Kesi ya jack cliff, wabongo wasusia

Kesi ya jack cliff, wabongo wasusia

  • Posted by GLOBAL on July 30, 2014 at 7:50am
  • View Blog

attachment.php

Stori; Musa Mateja

HUKU modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick', akisota jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na polisi nchini humo.

IMG20140726WA00041.jpg

Mrembo almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela' katika muziki wa kizazi kipya akiwa amenaswa na polisi China.

Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupitishwa kwa msako maalum wa kutokomeza biashara hiyo katika viunga vya Mji wa Hong Kong, China.

JUX, PETIT MAN WAPATA WAKATI MGUMU
Kwa mujibu wa chanzo chetu chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva, Juma Khaleed ‘Jux Vuitton' na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow, Petit Man nao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kuunganishwa kwenye oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa madawa ya kulevya nchini China.
attachment.php

Winnie Mandela' wa muziki wa kizazi kipya Bongo akiwa chini ya ulinzi mkali China.

MADAI YA KUBEBA UNGA
Ilidaiwa kwamba Winnie alijikuta mikononi mwa askari wa China akidaiwa kubeba mzigo wa unga tumboni hivyo kukamatwa na kutembezwa mitaani kuelekea kituo cha polisi.

APITA VIZUIZI, AKAMATWA
Ilisemekana kwamba Winnie ambaye ni msichana wa mjini Dar, alifanikiwa kupita vizuizi vyote lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nchini humo ndipo akajikuta akikamatwa na kutembezwa mtaani kama mhalifu wa kivita.

"Unaambiwa ilikuwa kama vita kwani polisi wa China huwa wana silaha za kutisha sana. Unajua Winnie alikamatwa kwenye mitaa ambayo kuna Wabongo wengi hapa Hong Kong," kilisema chanzo chetu kutoka Hong Kong.

Ilidaiwa kwamba askari hao walipokea agizo maalum kutoka kwenye kitengo cha kudhibititi madawa ya kulevya nchini humo kwani kwa sasa nchi hiyo imechafuka kwa uingizwaji wa madawa ya kulevya, jambo ambalo limeifanya serikali ya China ifanye oparesheni kubwa ya kuhakikisha wanatokomeza wimbi hilo.

KWA WABONGO CHINA
Chanzo chetu kilisema kwamba kwa sasa Wabongo wanaokwenda au wanaokaa China wanaishi kama digidigi kwani wamefikia hatua ya kutoonesha pasipoti zao na hata wengine wanadiriki kukataa uraia wao kwa kuwa Wabongo ndiyo wanasakwa kwa wingi.

"Sasa hivi jamaa wakisikia huyo ni Mtanzania wanamfuatilia sana kwani ndiyo wenye sifa ya uingizaji wa dawa za kulevya nchini China," kilisema chanzo hicho na kuongeza:

KAMA HUAMINI MUULIZE JUX AU PETIT MAN
"Hicho ndicho kilichomtokea Winnie. Nakwambia Wabongo wanazidi kukamatwa na madawa ya kulevya. Yaani ni aibu, huwezi kuamini.

"Wabongo wengi sana wamekamatwa Hong Kong na wengine familia zao Bongo hazijui.
"Kama Watanzania hawaamini wawaulize Jux na Petit Man ambao walishuhudia mtiti mwanzo mwisho."

BALOZI WA TANZANIA CHINA
Ili kupata undani na idadi ya Watanzania wanaokamatwa kwa ishu za madawa ya kulevya nchini China, gazeti hili lilimtafuta Balozi wa Tanzania China, Luteni General Abraham Shimbo ambapo simu yake ya ofisini iliita bila kupokelewa.

Wakati Jack Patrick akisubiri kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine mwezi ujao, ripoti zinaonesha kwamba wapo Watanzania wengi waliofungwa na wengine kunyongwa kwa msala wa madawa ya kulevya.
 
Attachments

  • madawa.jpg
    madawa.jpg
    80.2 KB · Views: 3,392
  • madawa 2.jpg
    madawa 2.jpg
    67.9 KB · Views: 3,263
Maskini shetani kishapiga watu ganzi hivyo hata hawasikii kabisaa.
 
Huwa napata kichfuchefu kuona mipaja iliyokunjamana vibaya hivyo au rangi za buluu na nyekundu za kujichubua .Samahani kusema binadamu wanatia kinyaa wakiamua kujiweka vibaya.Kwanini asingevaa hata suruali ndefu.
 
