Kero: Vyoo vya Simu 2000 ni vichafu sana

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,261
Reaction score
12,660
Vyoo vya hii stendi jirani na kituo cha Polisi cha Simu 2000 ni vichafu sana.

Unapoingia tu unakutana na masinki yale ya wakati wa COVID-19 ya kunawia mikono yana maji machafu yaliyotuama humo ni kama yamekuwa hapo kama mwaka hivi hadi yameoza.

Ukitoka hapo unalipia lakini ukiingia ndani vyoo ni vichafu sana kama unavyoona.

Hawa wanaopewa hizi kandarasi za kusimamia hivi vyoo Halmashauri huwa mnawakagua?!

Yuko wapi Afisa Afya wa Manispaa/Halmashauri Kinondoni. Hauoni huu uchafu unaohatarisha afya ya jamii?

Mnakera kinoma yaani!!! Hizi huduma tunalipia hamtoi bure eti!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…