Kero za kuondoa ili CCM ishinde kiulani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero za kuondoa ili CCM ishinde kiulani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwalimu Jr., Mar 3, 2010.

 1. m

  mwalimu Jr. Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CHAMA CHA JIHADI?

  ETI ni kweli kwamba CCJ ni chama cha Jihadi na kwamba waathirika wengi wa mauaji Mwembechai na Zanzibar wamejiunga na chama hicho?  Mambo ....ambayo CCM lazima ijirekebishe:
  1. Kuiba fedha za umma kwa ujanja wa kuamuru idara/wizara kununua kitu fulani ili chama hicho kipate kuiba kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya uchaguzi kila panapokuwa na uchaguzi mbele yake,
  2. Kuachia watendaji wa ngazi za chini kuendesha nchi kutoka Ikulu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Makamu wa rais na wizarani.
  3. Kuwa na makatibu wakuu wanaopendelea makabila, jamaa, ndugu na watoto zao.
  4. Kuinyima mikoa madaraka na uhuru wa kuendesha masuala yao ya kiuchumi na kijamii,
  5. Kutoruhusu redio za FM kutumia lugha za makabila zinakotangaza,
  6. Kushindwa kutatua matatizo ya wananchi na kuacha matatizo hayo kuwa matatizo mwaka ingia, mwaka toka,
  7. Kuachia watendaji wa CCM kula fedha yote inayopatikana katika mitaa na kata na hivyo kushindwa kuifanya miradi ya chama kuwa endelevu,
  8. Kung'ang'ania kuwa na makundi ya kichama badala ya makundi ya kitaifa kama vile yale ya vijana, wanawake, wazazi, wazee na kadhalika,
  9. Kula sahani moja na makampuni ya wachimba dhahabu na kuwahadaa wananchi kuuziwa shea wakati haijulikani hela watapata wapi,
  10. Kutumia fedha za misaada kwa matumizi binafsi badala ya yale yaliyokusudiwa,
  11. Kuwahonga viongozi masikini wa chama miradi ambayo ingestahili kuwa ya kijamii au ya watu wengi zaidi,
  12. Kupendeleana kwa kuchagua watoto wa makada wa chama na hivyo kujenga utawala wa kisultani nchini,
  13. Kuteua kombamwiko kuwa viongozi wa vyuo vikuu nchini badala ya watu wenye kujali maslahi ya wakufunzi na wanafunzi vyuoni,
  14. Kuifanya mikoa kama vile ni wizara badala ya maeneo yanayostahili kujitawala na kujiongoza yenyewe ili yawe na kiwango cha juu zaidi cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii,
  15. Baadhi ya viongozi kujitajirisha kwa kuwatumia wafanyabiashara na maofisa serikali fulani fulani nchini,
  16. Kushindwa kuja na mikakati inayofanya kazi ya kufanya shughuli za uzalishaji mali kama kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi kuwa na manufaa makubwa zaidi kwa Mtanzania,
  17. Kung'ang'anioa ATC kuwa na ndege za abiria badala ya mizigo ambazo zingelikuwa na tija na pato zaidi,

