William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
FMES Unaweza kuona hapo juu maelezo ya Mkandara, ccm waliizima ile issue ya Chenge kule bungeni na inawezekana ule unga unga ulikuwa ni mifupa ya albino kwani ukweli haujawekwa wazi na kitendo cha sakata lile kwisha labda kilihusishwa na uwezo wa kufanya kazi wa dawa hizo za kichawi...Ikapelekea viungo hivyo vya albino kuwa dili na ndio maana wenye kuhitaji viungo hivyo ni watu wenye uwezo ama madaraka. Kama issue ya unga unga ingeshughulikiwa ipasavyo basi labda albino wasingekumbwa na dhahma hii na waziri mkuu asingekuwa na haja ya kulia lia.
Hata hivyo pointi yangu inarudi pale pale, wewe na Mkandara mlisema JK anafanya kweli na bado unasisitiza kuwa thats the case,kwasababu mlijuwa kuwa sheria ni mbovu kama alivyosema Mkandara hapo juu na huku mkimsifia Mh Rais kwa kuwafikisha watuhumiwa hao kunako sheria mbovu.
- Hapana, mahakama ni moja ya vyombo vitatu muhimu vya serikali, ambavyo vinatakiwa ku-function independent of each other for the good of the people, sasa kama hili halifanyiki Tanzania, ni muhimu kujua sababu na kujaribu kurekebisha sababu,
Lakini ya kwamba rais wa jamhuri ahusike tena na mahubusu waliko mikononi mwa mahakama, itakuwa ni more than Banana Republic!
Nope nilikuwa nabeba zege!
Ok let's now get back to the topic. Kuhusu kupoliticize issues nadhani ni kaugonjwa ka viongozi wa kitanzania. And I especially smell a rat hasa pale uchaguzi unapokuwa ukikaribia. My point is and still is........ Not necessarily kwamba JK anahusika ( Well I am not ruling out completely maana Bongo kila kitu kinawezekana) Lakini katika jamii iliyomomonyoka maadili kiasi hiki je Liyumba hawezi kucheza faulo na hakimu pale Kisutu akatoka kwa staili aliyotokea??
Taarifa za uhakika za hivi punde kutoka mahakamani ni kuwa AL hakufika:
Uamuzi ni kama ifuatavyo
1. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 24 ambayo ndiyo ilipangwa awali kwa yeye kufika mahakamani
2. Hati ya kukamatwa wadhamini wake imefutwa. Hivyo watatakiwa tu kuripoti hapa mahakamani siku ya tarehe 24. Iwapo AL hatafika siku hiyo ndipo wanaweza kukamatwa. wameachiwa na wamekwenda makwao.
Habari ndo hiyo
Oh yes Sahib You can tell a lot on when and what people are thinking kutokana na body language......I dont know that part of expertise but its easy to read people kutokana na body language.
Kelly dear uko juu,mi nilihudhuria mahakamani siku moja na kitu cha kwanza kilichopita akilini ni huyu jamaa akipewa dhamana atatoroka,macho yake yalikua hayatuli halafu ukimwangalia anakwepesha haraka 'obvious flight risk'.Tukiacha yote ilishindikana hata kuweka askari wawili getini kwake wakague magari yote yanayoingia na kutoka?
Kuna mifano mingi tu ya serikali kukataa uamuzi wa mahakama(Kumbuka kesi za Mtikila na mgombea binafsi),
ku-ignore mapendekezo na maelekezo ya bunge, na ukiagalia kwa undani utaona kuwa bunge ni kama baraza la maongezi tu au printer ya serikali (ingawa mwaka jana na mwaka juzi lilionekana kurudi kwenye akili zake sina hakika kama itakuwa permanent au vipi)
- Hili sina clue kabisa ya unga unga wa Albino? What is that?
- Unachanganya mambo mengi sana ambayo hayahusiani kabisa, tatizo sio sheria zetu, tatizo ni mahakimu, sheria iko wazi kwmaba zimapotea Billioni 200, watuhumiwa lazima waweke nusu ya hela hizo katika dhamana, sasa kwa nini hakimu alikubali millioni 800?
Sasa unasema hili ni tatizo la rais wa jamhuri? Bado sikuelewi?
Mkandara alisema hakutegemea lolote na kwamba viuongo vya binadamu vinatumika kichawi ili kuzima kesi hizo,sasa albino si binadamu?
FMES. hapa Jmushi1 aliniacha hoi yaani duh... taabu kweli kweli!..iMkandara alisema hakutegemea lolote na kwamba viuongo vya binadamu vinatumika kichawi ili kuzima kesi hizo,sasa albino si binadamu?
