Kesi ya ajira: Je naweza kushinda kesi bila wakili?

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
620
342
Ni kesi ya ajira ninayotarajia kufungua hapa CMA mjini Iringa.

Kesi yenyewe ni unfair termination yaani mwajiri kakatiza mkataba wangu kiuonevu. Taratibu za kumwachisha kazi mwajiriwa ninazijua vizuri sana. Vipengele vya sheria alivyokosea mwajiri navijua vizuri pia.

tatizo langu ni kwamba sina fdha ya kutosha kuwalipa mawakili lakini sidhanikama mtu hakosi haki yake pale CMA kwa sababu tu hana wakili.

Naomba kusaidiwa, je mtu unaweza kushinda kesi ya namna hii bila kuweka wakili. Kuna tofauti gani kati ya kuweka wakili na kutokweka.

je, ni maelezo gani ninatakiwa kuyasema nikiwa sina wakili.

Nitashukuru nikisaidiwa haya maswali.
 
Kuwa muwazi Mkuu,situation yako ikoje na ni vipengele gani unavyovijua na vimekosewa,ili wadau wakusaidie kwa kujua specific angles!!!
 
Hivi chama cha wafanyakazi wana mchango gani juu ya mwajiriwa alionewa? Na je vilianzishwa kwa malengo gani kama sio kuwa watetezi wa wafanyakazi wanao nyimwa haki, ama ni kwa kiasi gani wanatoa semina kwa wafanyakazi kwa kuwafumbua haki zao za msingi katika kila mkoa na hususani hatua za kuchukua kwa mfanyakazi alionewa, kimsaada huwa wanatoa msaada gani hasa kwa kisheria kwa mfanyakazi alionewa maana kuna percent inakatwa kwenye mshahara kwende kwenye mifuko ya chamani kwa mfano TUICO ili kukipa uhai chama sasa basi tukipata majibu ya maswali yote hayo basi mleta mada mjadala wako utapata ufumbuzi wapi pakuanzia

Kwa upande wako binafsi sasa, juhudi za kuitafuta haki, kama victim, nafahamu termination of contract kuna vielelezo lazima vizingatiwe kukamilisha zoezi la termination mfano kupewa notes, kama mkataba bado haujaisha kuna malipo utalipwa kwa siku, miezi ama miaka iliyo bakia kwa kuangalia terms and condition za mkataba, wewe binafsi unaweza kushtaki bila hata wakili kama unajuwa kuna vitu havikuzingatiwa, wengi wanao pendelea kumchukua wakili unakuta kwenye kesi tata yani kesi inayo taka mbobezi katika mambo ya kisheria technical know how, ila kama ulivyosema vifungu fulani fulani umeona vimekiukwa na unavijuwa na viko wazi kabisa basi nikutie moyo tu hata wewe unaweza jisimamia kesi na ukashinda bila gharama yoyote na ukatoboa na siku ya mwisho kupata remedies zako na stahiki zako vizuri kabisa
 
Chodawu huwa wanato msaada wa kisheria mkuu...pia zipo Legal NGOS nyingi zinatoa msaada
 
Ni kesi ya ajira ninayotarajia kufungua hapa CMA mjini Iringa.

Kesi yenyewe ni unfair termination yaani mwajiri kakatiza mkataba wangu kiuonevu. Taratibu za kumwachisha kazi mwajiriwa ninazijua vizuri sana. Vipengele vya sheria alivyokosea mwajiri navijua vizuri pia.

tatizo langu ni kwamba sina fdha ya kutosha kuwalipa mawakili lakini sidhanikama mtu hakosi haki yake pale CMA kwa sababu tu hana wakili.

Naomba kusaidiwa, je mtu unaweza kushinda kesi ya namna hii bila kuweka wakili. Kuna tofauti gani kati ya kuweka wakili na kutokweka.

je, ni maelezo gani ninatakiwa kuyasema nikiwa sina wakili.

Nitashukuru nikisaidiwa haya maswali.
Wewe mdanganywa upo? Mbona unaanzisha uzi wa kutaka ushauri halafu unaingia mitini
 
Uzi wa zamani huo Mkuu
Sio zamani, juzi kati tu aliomba ushauri na mimi pia nikamshauri sasa hajarudi kutoa mrejesho amefikia wapi mkuu, wengi hujifunza kwa yale yanayo mtokea mtu sasa angerudisha mrejesho ili watu wajifunze kwenye swala hili la kudai haki zao punde wanapo pata manyanyaso kutoka kwa mwajiri ni hilo tu...
 
Back
Top Bottom