikuwa na nyingine mpya. Kama kweli hili ni pigo kwa hakimu na mafisadi sasa wanachekelea. Ila huenda ametoroshwa na mafisadi wenzake, maana huko mbele wazito wangetajwa tu.
 
Hakimu hajachukulwia na yeyote. Faili ndilo limeitishwa Mahakama Kuu (nadhani kwa ajili ya kuangalia kwa nini alipewa dhamana tofauti na masharti). hakimu ndiye aliyewaachia wadhamini wa Liumba yapata nusu saa iliyopita. jana alitoa hati ya kukamatwa Liumba na kuletwa mahakamani lakini hakupatikana nyumbani wala kwa jirani, simu yake kaputi ndipo walipotafutwa wadhamini. Leo tangu asubuhi walikuwa ndani na jioni hii hakimu amesema hawezi kuendesha kesi kwa sababu faili lipo Mahakama Kuu. Hivyo ameaachia hadi kesho asubuhi

Nasikia kichefu chefu..... Yaani kweli nikasikia wadhamini wameshikiliwa wanaweza kushitakiwa, sasa naambiwa wameachiwa tena!!!!!Hii picha ina wachezaji wengi sisi tutaendeela kuwa Watazamaji, na ndio maana leo Peter Noni ni shahidi na mshitakiwa wa kesi za EPA. Na Noni kuwa shahidiwahandishi wa abari wanaandika (tunaandika) na wako wanaomjuita Peter .... na si Peter Noni yule ambaye ana ukwasi wa kutisha mwenye mapesa mengi ya Vodacom aloyomuuzia Rostam hisa
 
Labda atorokee vijinchi visivyoeleweka.... akienda nchi "zinazofahamika" ambapo tuna makubaliano nazo kurudishiana wahalifu...atarudishwa tu!Labda utoro huu uwe na baraka za wenye mamlaka.
 
..ni kama nimeamka usingizini vile na kushtukia ni April mosi, ile siku ya waj...
kama siyo basi tumekwisha. Usalama wetu uko hatarini kwa hali hii! Mkono mrefu wa Serikali tunauhitaji hapo, na haraka mafisadi wote warudi ndani hatuna imani tena.. masikini waliomdhamini huyu jamaa hawakujua akili yake toka mwanzo? badala ya kufanya ya maana anahonga magari.
 
Nilipokuwa naangalia habari ile juzi usiku na kutangazwa Linyumba ameachiwa kwa dhamana ambayo haikukidhi masharti; nilimwambia wife huyu mtu ameshatutoroka na hii kesi ni kiini macho tu.

Ni kweli nchi hii ina askari na usalama wa taifa kwa ajili ya ccm tu na si vinginevyo; mtu muhimu km huyu na mafisadi wengine wote ilikuwa ni kuwawekea critical monitoring kuanzia pale alipotoka mahakamani hadi nyumabani kwake, anakutana na nani, anawasiliana na nani, anaenda wapi n.k. Lakini huuu usalama wa taifa wanamfuatilia dk. slaa, zitto, na wapinzani wengineo.

Namalizia na nukuu zifuatazo hapo chini: -

"MKURUGENZI Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk. Hassy Kitine, amesema taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la uongozi, ambalo halijawahi kutokea katika historia ya nchi.

Kitine ambaye aliiongoza idara hiyo nyeti kwa karibu miaka 30 zama za Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili, alisema ukosefu huo wa uongozi umesababisha nchi iongozwe kienyeji.

Kachero huyo namba moja kwa miaka mingi, ambaye alilazimika kujiuzulu wadhifa wa uwaziri wa nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, mwishoni mwa miaka ya 1990 kutokana na kuhusishwa na kashfa ya mkewe kufuja fedha za umma kiasi cha shilingi milioni 40, alirejea kutoa kilio chake cha miaka mingi cha kuporomoka kwa maadili ya uongozi nchini.

"Hali tuliyofikia si nzuri, tena niseme ni mbaya sana. Kuna kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya uongozi. Na hii nawaambia, nchi haijawahi kuwa katika hali mbaya huko nyuma kama ilivyo sasa. Kwa hali tuliyofikia, ni vigumu kurekebisha maadili ya uongozi.

"Tatizo kubwa ni viongozi kukosa integrity (uadilifu). Kwanza ni integrity ya viongozi wenyewe, pili ni commitment (wito), tatu ni nationalism (utaifa). Haya ndiyo yalikuwepo wakati wa Mwalimu," alisema Dk. Kitine.

"...Akizungumza kwa kujiamini kama ilivyo kawaida yake, Kitine alisema viongozi wengi wa serikali wamepoteza sifa kuu tatu za uongozi ambazo ni kuwa na uadilifu, wito na kuweka mbele utaifa, sifa ambazo alisema ndizo zilikuwa nguzo ya uongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, chini ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere..."

"... "Haiwezekani viongozi wakateuliwa kwa misingi ya mitandao …sijui, kwa msingi wa politics of division (siasa za makundi) ndani ya chama. Haiwezekani nchi ikaendeshwa kienyeji. Integrity should be number one (uadilifu unapaswa kuwa kitu cha kwanza kuzingatiwa).

"Mtu anajiuzulu, anafukuzwa uwaziri kwa sababu ya kashfa, kwa sababu ya kukosa maadili, halafu anabakia kuwa mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya chama, nini hii? Hii haifai. Waziri akikosa uadilifu anatakiwa aondolewe mara moja nyadhifa nyingine zote alizobakiwa nazo. Nadhani hii itasaidia," alisema Dk. Kitine pasipo kutaja jina la kiongozi yeyote..."


"..."Usalama wa Taifa should be completely clean (unapaswa kuwa safi kabisa). Idara hii inatakiwa kuwa, juu ya mambo ya rushwa, iwe safi kabisa. Usalama wa Taifa ndiyo unayoteua viongozi, ndiyo inayoshirikiana na rais kwa kumshauri katika kuteua mawaziri. Sasa kama Usalama wa Taifa ukiwa mchafu ndio tunapata viongozi wala rushwa. Nafikiri vigezo vinavyotumika kuteua viongozi pia vina matatizo,"
Dk. Kitine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom