Kero ya mgambo mijini je wanajenga taswira ipi kwa wananchi?

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Kimekuwa ni kilio kila uchao kutoka kwa wananchi wajasilia mali dhidi ya mateso na manyanyaso kutoka kwa mgambo.

Taifa letu kwa takribani miaka 5 sasa hakuna ajira rasmi ya uhakika ambapo kama ingekuwepo ingepunguza idadi ya vijana wasiyo na ajira rasmi.

Kwa kutambua hilo vijana wamebuni njia za kujiajiri ili angalau kujipatia milo miwili kwa siku ,hata kwa kuuza karanga,mahindi mabichi, kuuza madafu, kuuza mitumba,kuuza viungo vya chakula nk.

Lkn wamekuwa wakikutana na hawa watu mgambo wa mijini na kuwapora bidhaa zao au kuwapeleka kuwashitaki na kadhia nyingi tu na mwisho wao wanapoteza kila kitu kama sehemu ya mtaji wao.

Hadi sasa bado hili tatizo ni endelevu hawa mgambo hawasikii kabisa ,je wanatoa picha gani kwa wananchi wa kawaida juu ya serikali yao ambayo inajiita ya wanyonge?

Screenshot_20210123-165632.jpg
 
Back
Top Bottom