Kero zangu kwa Abood Bus Service

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,831
33,219
Napenda kuuandikia uongozi wa Kampuni ya Abood Bus Service juu ya kero kadhaa, kwanza niseme wazi kuwa lalamiko hili halijalenga kuichafua kampuni bali kuijenga kwakuwa mimi ni regular traveler kwa kutumia kampuni hiyo, vilevile sijalenga kumharibia kazi mtu yeyote ila nahimiza kutazama mambo ya msingi katika utendaji kazi na kustawisha utaifa wetu.

Nilisafiri na bus namba T868 DJP siku ya Jumapili tarehe 25.4.2021, kutoka Dsm kwenda Morogoro, safari ilianza Ubungo majira ya saa 6:33 mchana na ilikuwa njema, dereva alikwenda mwendo mzuri kabisa ambao hakuna abiria aliyeulalamikia , intertainment kwenye screen zilikuwa kwa sauti ya kawaida ambayo haikuwa na kero kwa wasafiri.

Lalamiko langu linakuja ilipofika majira ya saa 10:41 - 10:44 jioni tukiwa eneo la Kingolwira ulichezwa muziki mmoja ambao sikufanikiwa kusoma jina unaitwaije, lakini muziki ule ulimalizikia kwa maandishi UNIVERSAL (nasikitika sikuweza kurekodi video husika), muziki ule kiukweli haukuzingatia kabisa maadaili ya utanzania wetu kwa maana ya kwamba wachezaji wake walikuwa uchi kabisa na wengi wa wachezaji wale walikuwa ni wanawake ambao chuchu zao zilionekana wazi na hata sehemu za siri zilionekana wazi, kwa wanaoujua muziki huo wanaweza kutusaidia kwakuwa wachezaji hao walionekana kwenye matope wakati fulani.

Binafsi nadhani ifike mahali Mheshimiwa Abdulaziz Abood ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Abood, uwe makini na madereva wako na hasa linapofika suala la burudani kwenye mabasi, madereva wale si wote wenye kuheshimu utu, ni kama wanaona wasafiri wote ni wahuni wapenda ngono, na tafsiri yake ni kwamba kampuni yako inamtazamo wa kuendekeza sana masuala hayo, binafsi nakufahamu Mh. Abood kuwa ni Muislamu safi usiyeshabikia mambo ya kihuni kihuni, najiuliza maswali kadhaa,
  • Je, nini kinawafanya madereva kupenda sana kuweka video za nusu uchi na uchi kamili kwenye eneo ambalo watu wanasafiri na wake zao, wakwe zao, binti zao, mama zao, baba zao?
  • Je, entertainment ya mtanzania wa leo ni mambo ya uchi tu?
  • Hakuna mambo ya msingi yanayoweza kuonyeshwa kwenye public ili kulinda heshima za wasafiri na kampuni?
  • Hao madereva hawapewi mafunzo?
  • Ni nani aliyewaambia kuwa wasafiri wa Abood ni wapenda picha za ngono?
  • Kama wapo wanaotaka picha hizo si wakazitazamie kwao badala ya kwenye bus?
  • Kwanini madereva wanashindwa kuheshimu watu wengine?

Wanaosafiri kwenye mabasi yale ni watu wa aina mchanganyiko na wenye heshima zao, wasichukuliwe poa, wapo watoto, vijana, wazee wa aina zote wa kiume na wakike, waislamu, wakristo na hata wasio na dini, utamaduni wetu wa kitanzania haujatufikisha hapo kwenye kutazama picha za namna ile kwenye public, abiria wengi tulikwazika na jambo lile, inawezekana dereva hakujua kwakuwa yeye mwenyewe hakuwa mtazamaji wa kinachoendelea kwenye screen, upo uwezekano wanaojaza hizo burudani kwenye flash ni vijana wenye mtazamo huo wa kingonongono na hivyo dereva kujikuta anatumbukia kwenye mtego pasipokujijua, na kama anajua basi ana matatizo kichwani.

Itoshe kusema kwamba Mh. Abood, tunaupenda sana usafiri wako, ni usafiri mzuri, mabasi yanasafishwa vizuri, mwendo mzuri, lakini kuna jambo la kulitazama kwa jicho la karibu, ikikupendeza tunaomba:-
  • Madereva watambue kuwa wanaosafiri kwenye mabasi yale siyo vijana wa kizazi kipya tu, wapo rika zote,
  • ikikupendeza Mh. Abood weka timu itakayo screen flash zote zinazochezwa kwenye mabasi zisiwe hizo za nusu uchi na uchi kamili, na siyo kweli kwamba wote wanapenda mambo yale, ila ni kwamba watu wanakosa sehemu ya kupitishia malalamiko yao (suggestion box)
  • Pamoja na miziki, burudani zipo nyingi, kuna michezo mbalimbali kama mipira, mbio za magari, mashindano ya pikipiki, vipindi elimishi kama kilimo, ufugaji, utalii, mafundisho ya dini (huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani) na program nyingine nyingi zenye kumfurahisha kila mmoja na siyo picha za uchi, mambo ya hivyo yasubiri muda na mahali pake na si kwenye public services.
Naomba radhi kama kuna aliyekwazika na bandiko hili, ila message sent.
 
