Bank ya CRDB tawi la Turiani ni tatizo

Bank ya CRDB tawi la Turiani ni tatizo

Wegr

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2022
Posts
230
Reaction score
602
Wapendwa sitaki kuwachosha wakati wenyewe tulishachoshwa na maisha, niende moja kwa moja kwenye malalamiko.

Jamani hii sasa sio kero bali ni tatizo kwetu sisi wateja wa CRDB tawi la Turiani sio ndani wala ATM panapofanyakazi, ndani ntiti nje ntiti yani ndani kumefungwa na nje [emoji763] ujumbe uliop ni HUDUMA HAIPATIKANI KWA SASA yaani ni tatizo jamani wahusika tunaomba mtusaidie jamani, ukienda kwa mawakala unatoa hela lakini risit haitoki sababu ya mtandao na yeye hakupi hela akihofia pesa kurudi kwenye acc ya mteja na hii ni tangu jumapili mpaka mda huu naandika hakuna huduma tunapata.

Cha kushangaza ni tawi jipya halina hata miezi sita lakini adha tunayopata sio haki kabisa.
 
Mwisho wa mwezi + Sikukuu mashine zinazidiwa.
 
Kadi Yako ni ya ni visa card ...so mkuu katoe kwenye benk nyingine...... Nmb,NBC n.k
 
Back
Top Bottom