Kesi ya ACACIA

Wafukuzwe tuu eheeee acha wee , hao watu wapo kimkataba. Uwezi kufukuza kampuni kama Acacia kama unamfukuzisha kazi shamba boy,

Gharama wanazoleta ni kubwa,..tizam wamekamat kontena ngapi,na hili ilikua LA muda mrefu,na ukitizama report zao za mahesab wanapata loss tokea waanze,..sasa we unaona sawa akili zako si za apa,
 
Umeongea point
Na kwa facts
Mungu akubariki kaka
Viongoz wetu wanahitaji weledi mkubwa katika swala hill na cyo mihemko
 
Wala tusimtafute mchawi eti wawekezaji wanatuibia serious??wanaibaje??lete mkataba tuusome kama kweli wanatuibia.Siasa tunaipeleka kila mahali ila katika hili mimi sipo na mkulu,nachoona kitatokea hapo mbele ni kama wale samaki wake aliowakamata serikali ikashindwa kesi na kulipa bilioni tatu.
 
Umeongea point kaka
Mungu akubariki
 
Ni mikataba wa uwizi aliyoingia Mwekezaji ACACIA na nani sijui..maana wauita mkataba wa ACACIA wakati ni mkataba wa uwekezaji umeridhiwa na pande zote yaani Serikali na wao. Acha mahaba kaka jaribu kuwa msomi na sio mwanasiasa.
Mwambie huyo kaka
 
Umeandika Kisiasa zaidi kuliko Kisheria. Vyovyote Iwavyo - ACACIA WAMEFANYA UDANGANYIFU NA KWA HILI HAWATAPONA - JUHUDI ZAO ZA KUJIKWAMUA NI NYINGI SANA NYUMA YA PAZIA LAKINI SAFARI HII HAWATATOBOA - NI AFADHALI WAONDOKE NA TULIPE FIDIA KULIKO KUBARIKI WIZI WA MCHANA
 
Wakikurupuka si ndio furaha yako upate kuandika mipost yako kama mwendawazimu.... siasa zimekutoa akili ila bado hujajielewa kama wewe ni chizi siasa.
Mkishauriwa wabishi saa hizi ndio mnapiga mayowe.Hiyo hasira yako wapelekee ma-ccm wenzako waliosaini mikataba.

Ukipanda Bangi huwezi kuvuna mahindi.
 
Sasa si mkubali Tume Huru kama ACASIA walivyoshauri mambo yaishe?
 
Hapa kuna mambo mawili! kwanza unasema mchanga ni wa serikali na hivyo unajitahidi kutuaminisha kuwa siyo ya Watanzania bali ni ya wawekezaji!!! Pili unajivua Utanzania wako ... Lazima ifike mahala tuache unazi wa kichama....no matter what, tunatakiwa kupaza sauti kama taifa kukataa unyonyaji huu ...
 
Tuna pata asilimia 4 yaani 4% bora kuacha kuchimba madini
iko hivi,
-mrahaba 4%.
-corporate tax 30%
jumla 34% kama sikosei

mfano ghana

mrahaba 5%

cooprate tax 25%.

Kwahiyo sio kwamba tunapata 4% tu.

Sema tax holiday wanapewa ndefu mno,

mfano geita mine ilianza uchimbaji 2001,wamekuja kuanza kulipa kodi 2011,
yaani incentive tax ya miaka 10,

wakati Nigeria tax holiday miaka 3.
 
well clarified
 
Exceleent. Kuna haja ya rais kuwa makini. Hata wanapokuja kusachi chumbani kwako lazima mwenye chumba uwepo hawawezi wakasachi ini your absence halafu wakasema tumeona hiki au kile. Wakifanya hivyo una haki ya kukataa kuwa hicho hukijuwi na kuwa wamekubambikia
 
Wangefukuza tu ii acacia,..INA gharama kubwa
Hiyo siyo rahisi mkuu. Sawa na kuoa mke unamwoa kwa sherehe kubwa lakini siku ukitaka kumfukuza huwezi kumfukuza kama mbwa ni lazima sheria zifuatwe na anaweza kugoma kuondoka na usiweze kumfanya kitu
 
Nasikitika kuona mtu anasema eti madini ni mali ya wawekezaji. Huu ni ujinga tulio jengewa tayari. Serikali kwa taarifa yako ni mubia namba moja wa hii migodi na wala hawajauza madini kwa acasia. Wamepewa wawekeze kwa kuleta mitambo ya kuchimbia faida tugawane. Shida ni pale wanaposema wanatumia gharama kubwa mno kuliko wanachovuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…