JMushi1,
Wow! wait a minute mkuu wapi nimeandika kuhusiana na Chenge bungeni kuwa ni unga unga wa Albino?..
Mkuu jaribu kusoma maelezo ya mtu ukayatafsiri kama yalivyo badala ya kuongezea mawazo yako..
Mimi nilichoandika kinatokana na watuhumiwa kuwekewa dhamana ambayo ni haki yao lakini kutokana na MAZINGIRA yetu, kuna possibility mbili tatu za kutokea nikizingatia NDIVYO TULIVYO ktk imani za uchawi, kuhonga na kama ikishindikana kuingia mitini!..
Ni matokeo ambayo serikali yetu na vyombo vya usalama haijajifunza au wao wenyewe ni wahusika wakubwa..
Watu na mazingira ni somo ambalo tunahitaji sote tulifahamu vizuri sana kila tunapojaribu kujenga sera na utekelezaji wake..Kwa mfano mdogo tukianzia ngazi ya chini kabisa...hakuna kibaka anayeogopa askari Polisi isipokuwa wanaogopa wananchi zaidi. Kwa sababu anafahamu akikamatwa na askari mchezo utamalizika njiani kuelekea kituoni au utamalizwa kituoni penyewe..Bahati mbaya utafika mahakama na hapo bado kuna uwezekano wa kutoka au kesi kuchukua miaka 10 akiwa huru kwa dhamana isiyokuwa na mpaka..Ikishindikana kabisa ataingia mitini kuhamia mkoa mwingine akiwa chini ya dhamana iliyotolewa kisheria..
Sasa hali hii ipo ktk kila ngazi ya maisha na sikushangaa kabisa kusikia Liyumba kaingia mitini hasa baatya ya kusikia alikuwa akipelekeshwa kichini alipokuwa jela.. watu walikuwa na kisasi naye, toka Polisi, mahakama na hata wafungwa walitaka kumla akiwa hai!.... bahati dhamana hiyoo! sasa afanye nini?.
Hivyo, hili sio kosa la Kikwete ni kosa la watunzi wa sheria zetu na utekelezaji wake. Kikweyte hawezi kutunga sheria na kutoa amri ya utekelezaji wake kinyume cha sheria.. Ndio yalomkuta Pinda ktk issue ya Albino na wapo watu hadi leo wanaamini kabisa kuwa hatuhitaji zoezi la aina yoyote isipokuwa kutegemea vyombo vya sheria.. vyombo ambavyo wanafahamu vinafanya kazi kwa tender... mwenye kupanda dau zuri ndiye mshindi..
Tunarudi pale pale kuwa sisi NDIVYO TULIVYO...na huwezi kuamini niliposikia habari za Liyumba kutoroka nilijua tu watu wataanza kutafuta MCHAWI...baada yaa.. wakati wanafahamu fika kwamba system nzima ya sheria ni bomu.
unga unga wa Albino
- Mkandara alisema inahusika vipi na wewe kumhusisha rais na kutoroka wka Liyumba akiwa under sheria?
Habari zilizo patikana hivi punde ya kuwa Liyumba ametoroka na wadhamini wawekwa rumande baada ya kushindwa kumleta mshatiwa mahakamani!!!!
Kwamba rais alijuwa Liyumba ataoroshwa ndiyo maana akampeleka kunako sheria ili passport yake iliyopitwa na muda ikubalike kwani wananchi wamekomalia kichwa.
Hii ni balaa kubwa kama ni kweli Chenge alikuwa na unga unga uliotokana na viungo vya Albino, nimechoka kabisa kabisa!! Una afikiri vifo vya hawa ndugu zetu vitaisha kweli? Mkemia wa serikali naye alikuja na matokeo ya kujua mwenyewe? Kama Mh spika bado anao huo unga uje ufanyiwe tafiti na wataalam wa nje CIA, FDA, Scotland yard etc etc...
Mkuu ebu nambie wewe ulitaka Kikwete afanye nini na mafisadi?.. sikumbuki kama kuna mtu hata mmoja aliyetaka watu hawa wasifikishwe ktk sheria ila Kikwete afanye kitu tofauti!.. sikumbuki hata kuona maandishi yako wewe mwenyewe ukipnga watu hawa kufikishwa mahakamani..Kama mlijuwa JK kuwakimbizia hao watu huko kwenye sheria mbovu ili waweze kuwatolea huko then kwanini mlimsifu kuwa anafanya kweli? Mkandara you was # 1 kusema lets give him a benefit of doubt. Kuwachezea watanzania akili kiasi hiki si jambo jema hata kidogo...Ni sawa na ile michezo ya kitoto..Now you see it, now you dont.