Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,300
- 25,920
La kwanza, iwapo kila mshtakiwa yuko huru hadi atakapokutwa na hatia na Mahakama na iwapo dhamana ni haki kwa kila mshtakiwa (ikiwa tu shtaka lake linadhaminika), kwanini kuna mkwamo mkubwa kwenye dhamana ya Mbunge Godbless Lema wa Arusha Mjini ikiwa mashtaka yake yanadhaminika?
La pili, iwapo Mshtaki/Jamhuri (Mkurugenzi wa Mashtaka nchini-DPP) ana kesi zenye ushahidi na uzito wa hoja dhidi ya mshtakiwa Godbless Lema na iwapo kuna nafasi ya kuharakisha upelelezi na kuanza kusikilizwa kwa kesi za msingi, kwanini Jamhuri inatumia nguvu kubwa kwenye suala la dhamana?
La tatu, Mawakili wa Lema kwasasa wanapaswa kufanya nini hasa wakati huu ambapo Jamhuri imeshafika Mahakama ya Rufaa kupinga ruhusa ya Lema kukata rufaa, dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi kukataa kutoa dhamana, nje ya muda?
La nne, Jamhuri ina sababu gani kubwa na ya kisheria ya kuzuia kupewa dhamana kwa mshtakiwa Godbless Lema kwa mashtaka mawili yanayomkabili?
La tano, siku Mbunge na mshtakiwa Lema akikataliwa kabisa dhamana au akikubaliwa dhamana na kuachiwa kuendelea na kesi zake akitokea uraiani, hali itakuwaje na kwa faida ya nani?