Waziri Mkuu Majaliwa amezindua safari ya meli ya MV Mbeya II itakayotoa huduma katika Ziwa Nyasa nchini na nchi jirani za Msumbuji na Malawi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,035
2,000

PMO_3713.JPG
Meli ya MV. Mbeya II ambayo imezinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 5, 2021.i 20.1 ambazo zimetumika katika kujenga meli tatu ambazo kati yake mbili ni za mizigo MV Ruvuma na MV Njombe kwa thamani ya shilingi bilioni 11 na meli ya abiria na mizigo ya MV Mbeya ii kwa shilingi bilioni 9.1.

Meli ya MV Mbeya ii inauwezo wa kubeba abiria 300 na tani 200 za mizigo.

Ni MV Mbeya ll yenye uwezo wa kubeba abiria 300 na tani 200 za mizigo.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua rasmi safari ya meli mpya ya MV Mbeya II itakayotoa huduma katika Ziwa Nyasa nchini na nchi jirani za Msumbuji na Malawi.

Meli hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni 9.1 ni muendelezo wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria kwa lengo la kuboresha uchumi.

Amezindua safari za Meli hiyo leo (Jumanne, Januari 5, 2020) katika Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa. Amewataka wananchi waitunze meli hiyo ambayo imejengwa na kampuni ya Kitanzania ya Songoro Mrine.

Waziri Mkuu amesema Tanzania imezungukwa na nchi nane ambazo zinategemea kupata bidhaa mbalimbali kutoka nchini. “Wananchi tumieni fursa ya uwepo wa meli hii kufanya biashara.”

Amesema wananchi hawawezi kupata maendeleo bila ya Serikali kujenga miundombinu kama ya meli, barabara, bandari, hivyo amewataka waitumie vizuri kwa ajili ya kukuza uchumi wao.

“Serikali inajenga vitu kwa maendeleo ya watu na kwa kuzingatia hilo, Serikali imewekeza fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu itakayowanufaisha kiuchumi kama meli.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameagiza kuwe na kanzidata ya mafundi chipukizi wa Kitanzania wanaoshiriki katika ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati kama meli na madaraja makubwa.

Waziri Mkuu amesema kanzidata hiyo itaiwezesha mafundi hao chipukizi kutambuliwa kwa lengo la kuwaendeleza zaidi na kuwa na ujuzi ili baadaye wapewe miradi ya ujenzi.

Pia, Waziri Mkuu alikagua hali ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mbinga-Mbambabay yenye urefu wa kilomita 66 ambayo ujenzi wake umekamili. Amesema ameridhishwa na ujenzi wake.

“Nimekuja na barabara hii nateleza tu, wakati ule ulikuwa unatembea katika mawe, makorongo lakini sasa unalala tu. Naipongeza kampuni ya CHICO kwa ujenzi wa mradi huu.”

Naye, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema ujenzi wa barabara hiyo ni kutimiza ndoto za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuboresha miundombinu.

Amesema kukamilika kwa barabara hiyo pamoja na kuanza kwa safari ya meli ni ukombozi wa kiuchumi kwa wananchi wa wilaya ya Nyasa na ukanda mzima wa kusini. “Sasa Nyasa imefunguka.”

Mhandisi Kasekenya amesema Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi itahakikisha inasimamia kikamilifu bandari katika kukusanya mapato yake kwa njia ya kielektroniki ili ziweze kujiendesha na kwamba haitamvumilia mtendaji yeyote atakayekwenda tofauti.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alinanuswe Lazeck amesema ujenzi barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa kilomita 66 umegharimu shilingi bilioni 129.361.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Deusdedit Kakoko alisema katika ziwa nyasa kuna jumla ya bandari 15 kati yake sita zipo mkoani Ruvuma, sita zipo mkoani Njombe na tatu zipo mkoani Mbeya.

