Kero: Matangazo wakati unapopiga simu

Full 8

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
313
271
Inakera sana pale unapopiga simu kwa mtu hasa wa mtadao wa Tigo na Airtel badala ya simu kuita au kuambiwa haipatikani, kumekuwa na tabia ya kuweka matangazo mengi na marefu ambayo hayana umuhimu.
Hali hii huendelea na kuja kuambiwa kuwa namba haipatikani au inatumika baada ya sekunde nyingi sana kupita.
Hali hiyo:-
*Hutupotezea muda
*kumaliza chaji kwa simu
*kero kwani naweza kuwa si mtumiaji wa mtandao huo na wala sina mpango.

Mwisho.
Nawaomba Tigo na Airtel mbadilike, mnani(tu)kwaza sana.
 
Inakera kulikopitiliza. Mbaya zaidi Matangazo gayo wanatuandalia sisi wa Mitandao mingine ambayo kiitifaki haituhusu.

Shenzi kabisa. Ni kero kubwa sana.
 
Unapopiga simu kama namba inapatikana husikii matangazo bali namba ikiita, ukiona unaanza kusikia matangazo jua simu haipatikani hapo maana mwishoni watakuambaia haipatikani, so ku save muda kata upige tena baadae
 
hasa tigo yaani wanakera sana...hivi matangazo mbona wanafanya mengi sana kwenye vyombo vya habari, mabango n.k hawatosheki tu
 
Jamani hawa jamaa hawana uzi wao humu tuwabwatukie. Mi kuna wakati natamani hata niwatukane matusi mabaya ila iman yangu tu inanikanya. Afu hata kuna wakati ukipiga huduma kwa wateja hasa tigo wanatabia ya kuweka mziki background kitu ambacho ni kero sana kwa kweli
 
Unapopiga simu kama namba inapatikana husikii matangazo bali namba ikiita, ukiona unaanza kusikia matangazo jua simu haipatikani hapo maana mwishoni watakuambaia haipatikani, so ku save muda kata upige tena baadae
Kuna wakati mhusika anakuwa anaongea na simu nyingine, lakini hawakwambii hadi matangazo yao yaishe
 
Tigo tena wananiudhi mbaya ukianza tu kupiga wao wanaanza JAZA UJAZWE...nalichukia hilo tangazo balaa
 
Back
Top Bottom