Umepewa ya uso tayari...!!
Uandishi haujawahi kuwa kazi rahisi hasa kwa mtu ambaye kazi yake sio uandishi.
Ila usiache kusaidia pale kanuni za uandishi zinapokosewa Ila jitahidi kuwa mtu wa kutoa msaada na sio mkosoaji.
Nimeamua kutobishana naye, nukta yangu haipo kwenye mukhtadha alio onesha yeye, hata hivyo nipo sahihi, angalia:-
1. Kero ya uandishi m-baya...
(Uandishi m-baya wa nini?)
2. ...wa maneno
Sahihi kabisa. Ni kero moja ya uandishi m-baya...
Tuachane na hilo, nukta yangu bado ipo pale pale kwa wale ambao NAAMINI WAMESOMA KISWAHILI, lakini bado wanashindwa kuandika vizuri baadhi ya maneno, tena kwa kurudia kosa ama makosa hayo hayo mara kadhaa.
Wale wanaofupisha neno ama maneno kwa usahihi wala kwangu siyo kero, ukiandika KTK badala ya KATIKA mie hainipi kero, labda wale wanaoandika XAXA badala ya SASA, sijui hata wanafupisha nini, aaaaggggrrrrr!
FORTUNATUS ukiandika 42&2C angalau inaeleweka, lakini siyo ASUBUHI uandike HASUBUI, ingawaje wale walio athiriwa na lafudhi za lahaja zao wakati wakitamka hawanikeri, ila wakiandika kwa kukosea napo kwangu inakuwo ni kero.
Sizungumzii "typing errors", makosa ya typing inaeleweka.
Msingi wa uzi ulikuwa kuangalia huko mashuleni walifundishwa hivyo!? Ama ni nini kimetokea, maana vijana wengi wanaandika hovyo.