Kero kwa waajiri na ma hr.

mamabaraka

Member
Oct 18, 2011
92
14
wana jf wenzangu nakerwa na tabia ya baadhi ya waajiri wanaopiga simu. Unakuta ni mishare ya saa nne na nusu asubuhi unapigiwa cm kama hii. Nanukuu "haloo naongea na flani?napiga simu kutoka ....... Njoo leo saa tano na nusu asubuhi ofisi kwetu kinondoni kwa ajiri ya usaili fika na vyeti original tafadhari" Hii taarifa ni nzuri lakini kwa nini usinipigie siku tatu au nne kabla. Inaudhi manake huu uzembe umenifanya nikose interview mbili na huwezi jua yawezeka ndo ilikuwa nafasi yangu ya kazi. Unapigiwa simu ya hivyo saa nyingine umesafiri hauko Dar, au upo Dar lakini vyeti umeacha nyumbani na uko mbali huwezi kuvifata na ukawahi kwa muda uliopewa. Jamani kama inawezekana naomba hili lilekebishwe.
 
akufukuzae hakuambii toka na anaekunyima kitu lazima vikwazo kibaoo pole sana mama baraka..
 
[QUOTE) akufukuzae hakuambii toka na anaekunyima kitu lazima vikwazo kibaoo pole sana mama baraka.. ASANTE LAKINI INAKERA JAMANI HUU SIO UUNGWANA WAJIREKEBISHE BASI AU BORA WASIPIGE SIMU KABISA.
 
wana jf wenzangu nakerwa na tabia ya baadhi ya waajiri wanaopiga simu. Unakuta ni mishare ya saa nne na nusu asubuhi unapigiwa cm kama hii. Nanukuu "haloo naongea na flani?napiga simu kutoka ....... Njoo leo saa tano na nusu asubuhi ofisi kwetu kinondoni kwa ajiri ya usaili fika na vyeti original tafadhari" Hii taarifa ni nzuri lakini kwa nini usinipigie siku tatu au nne kabla. Inaudhi manake huu uzembe umenifanya nikose interview mbili na huwezi jua yawezeka ndo ilikuwa nafasi yangu ya kazi. Unapigiwa simu ya hivyo saa nyingine umesafiri hauko Dar, au upo Dar lakini vyeti umeacha nyumbani na uko mbali huwezi kuvifata na ukawahi kwa muda uliopewa. Jamani kama inawezekana naomba hili lilekebishwe.
pole sana mama baraka lkn ndo hivyo inavyokuwa..me pia juz kati walnipigia cm jion saa 11 kwaajili ya interview cku inayofuata saa 7 mchana dsm na mda huo nlikuwa tanga! ikabidi nipande bus alfajiri na nlipofika ubungo nkapitiliza direct kwenye hyo kampun yao na nlifika ontime namshukuru Mungu na nkafanya interview dk 20 nkasepa! huyo alienipigia cm nlijaribu kumuomba angalau anisogezee mda japo masaa 2 mbele..cha ajabu alichonijibu ni kuwa "we km uko mbali bora hata usije pumzika tu" tena kwa nyodo! ndo changamoto mama angu tuvumilie tu tunashida tutafanye sasa! pole lakn
 
Back
Top Bottom