Alisema katika kuboresha usafiri katika Ziwa Nyasa Serikali ilitoa shilingi bilioni 20.1 ambazo zimetumika katika kujenga meli tatu ambazo kati yake mbili ni za mizigo MV Ruvuma na MV Njombe kwa thamani ya shilingi bilioni 11 na meli ya abiria na mizigo ya MV Mbeya ii kwa shilingi bilioni 9.1. Meli ya MV Mbeya ii inauwezo wa kubeba abiria 300 na tani 200 za mizigo.

PMO_3604.JPG
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Meli ya MV. Mbeya II kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021.

Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,Deusdedit Kakoko, Mbunge wa Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya,Mwenyekiti wa Bodi ya MNamlaka ya Bandari Tanzania, Ignas Rubaratuka na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho.

PMO_3620.JPG

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Abdullah Mwingamno kuhusu uendeshaji wa Meli ya MV. Mbeya II wakati alipozindua Meli hiyo kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021.

PMO_3640.JPG

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitumia kionambali wakati alipozindua Meli ya Mv. Mbeya II kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021. Wa pili kushoto ni Mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme

PMO_3662.JPG

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kupiga king’ora kuashiria uzinduzi wa Meli ya MV. Mbeya II kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021.

PMO_3696.JPG
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzindua Meli ya JMV. Mbeya II kwenye bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021. Kulkia kwake ni Mkewe Mary.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,850
2,000
Sawa ngoja waje,kwanza wanatafuta kasoro ama changamoto kisha watakuja na options za lawama na sio pongezi kwenye ilo.
Mnataka pongezi za nini kwani hizo pesa za ujenzi mmetoa mifukoni kwenu?

Basi acheni kukusanya kodi na kuomba omba misaada nje halafu mkitengeneza tutawapongeza.
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,576
2,000
Mnataka pongezi za nini kwani hizo pesa za ujenzi mmetoa mifukoni kwenu?

Basi acheni kukusanya kodi na kuomba omba misaada nje halafu mkitengeneza tutawapongeza.
Kwa hiyo hata weweuliyetoa pesa za kodi huwezi kupongeza zilivyotumika vizuri?
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,850
2,000
Kwa hiyo hata weweuliyetoa pesa za kodi huwezi kupongeza zilivyotumika vizuri?
Simpongezi mtu kwa kutimiza wajibu wake, hiyo ni dhambi; kama hawawezi kuyafanya hayo wangeacha kutumia kura feki wakapumzike kwa amani.
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,436
2,000
Mnataka pongezi za nini kwani hizo pesa za ujenzi mmetoa mifukoni kwenu?

Basi acheni kukusanya kodi na kuomba omba misaada nje halafu mkitengeneza tutawapongeza.
Kinachowashangaza watu ni pale haya mambo yanapokuwa kama kununua nguo ya ndani, kwani kila pahala Miradi ipo na inakamilika, haya mambo watu wanajiuliza Kwa nini Leo na si kipindi cha upinzani mkubwa Sana enzi za kina kikwete??

Enzi hizo upinzani ulikuwa Moto Moto, kina Zitto, kina Mbowe, kina Lissu, kina Mdee, kina Kafulila na wenginewe waliokuwa hodari kupanga hoja na kupangua, Licha ya kuuliza na kupigia kelele Sana utumbuaji pesa Wakati huo, lakini Bado mabwawa ya uzalishaji umeme yalikuwa yakikauka, selikari kuwa na mikataba ya hovyo, serikali kukopa pesa Kwa ajiri ya kulipa wafanyakazi katibu kila mwezi

Sasa leo, Miradi inatekerezwa Kwa kasi, na Bado kuna wanafunzi Kusoma bule na wafanyakazi wanalipwa tena Kwa Wakati na mambo makubwa

Hicho ndicho kinachofanya watu waandike humu hayo maajabu na ndo mlikuwa mkiyapigia kelele ninyi wapinzani uchwara Mbele ya serikali imara!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom