Kesi ya ACACIA

Ccm ndio wakulaumiwa daima pamoja na Yohana ambaye hakuwahi kukataa kupitisha miswaada ya kipuuzi hivi
 
Fukuza hao wasengeli wametufilisi sana. asilimia 4 ndo nini hatupati hasara tukiwafukuza cha kufanya mchanga ule tugawane tusugulie masufuria kwa dharau. Madini tuchimbe wenyewe kama hatuwezi watakuja kuchimba wajukuu zetu.
 
Tusiwafanye wajinga wewe na nani? Usitumie PLURAL - Jizungumzie Mwenyewe
 
Ilikua 3% miaka yote, tulipo lia sana wakaongeza 1% ndio tunapata sasa hiyo 4%.
Jamani hebu tujitahidi kuyaelewa haya mambo bila mihemko. Hiyo 4% ni mrabaha na inalipwa kwenye gross value. Hapo mwekezaji bado hajatoa gharama za mtaji na uendeshaji. Bado atatakiwa kulipa kodi kibao kama kodi ya mapato ambayo ni 30%, SDL, PAYE, withholding tax, service levy nk. Kiuhalisia serikali inapata zaidi 45% ngoja wajuzi waje watupe figure kamili ya government take. Tupambane kuboresha maslahi ya taifa lakini tuepuke kupotosha, tutaishia kuwalaumu viongozi wetu
 
kwenda zako wewe usitutishe. hata kama mitego ya acasia kisheria ikoje lazima tujikwamue kwa huu ujambazi. hapa ndio hata lissu kama gwiji la sheria kweli kuonyesha uzalendo wake..wale wanaosema as a nation we should remain still na na kukubali kubakwa kiuchumi they can go to hell.
 
Mh wewe uko timamu kweli?
 
Mi nasikilizia tu hili sakata lakini naombea serikali ishinde katika hili
 
Mi huwa ni mvivu sana kuandika ninge andika kuuelezea huu mgodi ulivyo undergroud wa tanzania wangeona maajabu.
 
CCM walaaniwe pamoja na kizazi chao chote kumbe walishauza ardhi ya migodi pamoja na kile ambacho kiko chini ya ardhi kumbe ndio maana watanzania wakithubutu kutia mguu ndani ya ardhi ya migodi wanapewa zawadi ya risasi na wawekezaji na hawafanywi kitu chochote kwa kuwa ardhi na kilichopo chini ya ardhi kimebinafsishwa kwa wawekezaji.

Tusipokuwa macho na CCM tunaweza tukafikiri tuko huru kumbe tulisha pigwa bei zamani pamoja na nchi yetu.
 
Wabunge wa upinzani walitoka nje Kipindi hizi sheria zinapitishwa ,mkawaona hawana akili, leo mnasema wamenunuliwa. Msiejitambua ni nyinyi tena hata huyo anayejifanya mzalendo No1 alikuwemo kwenye baraza, ni mnafiki tu
uliwaona wanatoka nje au umeota?
 
Makinikia ya Magufuli safari hii lazima yawawowe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…