Shauli yake hawasikii wakiambiwa sasa kaingia anga zao
 
Wabongo wajinga,huyu mwandishi ANAANDIKA ETI KAVUKA VIZUIZI VYOTE? Haha..au jamaa walikuwa wakisubiri mahali sheria kali na ushahidi hauna ubishi.NA hivyo kuwa halali yao.Niliwahi waambia wabongo kuwa siku wanashindwa US ujue big fishes wameshajulikana na mtandao mzima upo ktk ushahidi na rada za fbi.Otherwise vinjoa havitashikwa kwanza havina faida na havitalipa gharama za operation wala kufunja mtandao.
 
Kuna Tetesi kuwa Western Powers wanatumia DIA na vijana wa Kitanzania kusafirisha Sembe kwa lengo la kuharibu mataifa ya Asia hususan CHina... Ifike mahala Vijana wetu waonewe huruma jamani, mmeshindwa kutumia utajiri wa nchi kuwapatia ajira ili muwatumie kwenye deals za mauaji kiasi hicho? kwanini CCM hamna Huruma kwa Vijana wetu lakini....
 
We mlevi ulikua wapi. Kitambo sjakuona au ulifichwa na yule mbaba wa kipare
 
Wanyongwe tu na wapigwe masindano ya sumu tu ili wafe,maana sihawataki kuwataja ma lord wao akina....
Mh! Nazihurumia kucha zangu mie nikaage kimya kama sijui!
-ila udhaifu huu wa jei kei kushindwa kuwadhibiti hao jamaa zake kuna pelekea vifo vya vijana wengi wanaodakwa na sembe wakiwa katika harakati za kuitekekeleza sera ya maisha bora.
 
Kuna Tetesi kuwa Western Powers wanatumia DIA na vijana wa Kitanzania kusafirisha Sembe kwa lengo la kuharibu mataifa ya Asia hususan CHina... Ifike mahala Vijana wetu waonewe huruma jamani, mmeshindwa kutumia utajiri wa nchi kuwapatia ajira ili muwatumie kwenye deals za mauaji kiasi hicho? kwanini CCM hamna Huruma kwa Vijana wetu lakini....
Haha..wengine wanaona ni OK kwa waarabu na waislam wote kupeleka magharibi ili kuharibu watoto wao.Ila kwa comrade china sehemu nyingine za Asia ni mbaya.Si sisi ni marafiki nao kuliko yeyote kwanini tuwape kila kitu kuanzia tembo,pori na samaki baharini na madini ardhini, na wanachukua bila huruma...tunawakuwadia kila kitu officially duniani na africa .Ila tunashindwa kataa hilo?Kufikiri ni kufikiri na kuchanganya fikra sahihi sahihi na mbovu kunaweza wapa wengine kipindi kigumu kujua kuwa wapi ni sahihi.Ila kihasilia wewe ndio unaharibu sana ubongo na patterns za kufikiri.Unaleta hisia kutetea usichotaka amini.China ilishaharibika sana, pamoja na kwamba unasikia hizo hadithi,kuna watu wanauza wengine,na kununua malaya, kuna watorishaji,wezi wa tafiti za watu,viwanda vya feki,na madawa na kuaribu wtu ngozi,------ etc..,kuna wachina wanaotaka hela za haraka ndio wanaowatumia wabongo kuingiza mzigo,km wanavyotumia serikali yetu kuwapatia veto UN,kuitawala africa na kupinga mataifa ya dunia,ndivyo wanavyotumia na kua abuse kila kitu.
 
We mlevi ulikua wapi. Kitambo sjakuona au ulifichwa na yule mbaba wa kipare
MSwahili wewe huwezi fikiri kitu kingine.Nilidhani hata ungefikiri kazi ,hata uulize km kazi zimebana ?Kumbe options zako kidogo sana.Unajua waswahili huwa hamna muda wa kufikiri hata kidogo..Naweza kukupa jipu la kweli kabisa ambalo hutataka likubali ukakimbilia kusema nimekutusi.Umewahi jiuliza km mama yako ndie kanificha nikikupa hilo jibu utaweza meza?
 
Hiyo ilikuwa ni siku aliponyongwa.. Si unaona hapo kwenye piacha huyo askari wa China alikuwa na kamba mkononi tayari. Kesi za namna hiyo huwa hazicheleweshwi.
 
tanzania mashamba ya kulima yapo meengi ila utashangaa watu wanabeba unga..

kufen tu si akili hamtaki kutumia bana.
 
