frontline7
Member
- Sep 26, 2013
- 31
- 25
Mimi kama mwanafunzi wa social science nina haya ya kuwaambia wana jf.
Hali si nzuri utawala wa social science.
Wafanyakazi wanaowaudumia wanafunzi hapa, wengi wao wamesahau maadili ya kazi na wanatumia vibaya vyeo walivyopewa ili kuwasaidia wanafunzi. Kero huwa kubwa zaidi wakati wa usajili wa wanafunzi pamoja na kusaini mikopo. Wafanyakazi hawa wana kauli mbaya pamoja na vitisho.
Wakati mwingine wanafikia hadI hatua ya kukataa kusikiliza matatizo ya wanafunzi wakitumia kero na visingizio vya kipumbavu na visivyo na tija. (Mfano; kanyoe nywele, kaniandikie barua kwanini saini yangu haipo kwenye form yako..n.k) ilhali wanatambua fika kuwa wanaosoma hapa ni watu wazima na wanaojitambua.
Ushkaji ni mwingi sana hapa.. hata ukisema ni umeamua kuchukua hatua na kwenda mbali zaidi kuwasilisha kero zako, tunachoambulia ni kufukuzwa chuo. Wengi hatupo nao na sababu walikua mstari wa mbele kutetea maslahi ya wanafunzi na kukataa amri zisizo na tija.
Upatikanaji wa vyumba (hostel) umekaa ki rushwa-rushwa tu, ma warden wakiongoza kwa kuwa na usumbufu pamoja na kauli za vitisho kwa wanafunzi.
Kuna miungu watu humu, wakwanza ni madam aziza. Yeye neno lake ni sheria, hata kama sheria yenyewe haipo kwenye students by laws.
Hii ni kuwapa taarifa tu wale wanaohitaji kuja kusoma hapa watambue kua changamoto ni nyingi. Ukiachana na maudhi ya utawala, mazingira pia yana changamoto zake nyingi sana.
Kama kweli serikali ina mtazamo wa kukifanya chuo hiki kuwa chuo cha kimataifa, kuna mengi ya kufanya na kuna majipu mengi sana ya kutumbuliwa.
Kuna mengi ya kusema ila kwa sasa ni hayo tu.
...where we dare to speak openly and freely"