Kwanza niawapongeze TRA kwa kubuni utaratibu mzuri wa kulipia Road Licence ambao kwa kweli umetuondolea usumbufu kwa kurahisisha kazi ya kujiaajili na kulipia kwa kutumia mtandao. Hata hivyo bado kina kero ambayo bado haijatatuliwa wakati wa kuchukua hiyo kadi ya Road Licence ambapo kumekuwa na foleni kubwa sana hivyo kupoteza muda mwingi kabla ya kupata hiyo kadi, hasa ikizingatiwa kuwa hairuhusiwi mtu mwingine akiwemo agent kukuchukulia hiyo kadi.
Ni vizuri TRA wabuni utaratibu mzuri ili kutuondolea usumbufu huu na kutuwezesha kuendelea na kazi zetu za ujenzi wa taifa. Wangeweza kumuuluza kabisa mtu anayelipia licence ni ofisi gani atachukulia hiyo licence ili waiprint kabisa na kumtumia sms baada ya kuiprint ili akaichukue. Wadau tusaidie kupigia kelele jambo hili.