decomm
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 726
- 655
Habari?
Hongera CAG mstaafu kwa kustaafu kwa heshima na karibu CAG mpya.
__
Moja kwa moja niende kwenye mada.
Ninaamini wadau waliomo humu wamepata elimu angalau ya darasa la saba, kama wapo wa chini ya hapo basi ni wachache sana.
Lakini bado najiuliza hivi ni kweli bado watu wanakosea kuandika maneno kwa usahihi licha ya kukaa shuleni zaidi ya miaka minne?
Sizungumzii "typing errors", bali nazungumzia kutokujua tofauti ya neno fulani na fulani ambayo ni maneno ya kawaida sana na hutumika kila siku. (nitatoa mifano)
Pia sizungumzii wale wanaoandika neno kwa usahihi lakini kutokana na lahaja ya alipozaliwa au kukulia akalitamka neno hilo tofauti kidogo, hii hainipi kero.
Nakerekwa na uandishi kama huu:
1. Abari, habali, abali badala ya kuandika "habari".
2. Ongera, Hongela, ongela badala ya kuandika "hongera".
Meneno yakosewayo yapo mengi, sehemu za kuweka R wanaweka L na kinyume chake, lakini pia sehemu za kuweka H hawaweki na kadhalika.
"Haina shida" msomi mzima utakuta ameandika "aina shida".
"Weka namba", utakuta imeandikwa "eka namba"
Hivi ni kweli walimu hawakufundisha kuandika vizuri?
Tatizo ni nini?
JF siku hizi nyuzi nyingi zina kero za uandishi wa namna hiyo. Vijana mnakwama wapi? Hata lugha yetu wenyewe?