Fred Katulanda
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 374
- 509
MAHAKAMA kuu ya kanda ya Mwanza itaanza kusikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita katika jimbo la Ilemela ambayo yalimpa ushindi mbunge Highness Samson (Chadema) dhidi ya Anthony Diallo (CCM), Oktoba 17 mwaka huu.
Shauri hilo namba 12/2010 lilifunguliwa na wakazi watatu wa Ilemela Yusufu Masegeja Lupilya, Nuru Ramadhani Nsubugu na Beatus Martin Madenge, limepanga kuanza kusikilizwa Oktoba 17 mwaka huu mbele ya Jaji Mfawidhi Mjemas wa mahakama kuu kanda ya Bukoba.
Akizungumza na waandishi wa habari msajili wa mahakama wa wilaya ya Mwanza Isaya Arufani alisema katika shauri hilo, wakazi hao wa Wilaya ya Ilemela wanamlalamikia Mgombea ubunge wa Chadema Highness Samson, msimamizi wa Uchaguzi wa jimo la Ilemela ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Willson Kabwe na Mwanasheria mkuu wa serikali.
Baada ya kufunguliwa kwa shauri hilo mwaka jana, mahakama ilipitia hoja za maombi ya kufungua shauri hilo na kujiridhisha, tayari ameshapangiwa Jaji Gadi Mjemas hivyo sasa limepagwa kuanza kusikilizwa mwezi huu wa Oktoba 17, alieleza msajili huyo wa mahakama.
Matokeo ya uchaguzi huo yanayopingwa ni kuwa Highness Samson aliweza kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ilemela kwa kumshinda Anthony Diallo wa CCM kwa kura 31,269 dhidi ya kura 26,270 hii ikiwa ni tofauti ya kura 4,999.
Hata havyo walalamikaji katika upigaji wa matokeo hayo ya uchaguzi wanapinga ushindi huo wakidai kuwa Tume ya Uchaguzi ilihamisha vituo bila utaratibu ikiwa ni pamoja na kuweka orodha ya majina ya wapiga kura ambao ni marehemu hivyo kuufanya uchaguzi kwa jimbo hilo kuharibika.
Wakati huo huo, Msajili wa mahakama ya Wilaya ya Mwanza amesema katika shauri lingine la kupinga uchaguzi wa Matokeo ya Ubunge Jimbo la Mwibara wilayani Bunda limemalizika na sasa linangoja hukumu toka kwa Jaji.
Alisema shauri hilo ambalo ni namba 7/2010 tayari limeshasikilizwa na pande zote mbili na kwamba kilichobakia ni kugojea jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo kukamilisha hukumu yake na ndipo itapangiwa siku ya kusomwa.
Alisema shauri hilo lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa Tiketi ya Chadema Chiriko Harun David dhidi ya Alphaxad Lugora wa CCM, msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Mwibara pamoja na Mwanasheria wa serikali.
Baada ya shauri hilo kusikilizwa mahakama ilitoa muwa wa mwisho kwao pande zote mbili kuandaa majumuisho na tayari wamekamilisha ambapo yamekwisha wasilisha na kilichobakia ni kukamilika kwa hukumu ambayo inatayarishwa na Jaji Chocha, Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Songea, alieleza.