Tindikali
JF-Expert Member
- Mar 26, 2010
- 2,128
- 2,914
Serikali Kuu ya Marekani jana imeanza mashitaka kwenye kesi iliyoahirishwa kwa karibia miaka miwili inayomkabili Joachim Guzman Loera, kinara wa miharadati wa dunia kutoka Mexico anaejulikana kama El Chapo, Mtu Mfupi.
Serikali imesema mwisho wa siku itadhihirisha mahakamani kwamba El Chapo, akitumia vikosi vya kitaalam vya mauaji aliua mamia ya Wamexico, alisafirisha madawa tani zaidi ya 200 kuingia Marekani kwa kutumia meli, ndege, mitumbwi na nyambizi, alikuwa na ankara za mishahara kwa maafisa wa serikali waliomlinda, na aliongoza taasisi ya kimataifa ya usafirishaji miharadati ambayo ilimkusanyia ukwasi wa dola bilioni 14 za fedha haramu.
Katika utetezi wake, wakili wake amesema El Chapo amebambikwa mzigo wa kesi na mtandao mpana wa washirika wake, wanasiasa mafisadi, wakiwemo marais wawili waliopita wa Mexico pamoja na maafisa wachafu wa vikosi vya Marekani vya kupambana na madawa ya kulevya ambao waliruhusu madawa kusafirishwa huru. Wakili huyo pia alitamja mshiraka wa El Chapo, Ismael Zambada Garcia, ambae hajawahi kukamatwa, kwamba ndie ndie kichwa cha mtandao wa uhalifu huu.
Hata hivyo waendesha mashitaka wameahidi kwamba wataleta mahakamani milima ya ushahidi yakiwemo madaftari ya rekodi za biashara, msururu wa mashahidi waliokiri kushiriki, picha zilizochukuliwa kwa mitambo ya Satelaiti pamoja na vielelezo vya tani 40 za miharadati iliyokamatwa.
Kabla ya kuanza kwa kesi hiyo mapema asubuhi, Jaji aliwatoa na kuwabadilisha wazee wawili wa baraza, mmoja akidaiwa na jaji kwamba ni mwoga-mwoga na hayupo sawa kusimama kwenye kesi ya El Chapo, ambae ametajwa kwamba ndie mjaalana maarufu na anaeogopwa kupita wahalifu wote wa karne ya 21.
Nchini Marekani kila mshitakiwa ana haki ya kesi yake kuamuliwa na "wazee wenzie" wa baraza, jury of peers, tofauti na mifumo michanga ya kisheria kama ya Tanzania ambapo wazee wa baraza ni kama watazamaji wa mpira, kelele zao za kudai ni penati au sio penati hazimbani mwamuzi aliyedhamiria mshindi.
Chanzo: NY Times