Kesi ya jack cliff, wabongo wasusia

Kesi ya jack cliff, wabongo wasusia

sawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
2,752
Reaction score
930
HATIMAYE modo maarufu Bongo
, Jacqueline Fitzpatrick 'Jack
Patrick' amepandishwa kortini kwa mara ya kwanza huko Macau nchini China, Aprili 10, mwaka huu kwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 huku ishu kubwa kwa muda wote aliokuwa mahakamani ikiwa ni kuangua kilio kila wakati.

Jack alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni
mara
yake ya kwanza tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga' Desemba mwaka jana akitokea Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo.
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua hiyo dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za Wachina tu zikimwangilia

"Yeye alijua angekuta Wabongo au hata watu weusi wakimpa kampani, lakini matokeo yake alikutana na sura za Wachina tu," kilisema chanzo chetu.
Kikaendelea: "Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo."
DAKIKA 10 ZATUMIKA KUMSOMEA MASHITAKA
Kuna madai kwamba, msoma mashitaka wa mahakama hiyo alitumia dakika 10 kutokana na taratibu za kisheria za huko huku akitakiwa kusema ndiyo au hapana tu kabla keshi hiyo kupigwa kalenda hadi Mei 23, mwaka huu

KUNA MADAI ALIZOMEWA
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke huo mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa nchi hiyo walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini.
Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au kumsema vibaya mtu aliyedakwa na madawa ya kulevya ni kawaida kwani hakuna biashara, inapigwa vita nchini humo kama ya unga wakiamini unaangamiza nguvu kazi ya kizazi kijacho.
NDUGU WADAIWA KUMKATIA MAWASILIANO
Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.
"Unajua ndugu zake walikata mawasiliano kabisa? Nchi nzima au tuseme dunia nzima kilio ni jinsi vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule kubainika kwamba Jack alibeba unga tumboni kwenda kuuza kumeifanya familia kujisikia vibaya sana," kiliongeza chanzo hicho kikiomba chondechonde kisitajwe gazetini.

KAMA ATARUDI BONGO SALAMA
Habari zaidi zinadai kwamba modo huyo ambaye pia ni Miss Ilala No 3, 2005, aliwahi kumwambia mshirika wake mmoja akiwa mahabusu kwamba, kama atabahatika kurejea Bongo salama,
atakwenda kupiga dua juu ya kaburi la
mama
yake ili amsimamie katika kumwondolea nuksi kama siyo mabalaa. Baba
wa Jack anadaiwa kuishi nje ya nchi.
TUJIKUMBUSHE
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akitokea jijini
Bangkok
nchini Thailand
kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China ambako ilidaiwa ndiko alikokuwa anafikisha unga huo.
Ilidaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kukamatwa kwake ni kuonesha uso wenye uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria, yaani '
passport
' kukutwa imegongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara jambo ambalo wakaguzi waliliona si la kawaida kwa msichana kama yeye

clip_image001_thumb%5B1%5D.jpg

 
Boss Lady!!!! Si ndo alimchomeshaga ngese binti kiziwi?
 
Ndivyo inavyokuwa unapokuwa kipindi cha neema marafiki na jamaa wanakuwa wengi lakini mambo yakiharibika huwaoni.

Pole yake
 
NDIO HIVYO MKUU watu wanajiita mabos lady kumbe kubeba sembe tena sembe zenyewe wanapoziweka wanajua wao wenyewe
dar kujishebedua sana tena sana alihojiwa kwenye kipindi cha wanawake live,hiyo mikoko unaweza kimbia kumbe ni sembe ndio inamfanya aishi mjini
 
sembe zone walimbwende wa bongo
cc masogannge
cc bintikiziwi
 
huyo aliyepata hii habari aliipataje kama hakuwepo mahakamani,muache umbea
 
masai dada inategemea idadi ya watu waliojitokeza walikuwa wangapi?
hasa maboss lady wa china wanaotoka bongo hakuwepo hata 1 si wanaogopa na wao kufuatiliwa mkuu
au umesahau na zile skendo za maboss lady kuuza wadada huko MACAU lazima wakimbie
 
masai dada umeelewa?au na wewe upo MACAU
 
masai dada inategemea idadi ya watu waliojitokeza walikuwa wangapi?
hasa maboss lady wa china wanaotoka bongo hakuwepo hata 1 si wanaogopa na wao kufuatiliwa mkuu
au umesahau na zile skendo za maboss lady kuuza wadada huko MACAU lazima wakimbie

nimeisoma vizuri kasema hakukuwa na ngozi nyeusi hata moja yeye kaipataje kama si ngoz nyeusi?????kwanza aweke source
 
Hawa dada zetu sijui wanaujasiri WA aina gani,waangeutumia kwenye vitu vya halali wangekuwa mbali Sana.tarehe 7 kkutokea Dar kwenda Dubai kwenye ndege ya Emirates kulikuwa na binti mwingine aliyekuwa amejibebebsha hayo madudu yao.toka mwanzo wa safari (tena ilikuwa na delay) mpaka kufika Dubai yule dada alikuwa anahangaika kwa maumivu na uchovu mpaka anatia huruma.inaonekana ilikuwa bahati take maana hatujasikia mtu kukamatwa huko na Mimi sikuweza mfatilia zaidi maana nilikuwa naendelea na safari.
 
Astaghafulila nasema hiv............................... anabahati tungebadilishana na uroda ingekuwa poa.
 
Hana hata lipedejeee likamtoee alikuaga anasema ana pesaa si zimsaidie kumtoaaa hahhhhhahhha pole yakee na Ray C anamuombeaa anyongwee kabisaaa,pole Jack
 
Hiv bint kiziwii jee bado kafungwaaa tu,,hayo madawaa wakiyameza yanawachokeshaa tenaa au wana makubwaaa
 
huyo alijua anafanya kazi ya hatari na alijua fika iko siku atadakwa....kwa hiyo muacheni tu.watu wangapi wanafanya dili haramu na hao hao serikali inawajuaa...kwa hiyo jack clif alipigana ki style yake ...wauza unga wako na wataendelea kuwepo kikubwa kila mtu na akili yake lazima utambie usijingize ktk jambo baaya....
 
Back
Top Bottom