Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Diallo Oktoba 17,2011

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
374
509
MAHAKAMA kuu ya kanda ya Mwanza itaanza kusikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita katika jimbo la Ilemela ambayo yalimpa ushindi mbunge Highness Samson (Chadema) dhidi ya Anthony Diallo (CCM), Oktoba 17 mwaka huu.

Shauri hilo namba 12/2010 lilifunguliwa na wakazi watatu wa Ilemela Yusufu Masegeja Lupilya, Nuru Ramadhani Nsubugu na Beatus Martin Madenge, limepanga kuanza kusikilizwa Oktoba 17 mwaka huu mbele ya Jaji Mfawidhi Mjemas wa mahakama kuu kanda ya Bukoba.

Akizungumza na waandishi wa habari msajili wa mahakama wa wilaya ya Mwanza Isaya Arufani alisema katika shauri hilo, wakazi hao wa Wilaya ya Ilemela wanamlalamikia Mgombea ubunge wa Chadema Highness Samson, msimamizi wa Uchaguzi wa jimo la Ilemela ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Willson Kabwe na Mwanasheria mkuu wa serikali.

“Baada ya kufunguliwa kwa shauri hilo mwaka jana, mahakama ilipitia hoja za maombi ya kufungua shauri hilo na kujiridhisha, tayari ameshapangiwa Jaji Gadi Mjemas hivyo sasa limepagwa kuanza kusikilizwa mwezi huu wa Oktoba 17,” alieleza msajili huyo wa mahakama.

Matokeo ya uchaguzi huo yanayopingwa ni kuwa Highness Samson aliweza kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ilemela kwa kumshinda Anthony Diallo wa CCM kwa kura 31,269 dhidi ya kura 26,270 hii ikiwa ni tofauti ya kura 4,999.

Hata havyo walalamikaji katika upigaji wa matokeo hayo ya uchaguzi wanapinga ushindi huo wakidai kuwa Tume ya Uchaguzi ilihamisha vituo bila utaratibu ikiwa ni pamoja na kuweka orodha ya majina ya wapiga kura ambao ni marehemu hivyo kuufanya uchaguzi kwa jimbo hilo kuharibika.

Wakati huo huo, Msajili wa mahakama ya Wilaya ya Mwanza amesema katika shauri lingine la kupinga uchaguzi wa Matokeo ya Ubunge Jimbo la Mwibara wilayani Bunda limemalizika na sasa linangoja hukumu toka kwa Jaji.

Alisema shauri hilo ambalo ni namba 7/2010 tayari limeshasikilizwa na pande zote mbili na kwamba kilichobakia ni kugojea jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo kukamilisha hukumu yake na ndipo itapangiwa siku ya kusomwa.

Alisema shauri hilo lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa Tiketi ya Chadema Chiriko Harun David dhidi ya Alphaxad Lugora wa CCM, msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Mwibara pamoja na Mwanasheria wa serikali.

“Baada ya shauri hilo kusikilizwa mahakama ilitoa muwa wa mwisho kwao pande zote mbili kuandaa majumuisho na tayari wamekamilisha ambapo yamekwisha wasilisha na kilichobakia ni kukamilika kwa hukumu ambayo inatayarishwa na Jaji Chocha, Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Songea,” alieleza.
 
Mods naomba mrekebishe hiyo heading maana jimbo sio la Diallo. Hakuna mtu anayemiliki jimbo. Huu ni ushamba, kutokujua au ushabiki wa mwandishi
 
MAHAKAMA kuu ya kanda ya Mwanza itaanza kusikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita katika jimbo la Ilemela ambayo yalimpa ushindi mbunge Highness Samson (Chadema) dhidi ya Anthony Diallo (CCM), Oktoba 17 mwaka huu.

Shauri hilo namba 12/2010 lilifunguliwa na wakazi watatu wa Ilemela Yusufu Masegeja Lupilya, Nuru Ramadhani Nsubugu na Beatus Martin Madenge, limepanga kuanza kusikilizwa Oktoba 17 mwaka huu mbele ya Jaji Mfawidhi Mjemas wa mahakama kuu kanda ya Bukoba.

Akizungumza na waandishi wa habari msajili wa mahakama wa wilaya ya Mwanza Isaya Arufani alisema katika shauri hilo, wakazi hao wa Wilaya ya Ilemela wanamlalamikia Mgombea ubunge wa Chadema Highness Samson, msimamizi wa Uchaguzi wa jimo la Ilemela ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Willson Kabwe na Mwanasheria mkuu wa serikali.

"Baada ya kufunguliwa kwa shauri hilo mwaka jana, mahakama ilipitia hoja za maombi ya kufungua shauri hilo na kujiridhisha, tayari ameshapangiwa Jaji Gadi Mjemas hivyo sasa limepagwa kuanza kusikilizwa mwezi huu wa Oktoba 17," alieleza msajili huyo wa mahakama.

Matokeo ya uchaguzi huo yanayopingwa ni kuwa Highness Samson aliweza kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ilemela kwa kumshinda Anthony Diallo wa CCM kwa kura 31,269 dhidi ya kura 26,270 hii ikiwa ni tofauti ya kura 4,999.

Hata havyo walalamikaji katika upigaji wa matokeo hayo ya uchaguzi wanapinga ushindi huo wakidai kuwa Tume ya Uchaguzi ilihamisha vituo bila utaratibu ikiwa ni pamoja na kuweka orodha ya majina ya wapiga kura ambao ni marehemu hivyo kuufanya uchaguzi kwa jimbo hilo kuharibika.

Wakati huo huo, Msajili wa mahakama ya Wilaya ya Mwanza amesema katika shauri lingine la kupinga uchaguzi wa Matokeo ya Ubunge Jimbo la Mwibara wilayani Bunda limemalizika na sasa linangoja hukumu toka kwa Jaji.

Alisema shauri hilo ambalo ni namba 7/2010 tayari limeshasikilizwa na pande zote mbili na kwamba kilichobakia ni kugojea jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo kukamilisha hukumu yake na ndipo itapangiwa siku ya kusomwa.

Alisema shauri hilo lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa Tiketi ya Chadema Chiriko Harun David dhidi ya Alphaxad Lugora wa CCM, msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Mwibara pamoja na Mwanasheria wa serikali.

"Baada ya shauri hilo kusikilizwa mahakama ilitoa muwa wa mwisho kwao pande zote mbili kuandaa majumuisho na tayari wamekamilisha ambapo yamekwisha wasilisha na kilichobakia ni kukamilika kwa hukumu ambayo inatayarishwa na Jaji Chocha, Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Songea," alieleza.

mmmmmmh Wana JF

Hivi huyu Diallo yeye anachokitaka ni nini ? as per yeye navyo mfahamu na elimu yake ya kuunga unga na mpaka kupata Jina la Senegal wakati yeye ni Msukuma wa malya khaaaa.

Hebu turudi sasa kwenye ulingo wa siasa diallo me ningekushauri tu binafsi endesha biashara zako angekuwa kijana mwenzake kama Highness anampinga hapo angarau tunge sema sema ila wewe ulisha zeeka mfano wangu ni tosha kwa umli wa highnes me niko primary skull(Nyanza na Lake) wewe Dialo ukiendesha makampuni yako makubwa na mpaka unaingia siasa nami namaliza Masomo leo hii nachukua jimbo mbele yako ebu huoni tofauti hapo ya umli wa highness na wewe diallo ni aibu yet wataka kwenda mahakamani. its Outrageous Diallo hana kazi nyingine za kufanya
 
Waha wanaojiita wananchi watatu watakua vibaraka wa Dialo, yeye aliona aibu kwanza kushindwa ukizingatia na vyombo vyake vya habari kuipigia kampeni. Sasa wale wapambe wake waliokua wanakula pesa zake wakaamua kufungua kesi ya kupinga matokeo ili kumshawishi Diallo kuwa bado ananafasi nyingine. Na akili zake zilivyo fupi amekubali na anaendelea kuliwa pesa tu. Watu wengine bwana!!!!! akili zimelala kila siku
 
Back
Top Bottom