Kero nssf....

Kero nssf....

Kayla

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
256
Reaction score
77
huu mfuko wa NSSF kwa kweli umegeuka na kuwa kero sana,system zao ni mbovu na utendaji wao ni mbovu kwa ujumla..unakwenda kujisajili kwa ajili ya kukatwa makato ya mafao ya kiinua mgongo wakati wa kustaafu lakini process inachukua muda mrefu mpaka inakera,hadi ufanikiwe kupata kadi yako ya uanachama ujue itakugharimu muda mrefu sana...mafao yako nako kwenyewe ni matatizo..mimi binafsi nimejiandikisha tokea mwaka juzi hadi leo hii sijapata kadi,ni jambo linalokera sana..nimefuatilia several times lakini hali ni hiyohiyo..jamani hii kadhia mpaka lini? hii mifuko ni mali ya nani hasa?
 
Hamia PPF au LAPF sheria iko wazi una uhuru wa kuchagua mfuko uutakao!!
 
Hamia PPF au LAPF sheria iko wazi una uhuru wa kuchagua mfuko uutakao!!
Hivi ni kweli na kama ni kweli ninaweza kuamisha account yangu kutoka nssf kwenda ppf,maana mimi mwenyewe naichukia nssf,hivi kweli watu wanachukua pesa za watu na kukaa nazo zaidi ya miaka kumi bila intrest
 
Sina hamu na hao jamaa NSSF! Nimefungua madai January 2011 na nimepata stahiki yangu April 2011. Kutokana na utaratibu waliouanzisha wa kutakiwa uwe na kadi mpya ya uanachama ndo usumbufu umezidi kiwango. Nilipiga picha za kadi mpya May 2010 pale ofisi zao Ilala (Dar) nimepata kitambulisho kipya January 2011 na kufungua madai pale ktk ofisi zao Ubungo (Dar). Mazingira ya kutaka rushwa yanachangia kwa kiasi kikubwa. Nimeyaona bila aibu. Mashirika ya hifadhi za jamii ni janga ktk TZ yetu. Wafanyakazi hawana Mjomba!
 
wanatanzania tunalala sana...mi mwenyewe nishaenda pale mpaka sasa nimeamua kuacha, siku nikijiskia nitaenda kuangalia, yani wale wafanyakazi hata sielewi huwa wanafanya nini, mambo mengine yanasikitisha kweli ni kwa sababu tuna ile tabia ya upole ambayo sijui itaisha lini! ingekua wenzetu ambao hawana tabia kama hii, watu wangeisha kwenda pale na viboko, fimbo mtindo mmoja ofc nzima
 
hairuhusiwi kuwasema vibaya NSSF......
 
Back
Top Bottom