Mbeya jiji na kero ya bajaji barabara kuu

Mbeya jiji na kero ya bajaji barabara kuu

Popo-

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2022
Posts
281
Reaction score
580
Habari ya Asubuhi wana jamii,

Leo Mh. Waziri mkuu anatarajia kufanya ziara mbeya mjini/mbeya city. Moja kati ya kero kubwa hapa mbeya mjini ni bajaji ambazo hazina utaratibu maalumu kama vyombo vingine vya moto.

Hii imekuwa kero kubwa sana hapa mjini tofauti kabisa na majiji mengine, utaona utaratibu wa bajaji zipite njia ipi, na kwa utaratibu fulani.

Hapa Mbeya hakuna utaratibu wowote, bajaji zinaamua zipite kwa namna zinavyojisikia, na wakati mwingine, traffic wanapewa fimbo eti kuzicontrol bajaji zipite njia gani. Hii kwa kweli si haki kwao traffic na inatengeneza uadui na vijana waendeshao bajaji. Zaidi sana vijana hawa wamekuwa wababe sana barabarani, mpaka kupelekea ajali za mara kwa mara, tumeshuhudia mtelemko wa simike ajali kadha wa kadha waanga wa ajali hizo sana sana ni bajaji kutokana na ukaidi pindi wanapopewa tahadhari. Lakini kwenye mataa ya mafiati baajaji hazifuati utaratibu wowote wa mataa, wao mda wowote wanapita kwenye mataa.

Ni wazi kwamba, bajaji hizi haziguswi kwasababu zinasadikika ni za kiongozi mmoja wa mhimili mkubwa wa nchi hii. Na zingine baadhi ni za polisi na watumishi sekta fulani. (Minong'ono ya mtihani). Tetesi hizi zimekuja baada ya kuona hakuna hatua zozote zinachukuliwa kwenye bajaji hizi, zaidi ya kuwapanga traffic mida ya jioni kuwashukia fimbo bajaji wapite pembezoni mwa barabara, of which zoezi hilo limekuwa gumu na la mateso kwa traffic hao.

Jambo jingine ni BARABARA. tunashuhudia wenyewe barabara kuu iendayo zambia kweli ni nyembamba sana, hivyo kuleta foleni kubwa zamani ilikuwa jioni, sasa ni toka asubuhi kuna foleni, mojawapo ni bajaji, ambao hupita njia moja na magari, huku wakipakia abiria katikati ya barabara of which pia imekuwa ikitengeneza foleni sana ya magari makubwa na madogo.

Jambo lingine, ni uwepo wa mikokoteni barabarani, hii imekuwa kero nyingine. Kuna service road pembeni. Lakini baadhi ya watu wanapita katikati barabara, bila wasiwasi na hata mamlaka zipo kimya..Hili laweza kuleta madhara makubwa ya ajali n.k.

Jambo lingine, ni service road kuwekwa udongo, bila ya ukarabati, hivyo kupelekea shida ya matope na kutwama maji.

Wadau, na wakazi pamoja na watu wote wenye mapenzi mema na mkoa huu. Tusaidiane kufikisha hizi kero. Kwani Mbeya kuitwa jiji hakuendani na hadhi ya ujiji kwa haya yanayoendelea.

Sote kwa pamoja katika maenedeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.


Ndimi,
Asumwisye Amenye Mwaipopo
 
Kwenye hizo bajaji unajua sa Mkurugenzi ni ngapi??? Tuliaa anazo ngapi??? Sugu jee[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kupanda Bajaji kuanzia Mafiat mpaka Mbalizi ni hatari sana. Maroli sio ya kukaa nayo karibu kwenye miteremko mikali ya Simike,Iwambi
 
Kupanda Bajaji kuanzia Mafiat mpaka Mbalizi ni hatari sana. Maroli sio ya kukaa nayo karibu kwenye miteremko mikali ya Simike,Iwambi
Ni hatari sana, Lakini ni kama serikali haioni haya mambo. Sijui kwanini?!
 
Halafu ni mji pekee nimeona bajaj ina utingo/konda...😀
 
Wanasiasa wakiingia kwenye biashara lazima waiharibu.

Miji yote bajaji na bodaboda zimekuwa kero mjini Iringa, Nzega, Mwanza, Dar es Salaam n.k nako ni changamoto wafadhili wa CCM wenye biashara ya kuagiza bajaju na bodaboda wanajali matumbo yao bila kukaa chini kuona ni barabara zipi tu za ndanindani zitumie usafiri huo na kwa uratibu wa karibu kujua idadi muafaka ya vyombo hivyo badala ya kufungulia idadi kubwa bila mpangilio.
 
Kuna Kitu wamefanya Makambako naona kama Bajaj zimetengenezewa lane zake nje ya highway
 
Back
Top Bottom