maadaili ya utanzania wetu kwa maana ya kwamba wachezaji wake walikuwa uchi kabisa na wengi wa wachezaji wale walikuwa ni wanawake ambao chuchu zao zilionekana wazi na hata sehemu za siri zilionekana wazi, kwa wanaoujua muziki huo wanaweza kutusaidia kwakuwa wachezaji hao walionekana kwenye matope wakati fulani.

Tatizo ktk lugha ya kiSwahili kuna maneno machache ya kuelezea jambo kiuhalisia, bora lugha ya Kiingereza imesheheni maneno ya kuelezea uhalisia, mfano maneno nude / naked yana maana tofauti.

Si ajabu wanaJamiiForums wakadai utupie picha ili waweze kupata uhalisia lakini kama ulivyosema hukufanikiwa kupata video clip au picha mnato wanaJF watoe hukumu kuhusu maadili .
 
Si ajabu wanaJamiiForums wakadai utupie picha ili waweze kupata uhalisia lakini kama ulivyosema hukufanikiwa kupata video clip au picha mnato wanaJF watoe hukumu kuhusu maadili .
Asante Mkuu, nilitamani nirekodi kipande kisicho na picha uchi ila sehemu ya picha kwa ushahidi tu ili wanaoijua hiyo video waizungumzie vilivyo na si vinginevyo
 
Tatizo ktk lugha ya kiSwahili kuna maneno machache ya kuelezea jambo kiuhalisia,
Naliona tatizo hilo hata hapa moderator ame edit title yangu inasomeka "Kero zangu kwa Abood Bus Service" binafsi naona kama mimi ndiye ninayesababisha kero kwa Abood Bus Service:)
 
Umeandika parefuuuu kero n video inaitwa UNIVERSAL ....hahaa ( DUNIA HAITASMAMA UKIGOMA KUTEMBEA NAYO...)
 
Tatizo lenu huu mwezi mbataka kila mmoja afuate mnachoamini. Tafsiri ya nusu unayotoa ni tofauti na watu wa amani nyingine , mila nyingine na mataifa mengine. Kwenye jamii mchanganyiko ustaarabu ni kuchagua kukifuata unachokiamini na kuacha watu wengine waamini wanachokitaka,
 
Pole sana Marx, ujumbe utamfikia Abood.. ..mimi nikiwa safarini huwa nakereka sana miziki yao
Upo sahihi mkuu, jinsi ilivyo ni kama miziki ya dezaini ile ndicho kivutio pekee cha wateja, kwa maneno mengine ni kwamba wabongo ni wapenda picha za ngono, kwahiyo ili upate wateja basi weka picha za uchi
 
Upo sahihi mkuu, jinsi ilivyo ni kama miziki ya dezaini ile ndicho kivutio pekee cha wateja, kwa maneno mengine ni kwamba wabongo ni wapenda picha za ngono, kwahiyo ili upate wateja basi weka picha za uchi

Ni ujinga kabisa, madereva/makonda wa style hiyo hawafai kabisa.
 
Lakini ukifuatilia Miziki hiyo hiyo ndio inayochezwa kwenye Vituo vya TV na Radio, na wao wanaoingiza hizo Nyimbo huwa wanachukuwa zile ambazo zinaonekana kufanya vizuri..,
Hivyo wa Kulaumiwa hapa ni hao wanaoruhusu Nyimbo zisizo na Maadili ama maudhui sahihi kuja kwa Walaji, kama Nyimbo hizo zingefungiwa sidhani kama zingeoneshwa huko kwenye Usafiri wa Umma!!!
 
Lakini ukifuatilia Miziki hiyo hiyo ndio inayochezwa kwenye Vituo vya TV na Radio, na wao wanaoingiza hizo Nyimbo huwa wanachukuwa zile ambazo zinaonekana kufanya vizuri..,
Hivyo wa Kulaumiwa hapa ni hao wanaoruhusu Nyimbo zisizo na Maadili ama maudhui sahihi kuja kwa Walaji, kama Nyimbo hizo zingefungiwa sidhani kama zingeoneshwa huko kwenye Usafiri wa Umma!!!
Sawa Mkuu, labda wanaohusika na haki za wasafiri nao wanapaswa kulaumiwa kwakuwa hawasimamii majukumu yao vilivyo, ila ile video ni kama waliitoa youtube sidhani kama ni ya kitanzania sijawa na utaalamu sana wa kuzitofautisha,
 
Back
Top Bottom