PreGE2025 Kesi ya Lissu yaiweka Chadema njiapanda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
1d6e0640-162b-11f0-ad14-a76bd5311d47.jpg

Hatua ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kufunguliwa mashitaka ya uhaini na uasi inakiweka chama hicho njiapanda, hasa ikielezwa kuwa kiongozi huyo ameonyesha ujasiri mkubwa kuikabili Serikali katika kampeni yake ya No Reforms No Election (Hakuna Mabadiliko Hakuna Uchaguzi).

Lissu aliyeongoza mikutano No Reforms No Elections katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini (Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi) na kisha kuhamia Kanda ya Kusini (Lindi, Mtwara na Ruvuma) huenda asionekane hivi karibuni kutokana na kesi hiyo.

Baadhi ya wanasheria wanasema kesi hiyo huenda ikakiathiri chama hicho, kwani kuna hatari ya Lissu kukaa rumande kwa muda mrefu.

Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma muda mfupi baada ya kukamilisha mkutano wake wa jioni na kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam.

Aprili 10, 2025 Lissu alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa mashitaka na upande wa Jamhuri kuwa ni ya uhaini. Kwamba mshitakiwa alitengeneza nia kwa umma kwa kutoa maneno yenye kuashiria uasi.

Mbali na tuhuma hiyo, Lissu pia anatuhumiwa kwa makosa mengine yakiwamo ya kuchapisha taarifa za uongo kwamba, “Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 uliharibiwa kwa maelekezo ya Rais (YouTube),” “Polisi wanatumika kuiba kura wakiwa na vibegi. (YouTube)” na “Majaji ni wa CCM hawawezi kutenda haki, ni wateule wa Rais wanataka uteuzi wa majaji wa rufani. (YouTube).”

Kutokana na kesi hiyo, Lissu amepelekwa rumande akisubiria siku nyingine ya kufikishwa mahakamani.
Sheria ni ngumu

Kwa mujibu wa Wakili Kiongozi wa Haki Kwanza Advocates, Aloyce Komba hatua ya Lissu kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ni maandalizi tu (PI), kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza ya uhaini.

“Tukumbuke kesi ya Tundu Lissu ipo hatua ya chini sana ya maandalizi yaani "PI" kama zilivyo kesi za mauaji au ugaidi au uhujumu uchumi. Yaani Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi,” amesema.

Kuhusu maandalizi ya kesi kwenda Mahakama Kuu, amesema kukamilika kwake ni kitendawili.

“Kesi za "PI" zinakaa mahakamani hata miaka mitano hadi 10!!! hazina tofauti na kesi za ugaidi. Halafu sheria inamnyima mtuhumiwa.

“Je, haki za kisiasa za Tundu Lissu zitalindwaje wakati huu anapokabiliwa na hii kesi ngumu ya jinai? Tusubiri "mapambano yake mahakamani" maana mapambano ya kisiasa yamekomea pale,” amesema Komba.

Suala hilo pia limeungwa mkono na Wakili Jebra Kambole anayemtetea Lissu akisema, “Ni kweli itachukua muda mrefu kwa kadiri watakavyotaka wenyewe (upande wa Jamhuri). Wanaweza kusema tu upelelezi haujakamilika.”

Kosa la uhaini likoje?

Kambole amesema kosa hilo haliwezi kutendwa na mtu ambaye hajala kiapo cha Serikali.

“Kifungu cha 39 (1) kinasema, mtu yeyote ambaye, akiwa na utii kwa Jamhuri ya Muungano(a) akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au mahali pengine popote… Kwa nini kisiseme mtu yoyote tu? Hicho kinawahusu waliokula kiapo cha utii kwa Serikali.

“Mtu wa kawaida ambaye hajala kiapo atatendaje kosa la uhaini? Linawahusu viongozi wa Serikali waliokula kipapo kama mawaziri na wengine wanaoapishwa. Wapo pia askari wa majeshi ya ulinzi na usalama,” amesema.

Ameongeza, “Sio kwamba hawajui hilo, ila wanachojua ni kwamba ameshawekwa ndani, basi.”

Akilichambua kosa hilo kisheria, Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS), Boniphace Mwabukusi amesema vigezo vya kisheria vya kosa la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code) [Cap. 16 R.E 2022] kinahusu kitendo cha kujaribu au kuchochea kuangusha serikali halali kwa njia ya vita au ghasia, maneno au maandishi yanayochochea umma, vitisho dhidi ya viongozi wa serikali, au njia yeyote ile inayoashiria uasi dhidi ya mamlaka halali.

“Siyo uchaguzi au Tume ya Uchaguzi… kosa la Uhaini kukidhi vigezo lazima lioneshe kuwepo kwa nia ya uhaini (mens rea), siyo nia ya kupinga au kuzuia uovu, kuwepo kwa kitendo cha wazi cha kutekeleza au kuchochea uhaini (actus reus) na ushahidi kwamba maneno au matendo hayo yalilenga kuvuruga au kuangusha serikali halali,” amesema.

Chadema wajipanga upya

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 11, 2025 katika makao makuu ya Chadema Mikocheni Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu (Bara), Amani Golugwa amesema wanajipanga kuendelea na mikutano ya No Reforms No Election.

“Vuguvugu la No Reforms No Election litaendelea, vuguvugu hili sio uasi, sio uhaini.

“Leo saa 8:30, sekretarieti ya chama itakutana katika ofisi zetu za hapa Mikocheni kujadiliana na kuweka kupanga kwa habari ya mwendelezo wa operesheni hii. Tunajua mwenyekiti bado yuko rumande, lakini viongozi wapo tukiongozwa na Makamu Mwenyekiti (Bara) Mheshimiwa (John) Heche na Makamu Mwenyekiti Zanzibar na wajumbe wa kamati kuu, tutaendelea,” amesema Golugwa.
 
Attachments

  • 1d6e0640-162b-11f0-ad14-a76bd5311d47.jpg

    78.6 KB · Views: 27
  • 1d6e0640-162b-11f0-ad14-a76bd5311d47.jpg
    1d6e0640-162b-11f0-ad14-a76bd5311d47.jpg
    78.6 KB · Views: 33
  • 1d6e0640-162b-11f0-ad14-a76bd5311d47.jpg
    1d6e0640-162b-11f0-ad14-a76bd5311d47.jpg
    87.1 KB · Views: 29
View attachment 3300363

Kwahiyo ww unaogopa lisu kukaa muda mrefu mahabusu, utakuwa punguani wa head
 
Hata Lissu akikaa Rumande agenda ya No Reform No Election ime sound kila kono ya nchi.
Hata huku ambako hajafika tumeshaipokea na tunaielewa!
Katika nyakati hizi za Utandawazi,mtu akisemea Japani au Wapi alichokisema kinasambaa kote duniani.
Kumfunga hakutabadili mindset ya watu ambao wameshaipokea ajenda hiyo.
Niseme hata Lissu asiposema MAWE YATASEMA.
 
  • 6028918-c90487a0a3c9f670172c401e803cbac6.mp4
    3.5 MB
Back
Top Bottom