KwetuKwanza
Senior Member
- Mar 13, 2023
- 121
- 218
Machi 23, 2022 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na unaofadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Kilijengwa choo cha kisasa katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Mkoa wa Shinyanga (Ibinzamata), mradi ambao uligharimu takribani Shilingi Milioni 160.
Mradi huo kwa wakati huo ulizinduliwa na Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Bonipace Chambi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo wakati huo, Jasinta Mboneko.
Wakati wa uzinduzi wa choo hicho, viongozi wa Serikali walisisitiza choo kutumika kama ilivyokusudiwa pamoja na kutunzwa ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Manispaa ilitakiwa kutafuta msimamizi wa choo hicho ambaye atahakikisha kinafanya kazi lakini anatoa huduma sahihi kwa watu wote ambao watakitumia ndani ya stendi hiyo.
Ni miaka minne sasa tangu choo hicho kianze kitumika, Manispaa ya Shinyanga imeweka wasimamizi ambao wanatoa huduma kwa wananchi ambao hutumia choo hicho.
Gharama za huduma katika choo hicho ambazo zimewekwa na Halmashauri ni kila Mwananchi anatakiwa kutoa kiasi cha Sh 300 kwa ajili ya kupata huduma ya choo.
Kwa muda wa siku za hivi kuimeibuka kero mpya, ambayo kwa inafanywa na watoa huduma katika choo hicho.
Wasimamizi wa choo hicho wamekuwa na tabia ya kutorudisha chenji kwa mtu anayekwenda kupata huduma ikiwa atatoa pesa inayozidi Sh 300.
Asilimia kubwa ya watu ambao utaka kupata huduma kwenye choo hicho wamekuwa wakitoa Sh 500 huku wakitegemea kurudshiwa chenji Sh 200, lakini watoa huduma huwa hawafanyi hivyo.
Katika uchunguzi ambao nimeufanya kutaka kujua ni kwanini watoa huduma katika choo hicho hawarudishii chenji wateja ambao wanatoa pesa inayozidi Sh 300?
Nikiwa kama abiria ambaye nilikwenda kwa ajili ya kupata huduma, nilikumbana na kero hiyo, ambapo nilitoa kiasi cha Sh 2,000.
Katika pesa hiyo nilitakuwa kurejeshewa Sh 1,700 lakini watoa huduma walinirudishia Sh 1,500, na nilipowataka wanipatie chenji yangu Sh 200 inayobaki walisema hawana.
“Hatuna chenji ya Sh 200, kama unataka chenji basi tukurudishie pesa ili utafute pesa kamili na ndiyo urudi upate huduma,” alisema Mhudumu.
Baada ya hali hiyo niliamua kukaa eneo hilo kuna utolewaji wa huduma kwa siku nzima, ambapo magari yote ambayo yalikuwa yanaingia ndani ya stendi hiyo abiria wake wote walipata huduma kwenye choo hicho.
Jumla ya Magari 50 ambayo yaliingia siku hiyo abiria wake wote walipata huduma, ambapo kila gari lilikuwa na abiria kuanzia 50 hadi 100.
Abiria wote ambao walihitaji huduma kwenye choo hicho, wote walipata changamoto ya kutorejeshewa chenji na watoa huduma katika choo hicho.
Jumanne Elias (siyo jina lake kamili) huyu ni mmoja wa viongozi katika stendi hiyo anasema hiyo tatizo la chenji katika stendi hiyo limekuwa kero kubwa ambapo wamepokea malalamiko mengi kutoka kwa abiria.
Elias anaeleza kuwa watoa huduma hao wamekuwa wakifanya maksudi kutafuta chenji, kwani katika maekelezo ambayo walipewa na uongozi wa manispaa ni kuhakikisha kila wakati wanakuwa na chenji ya Sh 200.
“Hili tatizo kiongozi ni kubwa sana, kama uongozi tumepokea malalamiko mengi sana, lakini hata sisi tumepeleka haya malalamiko kwa Meneja wa Stendi ambaye ni mtumishi wa Manispaa kwa ajili ya kufanyia kazi.”
Anaeleza kuwa tangu wamepeleka malalamiko hayo kwa viongozi wa manispaa hakuna kilichofanyiwa kazi “Inaonekana huyu aliyepewa hii tenda ya kukusanya ushuru wa choo anao watu nyuma wakubwa wananufaika na hizi chenji, maana hakuna hatua imechukuliwa.”
Nilikwenda mbali zaidi kutaka kujua takwimu za watu ambao wanaingia ndani ya stendi hiyo wakiwemo abiria.
Katika uchunguzi huo, nilielezwa na viongozi wa stendi kuwa kwa siku yanaingia magari makubwa na madogo (TATA) ya abiria zaidi ya 300, ambapo kila gari ubeba abiria siyo chini ya 50.
Wahusika wanasema kuwa Stendi hiyo inafanya kazi saa 24, ambapo magari uingia na kutoka kila baada ya dakika 10 mchana na usiku.