View attachment 175071

Stori; Musa Mateja

HUKU
modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na polisi nchini humo.

Mrembo almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela' katika muziki wa kizazi kipya akiwa amenaswa na polisi China.

Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupitishwa kwa msako maalum wa kutokomeza biashara hiyo katika viunga vya Mji wa Hong Kong, China.

JUX, PETIT MAN WAPATA WAKATI MGUMU
Kwa mujibu wa chanzo chetu chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva, Juma Khaleed ‘Jux Vuitton’ na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow, Petit Man nao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kuunganishwa kwenye oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa madawa ya kulevya nchini China.
View attachment 175072
Winnie Mandela' wa muziki wa kizazi kipya Bongo akiwa chini ya ulinzi mkali China.

MADAI YA KUBEBA UNGA
Ilidaiwa kwamba Winnie alijikuta mikononi mwa askari wa China akidaiwa kubeba mzigo wa unga tumboni hivyo kukamatwa na kutembezwa mitaani kuelekea kituo cha polisi.

APITA VIZUIZI, AKAMATWA
Ilisemekana kwamba Winnie ambaye ni msichana wa mjini Dar, alifanikiwa kupita vizuizi vyote lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nchini humo ndipo akajikuta akikamatwa na kutembezwa mtaani kama mhalifu wa kivita.

“Unaambiwa ilikuwa kama vita kwani polisi wa China huwa wana silaha za kutisha sana. Unajua Winnie alikamatwa kwenye mitaa ambayo kuna Wabongo wengi hapa Hong Kong,” kilisema chanzo chetu kutoka Hong Kong.

Ilidaiwa kwamba askari hao walipokea agizo maalum kutoka kwenye kitengo cha kudhibititi madawa ya kulevya nchini humo kwani kwa sasa nchi hiyo imechafuka kwa uingizwaji wa madawa ya kulevya, jambo ambalo limeifanya serikali ya China ifanye oparesheni kubwa ya kuhakikisha wanatokomeza wimbi hilo.

KWA WABONGO CHINA

Chanzo chetu kilisema kwamba kwa sasa Wabongo wanaokwenda au wanaokaa China wanaishi kama digidigi kwani wamefikia hatua ya kutoonesha pasipoti zao na hata wengine wanadiriki kukataa uraia wao kwa kuwa Wabongo ndiyo wanasakwa kwa wingi.

“Sasa hivi jamaa wakisikia huyo ni Mtanzania wanamfuatilia sana kwani ndiyo wenye sifa ya uingizaji wa dawa za kulevya nchini China,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

KAMA HUAMINI MUULIZE JUX AU PETIT MAN

“Hicho ndicho kilichomtokea Winnie. Nakwambia Wabongo wanazidi kukamatwa na madawa ya kulevya. Yaani ni aibu, huwezi kuamini.

“Wabongo wengi sana wamekamatwa Hong Kong na wengine familia zao Bongo hazijui.
“Kama Watanzania hawaamini wawaulize Jux na Petit Man ambao walishuhudia mtiti mwanzo mwisho.”

BALOZI WA TANZANIA CHINA

Ili kupata undani na idadi ya Watanzania wanaokamatwa kwa ishu za madawa ya kulevya nchini China, gazeti hili lilimtafuta Balozi wa Tanzania China, Luteni General Abraham Shimbo ambapo simu yake ya ofisini iliita bila kupokelewa.

Wakati Jack Patrick akisubiri kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine mwezi ujao, ripoti zinaonesha kwamba wapo Watanzania wengi waliofungwa na wengine kunyongwa kwa msala wa madawa ya kulevya.

Ni wakati mwafaka hao wanaokamatwa na hiyo mizigo wakalazimidhwa kuwataja waliowatuma.
 
Ni wakati mwafaka hao wanaokamatwa na hiyo mizigo wakalazimidhwa kuwataja waliowatuma.[/QUOTE Wanajidai wasili sasa dawayao kunyongwa tu jamani ivihakuna mtu mwenyepicha wapokunyongwa kwa maana tumechoka habari zakukamatwa nauyo jux atiliwe mashaka
 
Ninaamini uchaguzi 2015,ukiisha na hii biashara itapungua kwani sasa hivi wanatafuta fedha ya kampeni
 
Back
Top Bottom