GE2025 Kesi ya Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Kuendelea Kesho Mahakama Kuu Dar es Salaam

GE2025 Kesi ya Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Kuendelea Kesho Mahakama Kuu Dar es Salaam

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuuarifu umma kwamba kesho, Jumatatu tarehe 29 Septemba 2025, shauri lililofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake 2 dhidi ya Bodi ya wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu itaendelea Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Aidha, kesho Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi mdogo kufuatia maombi ya upande wa walalamikaji kuomba kupatiwa nyaraka, zikiwuhusisha mihtasari ya vikao vya Chama.

Pamoja na kwamba, Nyaraka wanazoomba kupatiwa hazina uhusiano na mgawanyo wa rasilimali za Chama, tunasubiri kuona ambacho kitaamuliwa na mahakama katika mazingira ya sasa.

Tunatoa wito kwa wanachama, wapenzi wa demokrasia, na wote wapenda haki, kujitokeza kwa wingi mahakamani kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hii.

Imetolewa leo tarehe 28 Septemba 2025,

photo_2025-09-28_21-04-25.jpg
 
Back
Top Bottom