Sehemu ya mahojiano kati ya Wakili msomi John Malya na Mkuu wa upelelezi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Mrakibu mwandamizi wa Polisi (SSP) Gerald Ngichi.
MALYA: Una miaka mingapi?
SSP Ngichi: 47
MALYA: Ulizaliwa mwaka gani?
SSP Ngichi: 1972
MALYA: Wakati unajiunga na Jeshi la Polisi ulikuwa na Miaka mingapi?
SSP Ngichi: Kimya
HAKIMU: Shahidi jibu tafadhali
MALYA: Kama hukumbuki nikusaidie?
SSP Ngichi: Nilikua na miaka 28
MALYA: Ulikuwa na taaluma gani?
SSP Ngichi: Degree ya Sheria
MALYA: Kwa mujibu wa PGO ni sahihi kwamba mtu akiwa na miaka 28 haruhusiwi kujiunga na jeshi la Polisi?
SSP Ngichi: Inategemea na elimu yake
MALYA: Kesi unayoitolea ushahidi inahusiana na maswala ya uchaguzi nyinyi kama wadau mlipewa elimu juu ya usimamizi wa uchaguzi?
SSP Ngichi: Natolea ushahidi kesi ya maandamano sio mambo ya uchaguzi
MALYA: Lakini hayo maandamano si yanatokana na uchaguzi?
SSP Ngichi: Ndio
MALYA: Ulipewa ratiba ya mikutano ya vyama vya siasa?
SSP Ngichi: Ndio
MALYA: Nani alikupatia?
SSP Ngichi: RPC Kinondoni
MALYA: Yeye alipewa na nani?
SSP Ngichi: Mkurugenzi wa Manispaa Kinondoni
MALYA: Kifungu cha 51 (5) cha sheria ya Uchaguzi kinamtaka Mkuu wa Wilaya ndiye awape polisi nakala ya Ratiba za kampeni. Kwa kifungu hiki, huoni kwamba mmevunja sheria?
SSP Ngichi: Kimya
MALYA: Vituo vya kupiga kura vilikuwa vingapi?
SSP Ngichi: Vingi sikumbuki idadi yake
MALYA: Unasimamiaje uchaguzi ambao hujui hata idadi ya vituo?
SSP Ngichi: Vilikua zaidi ya Hamsini
MALYA: Unafahamu mawakala lazima wale kiapo?
SSP Ngichi: Ndio
MALYA: Unafahamu kila mgombea anaweka utaratibu na Mkurugenzi wa namna mawakala wake kuapa?
SSP Ngichi: Ndio
MALYA: Kwahiyo mlifanya makosa kuvuruga mawakala wa Chadema kwenda kuapa?
SSP Ngichi: Walifanya maandamano yasiyo halali
MALYA: Ulijuaje ni maandamano?
SSP Ngichi: Walivuka barabara
MALYA: kama walivuka barabara ulijuaje kama walikuwa wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba?
SSP Ngichi: Hazifanyiki barabarani
MALYA: Zinafanyika wapi?
SSP Ngichi: Nyumbani
MALYA: Ili ufike nyumbani unapita wapi?
SSP Ngichi: Barabarani
MALYA: Kwahiyo unakubali walikua wanavuka barabara ili wakafanye kampeni za nyumba kwa nyumba?
SSP Ngichi: Waliandamana
MALYA: Kwanini?
SSP Ngichi: Kwa sababu walikua na viongozi wao
MALYA: Wataje
SSP Ngichi: Heche, Matiko, Msigwa na wengine
MALYA: Unajua sifa za mtu kuwa wakala?
SSP Ngichi: Hapana
MALYA: Unajua Heche alikua Wakala?
SSP Ngichi: Sifahamu
MALYA: Unajua Matiko alikua wakala?
SSP Ngichi: Sifahamu
MALYA: Unajua Msigwa alikua Wakala?
SSP Ngichi: Sifahamu
MALYA: Je unakubali kwamba viongozi hao walikua wanaongozana na mawakala wenzao kwenda kwa Mkurugenzi kula kiapo?
SSP Ngichi: Kimya
Hawa jamaa watamuua huyu SSP NGICHI