Kuna taarifa kwamba Amatus Liyumba, ambaye sasa anatajwa kwamba ametoroka na hajulikani hayumo, HAJATOROKA na kwamba alikuwa amejipumzikia akiangalia afya yake huku akijipanga kutimiza masharti ya dhamana ambayo yanaelezwa kwamba mawakili wake walifanya 'madudu' kwa kushirikiana na Hakimu Khadija Msongo.
Kwa taarifa hizo ambazo hadi sasa ni TETESI, Liyumba sasa anaweza kuibuka tena mahakamani kati ya kesho Jumatatu na Kesho kutwa Jumanne, kuwasilisha hati za ziada za dhamana zenye thamani sawa ama zaidi ya sh bilioni 54.
Kama hiyo ni kweli basi wiki ijayo tutakuwa na mjadala tofauti na tunaoendelea nao sasa.
Mods, mutaangalia kama haistahili mutaiunganisha kule!!!!!!!
Mahakama "inasimamia" Sheria...Polisi wanajukumu la kuhakikisha "utekelezaji" wa sheria hizo kwa mujibu wa Katiba.
Sio Jukumu la TAKUKURU "kusimamia" kama sheria inatekelezwa...wao ni jukumu lao ni "kuchunguza" iwapo sheria imevunjwa katika misingi ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka n.k. Hivyo wakiona sheria imevunjwa wanapeleka kesi yao "mahakamani", kama ilivyo hii ya Liyumba.
Mtuhumiwa akishafikishwa "mahakamani" jukumu la TAKUKURU kumlinda linakwamia hapo, Mahakama inatumia vyombo vyake ambavyo ni Polisi na Magereza kuhakikisha sheria na haki inasimamiwa.
Mtuhumiwa akitoroka (baada ya kufikishwa mahakamani) anakuwa ametoroka akiwa chini ya Ulinzi wa Polisi, na sio TAKUKURU. Hakimu aliposema akamatwe arudishwe rumande, alikuwa ametoa amri hiyo Polisi na sio TAKUKURU.
Polisi na Magereza vyote vipo chini ya Wizara ya Masha...anaposema anasubiri kuombwa na TAKUKURU ndio wafanye kazi yao...nashindwa kuelewa.
Iwapo Katiba imebadilishwa, naombeni kuelimishwa.
Kuna taarifa kwamba Amatus Liyumba, ambaye sasa anatajwa kwamba ametoroka na hajulikani hayumo, HAJATOROKA na kwamba alikuwa amejipumzikia akiangalia afya yake huku akijipanga kutimiza masharti ya dhamana ambayo yanaelezwa kwamba mawakili wake walifanya 'madudu' kwa kushirikiana na Hakimu Khadija Msongo.
Kwa taarifa hizo ambazo hadi sasa ni TETESI, Liyumba sasa anaweza kuibuka tena mahakamani kati ya kesho Jumatatu na Kesho kutwa Jumanne, kuwasilisha hati za ziada za dhamana zenye thamani sawa ama zaidi ya sh bilioni 54.
Kama hiyo ni kweli basi wiki ijayo tutakuwa na mjadala tofauti na tunaoendelea nao sasa.
Mods, mutaangalia kama haistahili mutaiunganisha kule!!!!!!!
Hapa nadhani umechemsha. Takukuru kama kitengo, kina mamlaka yote chini ya sheria ya kukamata na kushtaki kama Polisi. Kitengo hiki ni kama polisi lakini tofauti yake ni kuwa chenyewe kinajikita zaidi kwenye rushwa. sasa wewe huoni ajabu kama ingekuwa ni jukulu la Polisi kumsaka Liyumba ni vipi Takukuru ndiyo itowe fedha za zawadi ya kumpata na ni vipi iende kumsaka nyumbanio kwake na majumba ya marafiki zake?.
Yote haya yanafanyika chini ya Katiba ya nchi..
Mkuu halisi,
Mimi nakuamini kwa data za uhakika. Kama umesema tetesi basi hii habari ina ukweli zaidi ya asilimia 50.
Asante sana kwa muda wote kutupa habari za uhakika.
TK,
Haya maswala ya jukumu ni ujinga wa siasa zetu.. Chukulia Osama bin Laden unafikiria ni jukumu la CTU kumtafuta na sio vyombo vyote vya usalama nchini Marekani?.. iweje wamepeleka jeshi la nchi hiyo huko Afghabstan badala ya kuwa ni kazi ya CTU peke yao....
