Kero za wateja kwa watoa huduma

Kero za wateja kwa watoa huduma

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,074
Reaction score
11,270
Mteja ni mfalme,,,

Tumesemwa sana watoa huduma kuwa tuna lugha chafu, tunachezea simu muda wa kutoa huduma, muda wote hatuna change na mambo kibao. Sasa ngoja tuone upande wa pili wa wateja ukoje?

Aisee wateja wa bongo ni wasumbufu sana kuwahudumia inatakiwa usiwe na bandama wala nyongo ili hata akikushika mata** usikasirike la si hivyo utamtimua asirudi tena

Kwanza wengi hawajui kusoma wala kuandika, anaweza akakataa kitu wakati maandishi yanaonesha mfano umuuzie vocha ukamuingizia akakatwa na message katumiwa na deni lililobaki linaonesha na bado atakwambia hujamtumia na atajaza nzi wengi sana

Huwa hawafuatilii vitu vidogo vidogo wakawa na elimu navyo hata kwa uchache, utakuta mteja anamlalamikia wakala kamkata ela nyingi(makato ya kawaida sio lipa) wakati makato huwa hakati wakala bali kuna chati za miamala zinaonesha makato na hata umuoneshe hataki kuelewa

Mteja anakupa elfu 10 anataka kitu cha jero waenda hangaika change ukirudi ukimrudishia anatoa rundo la pesa za change anachanganya na ulizompa anaweka kwenye waleti au kipochi(dadeq) sasa unajiuliza huyu ni kopela au nini? Na hii inafanya siku nyingine hata hana kweli unamwambia tu sina change

Dah! Wateja huwa wana lugha za kukatisha tamaa sana, unakuta unauza duka limejaa mavitu ila kitendo cha kuuliza vocha ukamwambia sina aisee atafoka na kutukana na kukwambia "funga basi sasa hapo unafanya kazi gani maana kila kitu wewe huna"

Zipo nyingi sana izo ni chache tu

Ombi: ni kweli wateja wetu nyie ni wafalme lakini ufalme wenu unatokana kuwa na wahudumu hebu jaribuni kutuhurumia watoa huduma nasisi ni binadamu kama nyie tuna nyongo na bandama na mambo mengine tuhurumiane mtupe hela zenu nasisi tuwape huduma au bidhaa ni hayo tu
 
Sawa tumekusikia muhudumu wa m pesa .
Tunaomba maoni ya muhudumu wa bar na gest ....
IMG-20240705-WA0078.jpg
 
Hayo mambo ni hukohuko kwenu Maswa, Magu, Geita.
Hujakutana na wateja wa mbagala mkuu, hata hao wa Geita Wana nafuu.
Wateja wa mbagala (asilimia kubwa ni makabila toka kusini) ni wabishi sijapata kuona.
Anaenda kwa wakala kuweka pesa. Asipoona sms anakujazia watu. Unamwambia ndugu hela imeingia kwenye account angalia salio, Wala haelewi yeye anataka aone sms tu.
Ni wabishi Hawa watu sijapata kuona.
 
Nikiwa na miaka 11 nilianza kuuza duka pale nyumbani utaratibu wangu ni kumuhudumia kwanza yule aliefika kabla ya mwenzake kuna wale wateja wababe anakuta wateja 10 kabla yake na anataka ahudumiwe wa kwanza hadi kichwa kinauma

Usipokua na elimu ya biashara unaweza kuwaona kero na ukagombana nao kumbe inatakiwa ukishaona wateja wanazidi kuongezeka siku hadi siku unatakiwa uongeze idadi ya watoa huduma ili huduma ziwe bora na haraka zaid

Mteja kuwa na maswali mengi ni kawaida hiyo na unatakiwa umjibu ndo maana inatakiwa uwe na ujuzi/elimu ya huduma unayoitoa kwao
 
Kusoma hajui kuangalia salio ataweza!
 
Elimu na uzoefu na pia usiwe na hasira za haraka utaweza na watakupenda
 
Back
Top Bottom