Kero ya wanachuo kwenye vyombo vya usafiri

moghasa

JF-Expert Member
May 7, 2013
1,084
1,253
Wanajf Igweeeee!

Nipo ndani ya basi la ABC linalofanya safari zake kutoka Singida to Dar!
kero kubwa ninayokumbana nayo ni hii;

Kuna wanachuo sijajua ni chuo gani hapa Singida, ingawa najua ni hivi vyuo vya kozi mbalimbali (Singida hakuna university) wanakasheshe ndani ya basi kama wanafunzi wa kidato cha tatu B walioshida mechi kwenye kombe lao la MBUZI.

Watoto wanajisahau sana, unawezahisi kuwa basi limekodiwa, maisha ya kuigiza mpaka wamenifanya nimkumbuke Dr. Wangu enzi za chuo Bw Kadilikansimba, aliyependa kusema " The world out there (from university) is very complex "Ngoja wamalize chuo, kwa usawa huu wa Anko watakosa hata nguvu za kupiga kelele.

Ukikutana na mmoja wapo mwezi mmoja baada ya chuo unaweza kumfananisha na Yohane Mbatizaji kwa jinsi ilivyokuwa mpole.

Time will tell, we wait.
 
Back
Top Bottom