Kero: Meli ya MV Victoria imejaa kunguni, mamlaka hazichukui hatua pamoja na kujulishwa

lutajangurwa

Senior Member
Sep 21, 2019
126
172
Mv Victoria ni usafiri unaopendwa sana kati ya Bukoba na Mwanza. Cha kushangaza, matunzo na usafi ni hovyo.

Meli imejaa kunguni walioshiba vilivyo. Abiria wanaumia lakini hawana choice. Upande hatari ni G Main Deck Daraja la tatu. Kunguni wana jeuri mpaka wanatembea kwenye marumaru ya sakafuni. Ni hatari.

Abiria wazoefu wanasema hili tatizo ni la muda mrefu. Wameandika sanduku la maoni, lakini wapi! Nimeamua kupitia jukwaa hili, ili tatizo liwe public. Tusaidieni tunaumia. Hivi si mwajiri mtu mmoja wa fumigation apite anapulizia kila meli inapokuwa inafanyiewa usafi wa kila siku? Au mpaka tenda?

Upande wa 1F Upper Deck nako si shwari. Taa zimekwanyuka (Restaurant) na zingine kama zimebomolewa na mkono. Hivi kweli, uongozi wa MV Victoria mko serious.

Naisifu sana timu ya huko Restaurant, wanafanya vizuri. Hasa jamaa wa burudani
View attachment 2375437View attachment 2375438
 

Attachments

  • 20221003_051909.jpg
    20221003_051909.jpg
    52.2 KB · Views: 16
  • 20221003_065149.jpg
    20221003_065149.jpg
    83.7 KB · Views: 16
  • 20221003_051750.jpg
    20221003_051750.jpg
    62.5 KB · Views: 16
Back
Top Bottom