Kero ya foleni: Barabara ya Bagamoyo Road kuanzia Tegeta Nyuki inasababisha sana foleni

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,533
Serikali tafadhali muimulike hii barabara zipatikane 4 ways kuna kero mnoo ya foleni kuanzia Tegeta Nyuki hadi Bunju.

Kwa mfano shule zikifunguliwa wazazi wanapowapeleka watoto shule za Pwani Bagamoyo inakuwa kerooo.

Pia jioni unaporudi kazini ukifika Tegeta Nyuki tu mpaka ufike kwako Bunju 'B' au Mabwepande unatumia muda mwingi sana.

Askofu Gwajima barabara hii ipo kwenye jimbo lako. Tafadhali iweke kwenye vipaumbele vya kuisemea huko Bungeni tupatiwe barabara 4.

HIYO PICHA HAPO NI BOKO MAGENGENI KWA WAGOGO TUMESTAKI HAPO ZAIDI YA SAA 2 FOLENI HAIENDI KISA BARABARA FINYU WENGINE WAMEPITA PEMBENI LAKINI HAISAIDII. TAFAADHALI IMULIKENI HII BARABARA.

20210109_202031.jpg
 
"Askofu Gwajima barabara hii ipo kwenye jimbo lako. Tafadhali iweke kwenye vipaumbele vya kuisemea huko Bungeni tupatiwe barabara 4."

😂😂😂😂
 
Serikali tafadhali muimulike hii barabara zipatikane 4 ways kuna kero mnoo ya foleni kuanzia Tegeta Nyuki hadi Bunju...
Siku ya Jumanne ndio utakoma. Kuna mnada pale Boko Chama, bidhaa zinapangwa Barabarani. Kuna Mabasi ya Mikoani, Malori ya Mchanga, Mungu tuu uutulinda na anajua tabu tuipatayo. Laiti Utawala wa awamu ya NNE wangekumbuka kuipanua Barabara hii mpaka Mapinga darajani.
 
Mkuu N'yadikwa unaijua njiaa ya chini kupitia kwa Mwamunyange hadi Mbweni? Jaribu hii itakupunguzia shida kidogo
Nimepita hiyo na napita hiyo mkuu hata asubuhi napoenda kazini lakini hiyo pia siku hizi hasa asubuhi ina foleni pia pale Kunduchi wanafunzi wanapovuka na jioni pia...kwa ufupi hiki kipande cha Nyuki hadi Bunju 'B' wakuweka 4 ways itasaidia sana.

Kwa mfano ukitoka Boko hadi hapo njiapanda ya Nyuki foleni kali lakini ukishashika double Lane ya hapo nyuki hadi mwenge unaenda uzuri tu.

Njia ya chini ina absorb foleni lakini kwa kiasi kidogo kuliko ingetanuliwa hii waliyoishia Nyuki
 
Mgombea wa Chama kimoja cha siasa alisema maendeleo ya vitu sio kipaumbele chake....barabara na flyover za nini sasa!
 
Serikali tafadhali muimulike hii barabara zipatikane 4 ways kuna kero mnoo ya foleni kuanzia Tegeta Nyuki hadi Bunju..
Pole Sana Mkuu naona foleni imekudatisha Mpaka barabara umeiita road na road ukaiita barabara.Kwani lazima Uishii huko Mkuu, hamia Kimara, Mbezi, Kibamba, Kiluvya au kibaha.Mfano si tunaoishi kibaha tunatoka asubuhi hom na magari tunakuja yapaki hapa Kimara Mwisho,

alaf tunadaka Mwendokas kuingia Mjini, jioni tunarudi tunapanda magari yetu tunaenda kibaha, na huku kumebarikiwa Sana Mh.ametuwekea barabara 12 pana yaani hapa na kama 4 tu zinatika saiz ila hakuna foleni.Sasa nyie bakini hukohuko ambako Wachaga wote wameenda kujilundika wakidai ni njiapanda ya kwenda Moshi 😁.

Hata Mimi ningekuwa Mbunye wako ningekujibu kuwa serikali inatekelezairadi kwa utaratibu na kwa mipango sio kafoleni kametokea huko ndio tujadili bungeni eti haraka tuweke njia pana. Hameni huko kwani lazima kuishi huko, ?
 
Back
Top Bottom