Kero za Bajaji kwenye Highway Mbeya Mjini

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Igweee!

Karibu mbeya, sehemu ambapo kuna watuajasiri wenye nguvu na wachapa kazi, mji huu ni mzuri kuishi na kufanyia kazi kwa sababu gharama za maisha hapa ni wastani ukilinganisha na Dar na arusha.

Kwa wale wenye magari, hasa wanaopita ama wakaao hapa mbeya watakubaliana nami kuwa wanapata sana changamoto za barabarani waendeshapo magari yao kutokana UTITIRI WA BAJAJI ZISIZOFUATA SHERIA ZA BARABARANI.

Utitiri huu, unakufanya uwe makini sana barabarani otherwise unaweza sababisha ajali, au kuumiza gari yako kwa sababu hawa watu wa huku hasa wendeshao bajaji hujiamini sana kutokana na bajaji zao kuwa ni za chuma hivyo wakikutana na harrier, IST, hizi gari zenye bord laini lazima wakulize ile hatari.

Kusema kweli wamekuwa kero, tunatambua kuwa nao wanatafuta pesa za kulisha familia ama na kwao hiyo ni ajira yao pia lakini wawapo barabarani hujiona wao ndo magari nasi wenye magari ni bajaji.

CHA KUSHANGAZA zaidi ni kuwa wana wa mbeya wanasema bajaji hizo ni za mapolisi, wanajeshi na wafanyakazi wa serikalini kwa asilimia kubwa ndiyo maana zinafanya vile zitakavyo barabarani hasa kuvunja sheria, kama ni kweli kwenye hili INASIKITISHA SANA.


MAMLAKA za usalama barabarani zimekaa kimya hazisemi chochote.

DALADALA zilijaribu kuwagomea lakini wapi?!! hakuna HATUA zozote zilizochukuliwa.Imebidi daladala zikae kimya tu.

Kwa kweli karibu MBEYA ukifika tu kuanzia Uyole utakutana na hizi changamoto mwishowe uichukie mbeya.


TUNAOMBA MAMLAKA HUSIKA ZILIANGALIE HILI SWALA KWAMBA:
✓Kila mwenye bajaji awe na LESENI
✓Na wao wasimamishwe pindi wafanyapo makosa kama wenye magarina waandikiwe kama wenye magari.
✓Mamlaka ziweke utaratibu wa bajaji kama kuwapangia route za ndani kutokea barabarani na hata wakipita barabarani wapite service road kuepuka foleni n.k n.k
View attachment 1569819View attachment 1569820
 
Kweli yaani zimechukua nafasi ya dala dala,sana sana barabara ya mwanjelwa-iyunga,
 
Back
Top Bottom