Kibaka anaweza kamatwa na Mgambo iwe leo fisadi!.. unataka kunambia itakuwa jukumu la mgambo kumtafuta kibaka aliyekimbia kuhudhulia mahakamani!
Mkuu halisi,
Mimi nakuamini kwa data za uhakika. Kama umesema tetesi basi hii habari ina ukweli zaidi ya asilimia 50.
Asante sana kwa muda wote kutupa habari za uhakika.
Yebo Yebo,
Bila shaka, PCCB wanayo mamlaka makubwa ktk kesi za mafisadi lakini mtu anapotoroka linakuwa ni swala la Fugitive!.. hii ni hatua nyingine kabisa ambayo inahusiana na vitengo vyote vya Usalama.. Liyumb alipoiba BoT ilikuwa ni mamlaka ya BoT kumchukulia hatua lakini pindi swala zima lilipoingia ktk Ufisadi na kufunguliwa mashtaka haikuwa jukumu la BoT tena ingawa wanahusika kwa kiasi kikubwa..
Vile vile PCCB walipomfikisha Liyumba mahakamani mbele ya sheria inabidi nao wafuate sheria na taratibu za mahakama nje ya matakwa yao.. Sasa kama Liyumba angekuwa Keko unafikiria PCCB wangeweza kwenda pale na kumtoa nje bila dhamana kwa sababu ni jukumu lao, wana maamuzi yote!.. Uamuzi wowote wa mahakama ni sheria nje kabisa ya uwezo wa PCCB.. dhaman ikataliwe au ikubaliwe sio kazi ya PCCB kwani hiyo ni hatua nyingine..Na sidhani kama kisheria lilikuwa jukumu la PCCB kuhakikisha kwamba Liyumba hatoroki..hawa jamaa zetu hapa wanajichanganya tu..
Navyofahamu mimi hakuna sheria inayompa jukumu mshtaka kumchunga mshtakiwa hasa baada ya kesi kuwakilishwa mahakamani...sijui labda nipewe somo hapa!
Liyumba kakimbia kutohudhuria mahakama - ni FUGITIVE hilo swala la Ufisadi linawekwa pembeni..maswala ya zawadi hata mimi naweza kuweka zawadi ya kumkamata mtu aliyeniibia simu lakini haina maana ni jukumu langu kisheria kumtafuta!
Mkandara unayosema ni kweli. Pia inawezekana mojawapo ya masharti ya mdhamana ilikuwa ni kuripoti maybe kila wiki hapo mahakamani. Na inawezekana kutokutokea kwake bila ripoti ndipo wakasema ametoroka. Kiutaratibu siku ambayo hakuripoti mahakamani bila sababu za msingi na warrant inakuwa effective hapo hapo. Kwa wenzetu wanaingiza kwenye system na hata ukisimamishwa kwa kosa la traffic wanaweza kuona una warrant na wanakukamata. Sasa sijui ni rukhsa gani kina Masha waliyokuwa wakiizungumzia...Nadhani mtuhumiwa kama ni kweli katoroka basi ni mojawapo ya mbinu za kumwacha atokomee....Kama sivyo basi ni kweli tuna tatizo kubwa sana la uongozi na itakuwa ni kubwa kiasi cha kutisha.
Hivi Liyumba ameshtakiwa na nani hadi MASHA aseme akipata maombi kutoka TAKUKURU anaweza akasaidia kumtafuta huyu LIYUMBA?
Masha bado anasisitiza kuwa haja pata ombi la kumtafuta MKULU lakini anasema kwa kuwa zote (TAKUKURU na WIZARA) ni idara za SERIKALI anaweza kusaidia.
HIVI,POLISI wakiona kibaka au mtu anataka au amefanya uhalifu hawawezi kumkamata hadi aliyefanyiwa uhalifu alalamike au kuomba msaada kwao?
MASHA ANATAKA TUMUELEWE VIPI?Kwamba yeye na wizara yake hawawezi kuzuia au kukamata mtu anaye shutumiwa kwa uhalifu wa aina yoyote?
Akitimiza masharti ya hiyo dhamana mimi nita kana uraia wangu!!!!!!!