Kero: Ukosefu wa daraja la Chanika - Mgeule

Kero: Ukosefu wa daraja la Chanika - Mgeule

FIKRA HAI

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
231
Reaction score
81
UKOSEFU WA DARAJA CHANIKA - MGEULE.
Imani yangu ni Kwamba kero hizi tunazoziweka humu hupata ufumbuzi wake ili kuwatoa watch Kwenye adha hizi.

Ukifika CHANIKA Buyuni kuna Mtaa unaitwa Mgeule, kuna bonde lenye korongo la kupitisha maji nyakati za masika, hali hii hupelekea watch wanaoishi upande wa pili kupata Shida kuvuka, hivyo hulazimika kuvua nguo apite kwenye maji ndipo na avae nakuwahi kazini.

Kwakuwa huduma nyingi za wakazi hao hupatikana upande wa pili, kama vile shale,hospitali, biashara, nk wakazi hao hushindwa kwenda makazini, wanafunzi kutokuhudhuria masomo.

Adha imekuwa ni kero kubwa sana hasa katika kipindi hiki cha mvua.
Kupitia Uzi huu tunaomba kero hii ipatiwe ufumbuzi hata wa muda.
 
Back
Top Bottom