ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,141
- 951
Hili ni eneo la Vingunguti, katikati ya makazi ya watu ambapo barabara hii inayounganisha Barabara ya kutokea Tabata - Segerea na ile ya Mwalimu Nyerere (Kwenye mataa ya vingunguti). Manispaa ya Ilala ilijitahidi kujenga Daraja la Vingunguti (Karibu na Machinjioni) kwenye mto Msimbazi. Hata hivyo,barabara inayopitia darajani hapo japo ililengwa kutatua tatizo la foleni hasa kwa wale watokao maoeno ya Tabata Ubungo Kibangu, Makoka, Kilungule Kimara, nk kwenda Uwanja wa Ndege na maeneo ya UKONGA, Tazara, Mjini, Temeke nk imekuwa ni kero kubwa. Barabara hii haipitiki vizuri hata kakinyesha ka mvua kidogo sana, inatengeneza madibwi makubwa sana ambayo ni kero.
Kwa kiasi fulani, maana ya kuwa na daraja hilo la vingunguti imepotea kabisa. Kuanzia hapo darajani kuelekea upande wa Vingunguti machinjioni mpaka kufikia kiungio cha barabara ya Nyerere, kuna lami lakini kutokea hapo Darajani kuelekea kiungio cha barabara itokayo Segerea (eneo la Baracuda Bar) kuna tope la ajabu sana na madimbwi ya kuweza kuzamisha magari madogo na Bajaj haziwezi kabisa kupita.
Shime watendaji wa Manispaa ya ILALA na Mhe. Mbunge wa Jimbo la UKONGA (MAKONGORO MAHANGA,) Pia huko uone jinsi kodi za wananchi zilivyotumika vibaya kukarabati hiyo barabara..Tunapoelekea masika
barabara itakuwa haipitiki kabisa.