  18. Kulea mashirika bomu kama TRC, Tanzania Postal Service, TTCL, TANESCO na mengine kama hayo,
  19. Kushindwa kuwahamasisha wananchi katika vikundi vya watu 10 au zaidi ili watu hao waanzishe biashara na makampuni kama tulivyofanya wakati wa kutaifisha na kuwa na mashirika ya umma,
  20. Kushindwa kunyanyua viwango vya shule, vyuo na mahospitali ili viwe vya kimataifa na khivyo kuingiza pato la kigeni na hivyo kuisaidia nchi kuheshimika katika nyanja mbalimbali kuliko ilivyo sasa,
  21. Kushindwa kugawa na kugawa upya pato la taifa kwa namna ambayo walalahoi hatimaye wanajinasua na umasikini, njaa na maradhi.
  22. Kushindwa kuondoa kodi na ushuru katika maeneo mbalimbali ambayo yangelichangia si haba katika kuimarisha uchumi wa mlalahoi,
  23. Kushindwa kuifanya biashara ya machinga, mafundi na mama ntilie kuwa biashara halali inayofanyika kiustarabu na katika mazingira yanayokubalika kijamii na kitaifa,
  24. Kushindwa kutumia redio, televisheni na magazeti ya umma kujenga muafaka wa Kitaifa Tanzania,
  25. Kushindwa kuzifanya balozi zetu za nje kuwa balozi zenye kumsaidia Mtanzania awapo nje kufanikisha malengo yake ya kibiashara, kitaaluma, kiuchumi, kitiba na afya na kadhalika,
  26. Kushindwa kuwa na mkakati wa kuhakikisha kila nyumba nchini inapata umeme wakati nchi zilizokuwa vitani hivi majuzi kama Sierra Leone zimefanikiwa katika hilo,
  27. Kushindwa kuweka mkakati wa kumpatia kila mwanafunzi wa shule ya msingi Kompyuta wakati nchi kama Uruguay, Paraguay, Argentina na Brazil zimeweza au zinawezeshwa kufanya hivyo,
  28. Kushindwa kufanya baadhi ya mashirika muhimu ya umma kuwajibika na kufanya biashara kwa faida kama China, Vietnam na Russia zilivyofanikiwa kufanya,
  29. Kushindwa kuwa na mkakati wa kuipatia kila nyumba maji wakati tumezungukwa na maziwa, mito na maji yaliyo chini ya ardhi,
  30. Kushindwa kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kutumia gesi badala ya ukataji miti hovyo kitu kinachochangia kuharibika kwa mazingira,
  31. Kuruhusu fedha nyingi za Miradi ya Ukimwi kuliwa na maofisa mradi badala ya waathirika wa ukimwi,
  32. Kushindwa kuwa na viwanja vya michezo na bustani za burudani katika kila shule, mtaa na kata wakati nchi ina uwezo wa kufanya hivyo,
  33. Kuishindwa kuwa na mradi wa kuagiza na kununua mitambo ya rejeleza taka ili miji yetu iondokane na uchafu na magonjwa yanayosababishwa na uchafu,
  34. Kushindwa kuwa na nyumba bora za walimu kwa kila shule nchi nzima kwa kutumia nguvu za ziada za majeshi yetu yakiwemo ya ulinzi, JKT na polisi shirikishi,
  35. Kushindwa kuyatumia maji ya Ziwa Victoria, Nyasa, Tanganyika, Rukwa kuongeza uzalishaji mali na ubora wa maisha wa wazawa,
  36. Kushindwa kutumia majeshi yetu na wahandishi kujenga viwanda vya msingi, yaani, viwanda ambavyo ni lazima tuwe navyo ili tuepuke kutegemea nchi zingine kwa vitu kama balbu, pasi, sindano, pampu za maji, soketi, swichi, friji, eyakondishna, redio, tv, kompyuta na vitu vya kijinga kama hivyo,
  37. Kushindwa kutumia nguvu kazi tuliyonayo, mali asili yetu, akili zetu na utaalamu wetu kuhakikisha nchi nzima ina nyumba bora, barabara safi na huduma za uhakika katika kila eneo,
  38. Kushindwa kuweka mikakati ya vijana kujiajiri wenyewe kupitia michezo, burudani, sanaa, sinema na vitu kama hivyo,
  39. Kushindwa kutumia bahari, madini, mazao misitu yetu, ndege wetu, wanyama wetu, maziwa yetu, vijiji vyetu na vyote kama hivyo kuifanya biashara ya utalii imjaze zaidi mwanakijiji kuliko ilivyo hivi sasa.
  40. Kushinndwa kufanya hospitali zetu ziingize fedha nyingi za nje kuwatibu wagonjwa toka nje na hivyo wa kwetu kutibiwa bure,
  41. Kushindwa kuilinda mifuko ya uzeeni ikiwemo PPF, NSSF, LAPF na bima za afya za kila aina na hivyo kuachia taasisi hizo kuwekeza hovyo kiasi ambacho upo uwezekano mkubwa wa mashirika hayo kushindwa kuwalipa wastaafu wake baada ya miaka michache,
  42. Kushindwa kuhakikisha kuwa bidhaa za wananchi vijijini zinapata uchukuzi mrahisi bila matatizo na kuuzwa pale panapopatikana fedha na faida kubwa zaidi kuliko ilivyo hivi sasa,
  43. Kuziachia redio na televisheni kupumbaza wananchi badala ya kwaeleimisha zaidi ili kuongeza kasi ya maendeleoya kiuchumi na kijamii,
  44. Kuruhusu viongozi wasio na uwezo wa kuleta maisha ya wananchi kuendelea kuwa viongozi,
  45. Kushindwa kuweka mikakati ya Tanzania kupambana kiteknolojia, kielimu, kimichezo, kilugha, kiutamaduni, kijasiriamali
  \}}}}}}}}}}}}}}}+ na kisanyansi na majirani zake kama vile Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi ili nchi hii iwe namba moja na sio siku zote wa pili, tatu au wa mwisho kwa kila jambo.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sasa list yoote hiyo ya nini mkulu? Hata kaa ni embe wadudu wote hao litalika tena?

  Kama ingekuwa ni kwenye typing solution ni kui-highlight tu neno CCM na ku-press 'delete'.

  Kwisha habari yake.
   
 3. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Unataka tujadili kuhusu CCJ au kero ulizo ziorodhesha!?

  Na kama ungepanga malalamiko kwa mpangilio yangevutia sana watu kusoma, ila nimelipenda lalamiko lako la 36, na nimechukizwa na lalamiko la 5. halijakaa vizuri hata kidogo! Kwahilo sikuungi mkono!
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kazi sana kwa CCM kuondoa vitu hivyo maana kuna watu wanapata ulaji juu ya mambo haya na ndio mambo ya msingi leo Tanzania na kwanini tupo hapa tulipo kama ndio hivyo
   
 5. m

  mnyakyusa JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 248
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dah hii imetulia....ikifanya hivi basi bongo kama Ulaya ya Afrca
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Die CCM, Die CCM, your burial ceremony will be a one to remember happier day!
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Yaani umekaa na wenzako mkaorodhesha mambo kibaao huku lengo lenu ni kuichafua CCJ tulishasema UWT wa bongo hamuna kitu hawajui kufichama.
   
 8. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa nini CCJ inawatia homa watu?
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  That is a good question jana kulikuwa na vyama viwili vilivyopata usajili wa muda CCJ na NDM sijaona watu wakihoji hata MKiti na katibu wa hicho chama kingine why CCJ only!
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Halafu unaenda kwenye recycle bin na ku-empty kabisa.
   
Loading...