Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
UPANDE wa utetezi katika kesi ya wizi wa Sh1.8 bilioni kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) inayomkabili Rajabu Maranda na ndugu yake, Farijala Hussein, umedai kuwa washtakiwa hao hawana kesi ya kujibu kwa sababu hakuna mtu yeyote aliyetoka (BoT) na kusema kuwa benki hiyo iliibiwa.
"Mahakama inatakiwa kutoa maamuzi kwa kuzingatia ushahidi na si kufanya kazi kwa hisia kwa sababu inaweza ikajiweka katika wakati mgumu kusema washitakiwa wana kesi ya kujibu wakati BoT haijaja kulalamika kama imeibiwa," alidai Magafu.
"Anayestahili kulalamika ni BoT kwa sababu wao ndio waliopewa dhamana ya kutunza fedha hizo na ndio walikuwa wamiliki wa akaunti ya EPA," alidai.
"BoT ina viongozi mbalimbali wakiwemo gavana, manaibu wake, mkurugenzi wa fedha, mkurugenzi wa sera na uchumi, mkurugenzi wa utawala na utumishi na wakuu wa vitengo tofauti, lakini hakuna kati yao aliyefika mahakamani kutoa ushahidi kwamba benki hiyo iliibiwa" alimalizia.
Swali - kwanza, mwizi ni nani, mlalamikaji ni nani na anayeshitakiwa ni nani kwa kumwibia nani. My take - Usanii wa serikali at its best. Wanasheria wa JF, mnasemaje.