KESI haiishi,WAHITIMU hawaishi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KESI haiishi,WAHITIMU hawaishi...

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by VUTA-NKUVUTE, Apr 13, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Ile kesi ya wanafunzi 172 na wengine inayohusu wanafunzi hao kukataa vyeti vya Chuo Kikuu cha Ardhi na kutaka vya UDSM imechukua sura mpya.Kesi hii iliyoanza mwaka 2007 ipo mbele ya Jaji Dr.Feuz Twaib wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Kanda ya Dar es Salaam.

  Ilivyokuwa: Wanafunzi walipata udahili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya UCLAS(sasa Ardhi University).Wakati wameshasajiliwa na kuanza masomo,UCLAS ikawa chuo kamili:Ardhi University.Walipomaliza masomo yao,Ardhi wakataka kuwatunuku vyeti wanafunzi hao.Wanafunzi wakagoma.Wakafungua kesi.Wakaiomba Mahakama Kuu itoe amri kukishinikiza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiwape vyeti vyao.Jaji Twaib akawapa amri waliyoiomba.Utekelezaji ukaanza.Katikati pakatokeo jambo.UDSM na Ardhi wakataka kugawana wanafunzi wa kuwapa cheti huku na kule.

  Wanafunzi wakagomea hilo tena.Wakamrudishia Jaji Dr.Feuz Twaib hukumu yake aitafsiri kwa njia ya maombi maalumu kisheria.Jana ilikuwa siku ya hukumu.Kesi imeahiriswa hadi tarehe 19 mwezi huu.

  Kimsingi,wanafunzi hawa hadi sasa hawana vyeti.Hawaajiriki.Wataishije? Nani alaumiwe hapa?

  Kesi yajulikana kama:Lelo Didas and 171 Others versus 1.ARDHI UNIVERSITY 2.UDSM 3.ATTORNEY GENERAL
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Hoja yako nzuri sana lakini hasa unataka tuchangie nini/kwa vipi. labda kwa swali la nani alaumiwe, ni vyuo hivyo tu hasa UDSM, mkataba wa masomo upo na UDSM and not otherwise. Kama kungelikuwa na transfer of contract, both parties should agree to the terms of transfer and not one side. Remember in law of contract,m, both parties agree to the terms of the contract. It seems in this case one party dictated the terms of the contract by transfering student registration to UCLAS without the consent of the other party(students). The UDSM is the ones to blame
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Nadhani uongozi wa UDSM na hata UCLAS/AU ulikurupuka katika kufanya maamuzi kuhusiana na transitional arrangements.

  Hata hivyo ni kwa nini hao wanafunzi wasingekubali vyeti vya AU na kisha kudai hivyo vya UDSM mabavyo ndio kimsingi/kisheria wanastahili? Wakati wanaendelea na kesi wangetumia hivyo vya AU kuajiriwa au kuendelea na masomo ya juu badala ya kupoteza muda wote huu wa miaka 5!
   
 4. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aisee mbaya sana hii, inamcost sana mdogo wangu maana nae ni mhanga wa hii kitu.
   
Loading...