Wanasema kuwa katika takwimu za chini takribani watu 15,000 wanaingia katika stendi hiyo kila siku, ambapo asilimia 90 ya watu hao hutumia choo hicho kwa ajili ya kupata huduma.
Katika hesabu za kiwango cha chini kabisa, watoa huduma katika choo hicho wamekuwa wakipata kila siku zaidi ya Sh Milioni tatu (3,000,000) pesa ambazo zinawanufaisha wao kinyume na utaratibu.
Mmoja wa viongozi wa Boda boda ndani ya Stendi hiyo anasema kuwa watoa huduma hao wamekuwa wakinufaika kwa kiwango kikubwa kupitia chenjia ambazo wamekuwa wakibaki nazo.
“Kila gari likija hapa hasa haya makubwa ya safari ndefu, wanawatangazia abiria wao kuchimba dawa ni dakika tano tu, kutokana na muda kuwa mchache akiambiwa hakuna cheji yeye anaacha, anachojali ni kupata huduma tu,”…
“Hapo ndipo wanaponufaika hawa watu, wanajua kabisa hakuna abiria ambaye atakaa muda mrefu kutaka chenji, mtu akiambiwa hakuna Sh 200 moja kwa moja anapata huduma ili aweze kuwahi gari,”
Baadhi ya wajasliamali wanaofanya biashara ndani ya stendi hiyo wanasema kuwa kero ya kutorudishia chenji abiria ambao wamekuwa wakipata huduma katika choo cha stendi hiyo imekuwa kubwa sana.
Elias Jumanne (Siyo jina lake halisi) ni Mjasliamali anasema kuwa abiria wengi wamekuwa wakilalamika juu ya kero hiyo ambayo imeshindwa kutatuliwa na viongozi.
“Hili jambo lina watu wakubwa na ndiyo maana wameshindw kulitatua, ukipiga hesabu ya magaro yeto yanayoingia humu ndani, hiyo chenji ukajumlisha pesa wanayopata ni kubwa sana, na inaingia mifukoni mwao,” ananieleza Jumanne.
Kero kama hiyo siyo tu ipo katika Stendi ya mabasi Shinyanga, kero kama hiyo ipo katika kivuko cha abiria Kisorya katika Wilaya ya Buda Mkoani Mara kuelekea Wilaya ya Ukelewe Mkoani Mwanza.
Katika kivuko cha Kisorya kuelekea Ukelewe Ziwa Victoria ambacho kinasimamiwa na TEMESA, gharama ya kuvuka ni Sh 400 kila mtu mmoja.
Katika kivuko hicho wamekuwa na kero ya kutorudisha chenji ya Sh 100.
Wananchi wa Wilaya hizo wanasema wao wamezoea, ukitoa Sh 500 kwa ajili ya kupata tiketi ili kuvuka upande mmoja kwenda upande wa Pili ni kawaida kutorudishiwa chenji ya Sh 100.
“ Hii changamoto ya kutorudishiwa Chenji hasa Sh 100 ina miaka mingi sana, mwanzoni tulilalamika lakini hakuna hatua zilichukuliwa, tukaamua kunyamaza na tumezoea hivyo”
Kero hiyo imeibua fursa kwa wananchi wa maeneo ya kivuko hicho hasa upande wa Kisorya Bunda, wanawake wajasliamali wamekuwa wakifanya biashara ya kuuza chenji eneo la kukatia tiketi.
Wanawake hao wanauza chenji hiyo, ambapo ukiwapatia Sh 500 wanakupatia Sh 400 gharama ambayo inahitajika kwa ajili ya kupata tiketi ili kuvuka.
Mmoja wa wajasiriamali hao (Jina tunalihifadhi) anasema kuwa waliona ni kama fursa, baada ya kugundua kuwa Sh 100 wamekuwa wakinufaika watumishi ambao wanakatisha tiketi.
“Hili jambo lina muda mrefu sana, ilianza kama kero kwa kipindi kirefu hadi watu wakazoea na sisi tukaona ni fursa, tumekuwa tunauza chenji, ili kupunguza usumbufu wa kukosekana Sh 100,”..
Takwimu ambazo nimepewa zinaonyesha kuwa kivuko hicho kwa siku kinasafirisha abiria zaidi ya 2,000 kwa siku kutoka upande mmoja kwenda katika upande mwingine.
Asilimia 100 ya abiria hao wamekuwa wakiacha hiyo Sh 100 kutokana na wahusika kudai kuwa hawana chenji, jambo ambalo limedumu kwa miaka mingi katika aneo hilo bila ya hatua kuchukuliwa.
Hata hivyo licha ya wananchi kutolalamika kwa sasa kutokana na kuona jambo la kawaida, chenji hizo ambazo ubaki wamekuwa wakijinufaisha watoa huduma kwenye kivuko hicho.