Kesi ya bilioni moja wanayodaiwa polisi Arusha yaahirishwa baada ya jaji kuugua

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
591
1,000
Kesi ya madai ya sh,bilioni moja dhidi ya jeshi la Polisi iliyofunguliwa na mfanyabiashara Mathew Mollel imeshindwa kuendelea katika mahakama kuu ,Arusha mara baada ya jaji anayesikiliza kesi hiyo , dr. Opiyo kushindwa kuhudhulia mahakamani hapo kutokana na matatizo ya kiafya.

Mfanyabiashara Mathew Mollel amefungua kesi ya madai namba 8 ya mwaka 2017,akimshtaki Mkuu wa polisi nchini IGP,RCO Arusha na mwanasheria mkuu wa serikali akiwataka wamlipe kiasi hicho cha fedha baada ya kuikalia Kitako hati yake ya umiliki wa nyumba bila sababu za msingi kwa zaidi ya miaka Minne na kumfanya ashindwe kufanyabiashara zake ikiwepo kukopea benki.

Awali kabla ya kesi hiyo iliyopangwa kutajwa leo Polisi Mkoani hapa juzi walijaribu kuikabidhi hati hiyo katika mahakamani ya hakimu mkazi Arusha mbele ya hakimu Gwantwa Mwankuga ili kuondoa dhana kwamba wanaishikilia lakini hakimu hiyo alikataa na kuwataka waache kopi tu na original waondoke nayo.


351c87c6b83691a74c16d6c5fbfad292.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom