Kesi ya Godbless Lema na wenzake Februari 7

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
KESI inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema itaanza kusikilizwa maelezo ya awali Februari 7 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha.

Lema na wenzake 19 walishitakiwa kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali na kutotii
amri halali ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji.

Walifikishwa mahakamani hapo Oktoba 28, mwaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Judith
Kamala, wakishtakiwa kwa makosa matano ya kukusanyika bila kibali, kuhamasisha watu
kufanya vurugu, kutokubali amri halali ya OCD Mwombeji na kula njama ya kutenda kosa.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Rose Sulle aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa
kesi hiyo umekamilikana akaiomba kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza maelezo ya awali.

Kabla ya kupanga tarehe hiyo, Hakimu Judith alimuuliza Lema wapi aliko wakili wao, Method
Kimomogoro, naye akajibu kwamba amepatwa na dharura.

Hakimu Mkazi Judith aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 7, mwaka huu.

Hata hivyo, Lema baadaye aliiomba mahakama hiyo kuzingatia muda wa kuanza kesi akitoa
mfano wa kesi hiyo iliyopangwa kuanza saa 3: 00 asubuhi, lakini ilichelewa kuanza hadi saa 5:00 asubuhi.

Hakimu Judith alisema Mahakama inazingatia sana muda lakini wakati wa asubuhi
wanasikiliza kesi za madai na kuzitolea uamuzi na baada ya hapo ndipo wanasikiliza kesi za
jinai.
 
Mungi!

Tunashukuru kwa ratiba na MUNGU aki2jalia tutakuwa wote hapo!

Hii mbinu ya hii mahakama itaisha tu!
 
Back
Top Bottom