Kesi ya Hamadi na wenzake kunguruma leo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
James Magai na Raymond Kaminyoge

MAHAKAMA Kuu Dar es Salam leo inaanza kusikiliza maombi ya Mbunge wa Wawi, Hamadi Rashid na wenzake 10 waliofukuzwa uanachama wa Chama cha Wananchi (CUF).

Rashid na wenzake, Januari 10 mwaka huu waliwasilisha maombi mahakamani hapo wakiiomba mahakama hiyo iwaamuru wadhamini wa chama hicho waitwe mahakamani wajieleze ni kwa nini wasitiwe hatiani na kufungwa kwa kupuuza amri ya mahakama.

Pia, anaiomba mahakama ibatilishe uamuzi wa Baraza Kuu la chama hicho wa kuwafukuza uanachama na itamke kuwa wao bado ni wanachama halali wa chama hicho.

Wakili wa Rashid na wenzake, Augustine Kusalika alisema jana kwamba tayari wadhamini wa CUF wameshapelekewa wito wa kufika mahakamani leo kwa ajili ya usikilizwaji wa maombi hayo saa 3:30 asubuhi.

Wakili Kusalika alisema hadi jana walikuwa hawajapokea majibu ya madai yao kutoka kwa wadhamini hao wa CUF ambao ndio walalamikiwa katika maombi hayo, lakini akasema kuwa wanaweza kuomba muda mahakamani leo ili waweze kujibu maombi yao.

“Tunatarajia kuwa mahakama itasikiliza maombi yetu leo. Tayari tumeshawa-serve summons (kukabidhiwa wito wa mahakama) Respondent ( wajibu maombi), lakini hadi sasa bado wao hawajatu-serve counter affidavit (hawajajibu maombi).

Hivyo wanaweza wakaomba leo muda wa ku-file hiyo counter affidavit kwani sheria inawaruhusu kufanya hivyo,” alifafanua Wakili Kusalika.

Maombi hayo yatasikilizwa na Jaji Agustine Shangwa ambaye ndiye anayesikiliza kesi ya msingi iliyofunguliwa na kina Rashid na ambaye ndiye aliyetoa amri ya Baraza Kuu la CUF kutokuwajadili na kuwafukuza uanachama Rashid na wenzake.


Katika kesi yao hiyo ya msingi namba 1 ya mwaka 2012, Rashid na wenzake wanahoji uhalali wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho na uteuzi wa wajumbe wake.Kamati hiyo ndiyo iliyowahoji Rashid na wenzake na kisha kupendekeza kwa Baraza Kuu wafukuzwe au kuwasimamisha uanachama.

Amri ya Jaji Shangwa ya Januari 4,2012 kulifunga midomo Baraza Kuu la CUF dhidi ya kina Rashid ilitokana na maombi yao ya Januari 3, 2012.

Katika maombi hayo waliiomba mahakama hiyo iamuru mkutano wa Baraza Kuu la CUF wa Januari 4, 2012 ambao ulikuwa na lengo la kuwafukuza uanachama usitishwe hadi kesi yao ya msingi itakapomalizika.

Hata hivyo licha ya amri hiyo ya Jaji Shangwa, ambayo Hamad na wenzake waliiwasilisha mbele ya Baraza hilo kabla ya kufikia uamuzi wa kuwafukuza, CUF kiliendelea na kutimiza azma yake ya kuwafukuza uanachama.

Uamuzi huo ndio uliowasukuma Rashid na wenzake kurudi mahakamani kwanza kuijulisha mahakama kuwa chama hicho kimepuuza amri yake na kisha kuiomba mahakamani iwaamuru wajieleze ni kwa nini wasitiwe hatiani na kufungwa kwa kupuuza amri hiyo halali ya mahakama.

Akizungumzia uamuzi huo wa CUF kupuuza amri ya mahakama, Rashid alisema CUF wamevunja katiba ya nchi kwa kuidharau amri ya mahakama pamoja na katiba ya chama chao.

chanzo. Kesi ya Hamadi na wenzake kunguruma leo
 
USHAURI KWA HAMADI.

Kama anaamini kuwa anakubalika kwa wapiga kura wake basi akawashitaki CUF kwa wapiga kura wake na achague chama haraka kabla hasira za wananchi hazijatulia. Uchaguzi ukirudiwa mara moja anakuwa mbunge kupitia chama kingine.

Hizi mahakama zetu hazina fedha, hiyo kesi inaweza kuchukua mwaka lakini mwisho wa siku lazima atapoteza ubunge kwa sababu wenzake hawamtaki tena. sasa yanini kupoteza muda wakati mtaji wako ni wannchi wa Jimbo la WAWI?

Kwa Heshima nawasilisha.
 
Back
Top Bottom